TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, August 25, 2014

Madini Migodini yapo Salama- Maswi

1.  Meneja wa Kampuni ya TANCOAL  (wanne kulia) Tan Brereton  na  Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo Emmanuel Constantinides (wa tatu kulia) wakimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi  na ujumbe wake namna shughuli za himbaji Makaa ya Mawe zinavyofanyika.
 Gari la kubeba kupakia Makaa ya Mawe likiendelea na kazi hiyo katika Mgodi wa Ngaka unaomilikiwa na kampuni TANCOAL.
 Mashine ya kusaga makaa yam awe katika viwango mbalimbali kulingana na mahitaji ya wateja ikiendelea na kazi ya kusaga mawe katika Mgodi wa Mkaa ya Mawe wa Ngaka unaomilikiwa kwa ubia na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Australia.
  Gari la kubeba makaa ya Mawe katika mgodi wa Ngaka likimwaga makaa sehemu maalum kutoka mgodini kabla ya kusagwa katika viwango mbalimbali kulingana na mahitaji y wateja.
 
=======  ========  ======
Madini Migodini yapo Salama- Maswi
Ø Aeleza TMAA wapo kuhakiki   mwenendo wa uzalishaji,uuzaji
Ø Mwekezaji  asisitiza Makaa ya Ngaka yana ubora wa juu
 
Na Asteria Muhozya, Mbinga
 
Katibu Mkuu  wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amewataka watanzania kuondoa dhana kuwa madini  yanayochimbwa katika migodi mbalimbali nchini yanaibwa  na wawekezaji wakubwa na kusisitiza kuwa, Wizara  kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), wapo katika migodi yote nchini kuhakikisha kwamba madini hayo hayatoroshwi .

Maswi  ameyasema hayo alipotembelea Mgodi wa kuchimba Makaa ya Mawe  wa kampuni ya  Tancoal eneo la Ngaka wilayani Mbinga inayomilikiwa kwa ubia kati ya Kampuni ya Australia na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kuongeza kuwa, TMAA wapo katika kila mgodi  kujua kiasi cha madini kinachochimbwa, kinachouzwa na kwa  ajili ya kuhakiki vyeti vya mauzo ya madini hayo kuhakikisha kuwa vinakwenda sambamba na kiasi cha mrahaba kinachotolewa na wawekezaji.

Kwa upande wake Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja alisisitiza hoja ya Katibu Mkuu Maswi na kuongeza kuwa, Wizara kupitia maafisa wa TMAA wamekuwa wakifanya ukaguzi kuhakikisha kwamba serikali inapata mrahaba stahili kupitia madini yanayouzwa na kutoa mfano kwa madini ya Makaa ya Mawe ya Ngaka kwamba serikali inapata asilimia 100 ya mrahaba.

“Nawapongeza sana TanCoal ni wasikivu, maafisa wa TMAA huwa wanafanya ukaguzi kila baada ya miezi mitatu kujua kiasi kinachozalishwa na kinachouzwa hivyo, tunakwenda nao vizuri,” alisisitiza Masanja.

Naye  Mkurugenzi wa Tancoal  Tan Brereton ameeleza kuwa,  mgodi wa wa Ngaka ni mradi mkubwa kwa Tanzania na kuongeza kuwa, uwepo wa mgodi wa makaa ya mawe wa Tancoal ni mafanikio na maendeleo makubwa kwa Tanzania kutokana na  kuwezesha ajira kwa wataalamu mbalimbali nchini ikiwemo serikali kupata kodi na mirahaba kupitia mgodi huo jambo ambalo litawezesha kuboresha huduma za kijamii.

Aidha, amezitaja faida  za nyingine za mgodi huo kuwa, uwepo wa Mgodi huo utawezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha nishati ya umeme kutokana na uwepo wa kiasi kikubwa cha makaa hayo katika mgodi wa Ngaka  na kueleza kuwa, makaa ya mawe kutoka katika mgodi huo yana ubora wa kiwango cha juu tofauti na madini yanayochimbwa nchini Afrika Kusini.

“Makaa ya Ngaka yana ubora wa hali ya juu sana tofauti na makaa ya nayochimbwa Afrika Kusini kwasasabu madini haya hayahitaji kusafishwa kabla ya matumizi tofauti na mengine ambayo husafishwa kabla ya kutumiwa ,alisisitiza Tan.

Aidha ameongeza kuwa,  kampuni hiyo ina uwezo wa kuzalisha kiasi cha tani  480,000  za makaa ya mawe kwa mwaka na kuongeza kuwa, tayari kampuni hiyo imesaidia huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo ya afya,shule ,maji na kuwaendeleza vijana na kutumia zaidi ya shilingi milioni mia sita na kuongeza kuwa, kampuni hiyo imekwisha toa kiasi za bilioni 2 kama kodi na mrahaba  kwa serikali.

Kwa mujibu wa Tan, ameeleza kuwa, makaa yanayozalishwa na kampuni hiyo yanatumika katika viwanda vya  saruji vya Mbeya Tanga Lake,  kampuni ya METL na viwanda vya karatasi viwanda vya nguo.

Pinda ataka urais

  • Atumia mgongo wa Ikulu na viongozi wa dini
  • Ataja watano watakaopenya Kamati Kuu, NEC
Pinda ataka urais 
WAKATI makada watano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakitumikia adhabu ya mwaka mmoja kwa kosa la kuanza kampeni za urais wa 2015 kabla ya muda, Waziri Mkuu Mizengo Pinda naye anadaiwa kutangaza kusudio la kuwania urais,
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Pinda alitangaza nia yake katika kikao cha wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kutoka mikoa sita ya kanda ya Ziwa, alichokiitisha juzi jioni Ikulu ndogo jijini Mwanza.
Katika kile kinachoonekana kama amepangwa rasmi kimkakati, Pinda aliwaeleza wajumbe hao kwamba hakuwa na nia ya kugombea lakini ameshawishiwa na baadhi ya maaskofu, masheikh, mkewe pia na anaungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete.
“Waziri Mkuu alituita juzi sisi wajumbe wote wa mkutano mkuu Taifa kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa. Tuliitikia wito tukakutana naye hapo Ikulu ndogo ya hapa Mwanza.
“Hakukomea hapo, bali alituambia kuna majina ya watu watano bora akiwemo yeye, Edward Lowassa, kijana, mwanamke na Mzanzibari kuwa ndiyo watakayopitishwa na Kamati Kuu kwenda NEC,” kilieleza chanzo chetu.
Ingawa Pinda hakupatikana kwa simu kuzungumzia madai hayo, ila mtoa taarifa hizo ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe walioshiriki kikao hicho, alisema kuwa kada huyo wa CCM alijivunia utumishi wake wa muda mrefu Ikulu tangu mwaka 1974.
Kwamba, alisema kuwa hatakuwa rais wa kutumia fedha chafu kuhonga wajumbe kama wanavyofanya baadhi ya wanasiasa wengine, bali atatumia fedha za marafiki zake kuwasaidia wale wote watakaomuunga mkono.
Inaelezwa kuwa kila mjumbe alipewa posho ya sh. 50,000 kwa ajili ya nauli, chakula na malazi kwa siku moja, kiwango ambacho hata hivyo kimelalamikiwa na wajumbe wakidai ni kidogo.
“Hadi makatibu wa CCM wilaya za mkoa wa Mwanza wamepewa maelekezo na kigogo mmoja wa mkoa ili wamuunge mkono Pinda katika safari yake ya kuutaka urais,” alisema na kuongeza;
Pinda amelazimika kukutana na wajumbe hao ili kujenga ushawishi kwao, kwa sababu anahofia nguvu kubwa ya kukubalika Lowassa ndani ya chama katika mbio hizo za urais 2015.
“Tulipomaliza kikao na Pinda pale Ikulu na kutoka nje, wajumbe wengi walipuuza mpango wake huo wakidai hafai kuwa Rais. Walisema kwanza yeye mwenyewe hana nia ya kugombea ila ameshawishiwa tu.
“Pili, wajumbe walihoji Pinda ni mjumbe wa Kamati ya Maadili, NEC na Kamati Kuu ya chama, aliyeshiriki kuwafungia Lowassa, Stephen Wassira, January Makamba, Bernard Membe, Fredrick Sumaye na William Ngeleja kwa miezi 12 kutokana na kukiuka taratibu na kaunza kamapeni mapema, kwamba yeye itakuwaje,” kilisema chanzo hicho.
Pinda aliingia jijini Mwanza juzi na kwenda kumhani Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga aliyefiwa na mtoto wake, Vedastus Kitwanga na jana usiku aliongoza harambee ya Taasisi ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, iliyofanyika jijini Mwanza. CHANZO >>>>>>

MAAMUZI YA MAHAKAMA JUU YA HOTELI YA SNOWCREST ARUSHA

???????????????????????????????
Moses Mashalla,
Mahakama kuu nchini kitengo cha biashara kanda ya Arusha imemuamuru mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa hoteli ya Snowcrest ya jijini Arusha,Wilfred Tarimo pamoja na familia yake kumlipa jumla ya $ 1.7 sawa na zaidi ya sh,3 bilioni mkurugenzi wa kampuni ya Grand Alliance Ltd,James Ndika kama malipo ya awamu ya kwanza ya kununua hisa ndani ya hoteli hiyo.Mbali na agizo hilo mahakama hiyo pia imeagiza washtakiwa wanne kati ya watano katika kesi hiyo  walipe  kiasi cha riba cha asilimia 4 ya fedha hizo  tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo na kiasi kingine cha asilimia 7 tangu kufungwa kwa shauri hilo hadi siku ya malipo.
 
Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Robert Makaramba mbele ya mahakama hiyo mara baada ya kueleza kuridhika na ushahidi uliowailishwa na upande wa mlalamikaji kupitia kwa wakili wake Melkizedek Lutema.
 
Katika kesi hiyo iliyopewa usajili wa nambari 9 ya mwaka 2012 Ndika alieleza kutapeliwa jumla ya $ 1.7 milioni  sawa na sh,3 bilioni baada ya kupatiwa hati mbili za eneo la hoteli hiyo lakini baadaye ilikuja kubainika kwamba eneo la hoteli hiyo lina hati tatu.
 
Katika hati ya madai mlalamikaji anadai kuwa hati moja kati ya tatu ilikuwa na mkopo wenye riba wa kiasi cha sh,1.5 bilioni kupitia benki mojawapo hapa nchini na baada ya kugundulika hilo ilikwamisha biashara ya mauziano ya hoteli hiyo.
 
Kwa mujibu wa nakala ya hukumu iliyosainiwa na Jaji Makaramba washtakiwa watano katika kesi hiyo mshtakiwa wa kwanza ,Wilfred Tarimo,Derick Tarimo,Doreen Tarimo ambaye ni mke wa mshtakiwa wa kwanza Irene Tarimo pamoja na kampuni ya Snowcrest And Wildlife Safaris Ltd  wameamriwa kumlipa Ndika fedha hizo pamoja na kiasi cha riba hadi tarehe ya kukazia hukumu.
 
Mbali na agizo hilo washtakiwa wote katika kesi hiyo pia waliamriwa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo  tangu ilipoanza kuunguruma huku wakipewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 30  tangu hukumu hiyo ilipotolewa.
 
Akihojiwa jijini Arusha wakili wa upande wa mlalamikaji,Lutema alisema kuwa wao wameridhika na hukumu hiyo na kwa sasa wanajiandaa kuwasilisha gharama za uendeshaji wa kesi hiyo tangu ilipoanza kuunguruma mnamo Januari 5 mwaka 2012.

MWIGULU AMSIMIKA SALIM ASAS KUWA KAMANDA WA VIJANA RINGA


MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas akisimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.
Mwigulu Nchemba akizingumza na umati wa watu katika viwanja vya mwembetogwa mwishoni mwa wiki mjini Iringa
MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas akizungumza na Wananchi mwishoni mwa wiki mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.
 Salim Abri Asas akiwa na Wazee wa Kimila kabla ya kusimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano.
 Shughuli za kusimikwa zikiendelea huku wanahabari wakiendelea kurekodi tukio hilo.

Na Denis Mlowe,Iringa

MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas mwishoni mwa wiki amesimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.

 Akimuapisha Asas kuwa Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM alisema analitumikia taifa hili akijua sehemu kubwa ya wananchi wake ni masikini na lengo kubwa ni kuwaondoa katika lindi la umaskini.


Nchemba alisema nchi inaliwa na moja ya eneo linalowaweka katika kazi kubwa ya mapambano ni fedha zinazotolewa kwenye halmashauri kwa ajili ya maendeleo ambazo hazitumiki ipasavyo na watendaji kwa kuzitumia katika miradi isiyo endelevu na kusababishia nchi kutokuwa na maendeleo.

“Kuna mambo mengi yanatokea katika halmashauri zetu kwasababu ya kukosa usimamizi unaosababisha watu wetu wakose hali ya kupata huduma zinazotakiwa kutekelezwa katika miradi ya maendeleo hivyo nitahakikisha kuwabana na kuwafuatilia kwa kila halmashauri kuleta mchanganuo wa fedha jinsi zilivyotumika na kuhakikisha mradi umekamilika na sio kusema kiasi Fulani kimetumika.”  Alisema Nchemba.
 
Aliongeza kuwa serikali inaendelea na mikakati ya kuwasaka, kuwakamata na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya dola watumishi wa umma wanaokula kodi za wananchi kwa mikono miwili bila kunawa.

Mwigulu alisema mambo mazuri yanakuja na serikali itaendelea kutengeneza sera  zinazojali watanzania ili keki ya taifa iliwe na watanzania wote na kudhibiti matumizi ya ovyo na fedha tutakazokuwa tunatoa hatutaruhusu zitumike kwa kazi tofauti na ile iliyokusudiwa.

Akimpongeza Asas kwa kuwa kamanda wa UVCCM, Alisema UVCCM wakitimiza wajibu wao ipasavyo watasaidia kupunguza maadui wakubwa wawili wa CCM ambao wameendelea kuwa na athari kubwa wakati wa chaguzi za serikali.

Aliwataja maadui hao kuwa ni pamoja na kujiingiza kwenye makundi ya wagombea na hila zinazosababisha baadhi ya wana CCM wasitendewe haki stahiki kwenye vikao muhimu vya chama.

Kwa upande wake Kamanda Salim Asas alisema baada ya kuapishwa kwa kipindi kingine lengo ni kuwainua vijana kiuchumi na kutaka ushirikiano katika kuleta maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Iringa bila kujali itikadi ya vyama na dini.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI AFANYA UTEUZI WA BARAZA LA MAWAZIRI, MANAIBU WAZIRI, WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA .

Mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na Uteuzi wa Naibu Waziri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na pia kumteuwa Naibu Waziri kama ifuatavyo-

(a) Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mamboya ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Suleiman Othman Nyanga.

(b) Mhe. Juma Duni Haji ameteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano akichukuwa nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Rashid Seif Suleiman ambaye sasa anakuwa Waziri wa Afya.

 (c) Mhe. Rashid Seif Suleiman ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya akijaza nafasi ya Mhe. Juma Duni Haji ambaye sasa anakuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano.

(d) Mhe. Mahamoud Thabit Kombo ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afya akijaza nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mamboya ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili.
Na pia amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Aidha, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya kama ifuatavyo:-
(1). Major Mstaafu Juma Kassim Tindwa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Bwana Pembe Juma Khamis.
(2). Bibi Mwajuma Majid Abdulla ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kusini, Pemba akijaza nafasi ilioachwa wazi na Major Mstaafu Juma Kassim Tindwa ambaye amehamishiwa Mkoa Kaskazini, Unguja.
(3). Bwana Omar Khamis Othman ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Pemba akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Bwa. Dadi Faki Dadi.
(4). Bwana Ayoub Mohamed Mahmoud ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bwa. Hassan Mussa Takrima.
(5). Bibi Hanuna Masoud Ibrahim ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake akijaza nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bibi Mwanajuma Majid Abdulla ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kusini, Pemba. Utezi huo umeanza leo tarehe 24 Agosti 2014.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI ZANZIBAR.

WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO

 Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
 Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro. 
Wakongwe wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro.

 Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakongwe wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro. 
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro.

‘MADINI HOUSE’ KUJENGWA ARUSHA, Kuwa na huduma za kibenki, Helkopita kutua moja kwa moja kituoni

Afisa Madini Mkaazi Tunduru Fredrick Mwanjisi (kushoto) akifurahia jambo wakati akimwongoza Katibu Mkuu Nishati na Madini Eliakim Maswi (wa pili kushoto) kutembelea eneo itakapojengwa ofisi ya Madini Tunduru. Wengine katika picha ni ujumbe wa Maafisa walioongozana na Katibu Mkuu na watumishi wa ofisi ya Madini Tunduru.
Jengo ambalo litatumika kama  Makao Makuu ya Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa Nyasa mjini Songea. Jengo hilo limenunuliwa na Wizara na litaanza kutumika mara baada ya ukarabati. Wengine katikati ni Kaimu MKurugenzi Idara ya Utawala Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Msika na wengine ni maafisa wWizara ya Nishati na Madini na Maafisa wa Madini Kanda waliofuatana na Katibu Mkuu.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja, (wa kwanza kushoto) akitafakari jambo mara baada ya kukagua kiwanja kitakapojengwa ofisi ya Madini ya Kamishna Mkaazi wa Madini, Nachingwea. Wa pili kushoto ni  Katibu Mkuu  Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, wa kwanza, wengine ni  Afisa Madini Mkaazi Nachingwea, Mhandisi Mayigi Makolobela (wa pili kulia) na wa kwanza kulia ni Mjiolojia kutoka ofisi ya Madini Mtwara.
=======   ========   =======

Na Asteria Muhozya, Songea
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini itajenga kituo maalum cha kuuza na kununua madini ya vito kutokana na nchi kuwa na hazina kubwa ya madini jambo ambalo pia litachangia katika kuyaongezea thamani madini hayo. 

 Masanja ameyasema hayo  mjini Songea wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Eliakim Maswi kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wizara ikiwemo kuonana na Makamishna Wasaidizi wa Kanda, Maafisa Madini Wakaazi, Watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania, kuangalia shughuli za wachimbaji wadogo wakiwemo wafanyabiashara wa madini na wawekezaji katika sekta ya madini. 

 Kamishna aliongeza kuwa, kituo hicho kitakuwa na huduma zote muhimu zikiwemo za kibenki ambazo zitawawezesha wachimbaji na wafanyabiashara kutokutafuta huduma muhimu zinazoendana na shughuli hizo nje ya kituo hicho. “Shughuli zote za uuuzaji na ununuzi madini ya vito na usonara zitafanywa katika kituo hicho. 

Kutakuwa pia na helkopita itakayotua moja kwa moja katika jengo hilo jambo ambalo litawezesha uwepo wa usalama katika biashara nzima ya kuuza na kununua madini,” alisisitiza Masanja. 

 Aidha, aliongeza kuwa, ili kuiwezesha sekta hiyo kupaa kwa kasi na kuchangia katika ukuaji wa uchumi, wizara imeamua kuanza kwa kuboresha ofisi za kanda za madini ikiwa ni pamoja na kununua maeneo maalum kwa ajili ya kujenga ofisi hizo ili kuboresha utendaji wa sekta ya madini nchini na kuwa na ofisi za uhakika. 

 “Tunataka kupitia sekta ya madini kuiwezesha serikali kuongeza mapato yake na kutoka hapa tulipo kiuchumi. Jambo hilo linawezekana ndio sababu tunaanza na kuboresha sehemu za kazi ili kuwawezesha watumishi kufanya kazi katika mazingira mazuri zaidi na kuongeza uwajibikaji,”aliongeza Masanja. 

Katika hatua nyingine, Kamishna Masanja amewataka Makamishna Wasaidizi wa Kanda na Makamishna Wakaazi walioteuliwa hivi karibuni kutimiza wajibu wao vizuri na kufikia lengo la makusanyo ambayo wizara imewapangia na kwa wale wasiotekeleza agizo hilo la makusanyo ndani ya kipindi cha miezi mitatu wataondolewa katika nafasi zao. 
“Tumeamua kupaa kupitia sekta hii, asiyeweza kutekeleza jambo hili kama tulivyokubaliana, tutamwondoa na kuwapa wengine wenye uwezo wa kufanya hivyo. Tunataka kufanya kazi kwa kasi na kisasa zaidi,” alisisitiza Masanja. 

Wakati huo huo, aliwata watumishi wote walioko katika ofisi za Kanda kuwa waadilifu, wawajibikaji, wawazi na wabunifu ili kuweza kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwemo kufuata sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma. 

Vilevile, aliongeza kuwa, wizara imejipanga kuanza kutumia mfumo wa kieletroniki kuanzia mwezi Septemba kwa ajili ya waombaji wa leseni jambo ambalo litasaidia kurahisisha zoezi la uombaji wa leseni na kuondoa manungu’niko miongoni mwa waombaji.

Sunday, August 24, 2014

Safari ya 40 ya Bibi Maarufu Mwananyalama A leo

Bibi kijino ni Bibi aliyekuwa maarufu sana katika mitaa ya Mwananyamala A kutokana na kuishi eneo hilo kwa Miaka Mingi Kitendo cha kuiteka Mwananyama, 
aidha inasemekana kuwa Bibni huyo aliyekuwa maarufu alikuwa Mcheshi na mtu wa kupenda kuzungumza na watu wa aina mbali kitendo kilichompatia Umaarufu Mkubwa.
Safari ya 40 Baada ya kifo chake imekamilika jijini Dar es Salaam leo Maeneo ya Mwananyamala A ambako ndiko alipoiacha Familia ya Watoto na Wajukuu wake akiwemo Mjukuu Wake Maarufu kwa Jina la Jasmini ambaye pia ni Mwanahabari katika Magazeti ya Babu Kubwa.

MWIGULU NCHEMBA USO KWA USO NA AJALI AKIELEKEA IRINGA.

Baadhi ya Watu wakiwa katika hali mbaya kutokana na ajali hiyo.

Na: Mwandishi Wetu
 
Jana Akiwa njiani kuelekea Iringa,Bahati mbaya anasema aliishuhudia ajali mbele yake ambayo kwa Uweza wa Mungu haikuleta Maafa yoyote kwa abiria na waendesha hivyo vyombo vya Usafiri.

Lakini hata hivyo pamoja na kwamba alikuwa katika safari zake za kikazi ilimrazimu kufanya jitiada za Uongozi ikiwa ni pamoja Kusimama kisha Kusaidia Majeruhi kabla ya hatua za Matibabu Makubwa Kuendelea kutoka sehemu husika.

Mwigulu anasema kuwa katika habari yake iliyotufikia moja kwa moja katika dawati letu la habari "Nashukuru niliweza Kutoa huduma ya Kwanza kwa Majeruhi hapo hapo na baadae kuwakimbiza Hospitali, Tudumishe Utanzania na Ubinadamu Wetu" anasema Mwigulu

aidha kutokana na kitendo hicho Mheshimiwa Mwigulu ameonyesha ni jinsi gani alivyo mtu wa Msaada kwa jamii kutokana na kwamba pia ameonyesha umuhimu wake kwa jamii kwani katika jamii yoyote inatakiwa Kiongozi kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yanayowakabili wananchi na siyo majukumu yanayoikabili Serikali.