TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, December 14, 2014

HOT NEWS…….NDOA YAVUNJIKA RASMI WAVUTANA KURUDISHIANA FEDHA WALIZOPOKEA.

Bwana harusi akiwa na mpambe wake kanisani wakimsubiri bibi Harusi
Jamaa wameshika vichwa hali haieleweki
Bi Harusi Naomi Ngoje akiwa amejilalia chumbani akiwa anahuzunika na kushangaa wazazi wake kurudisha mahali ya mchumba wake

HABARI zilizotufikia hivi punde kutoka nyumbani kwa familia ya Bi harusi ambayo ilikuwa ikipinga ndoa isifungwe kutokana na Bwana harusi kushindwa kumalizia sehemu ya Mahari zinadai kuwa ndoa imevunjwa rasmi na kilichobaki ni mzozo wa kurudishiana fedha.

Pande hizo mbili ya Kiume na Kike zimengia kwenye Mzozo na kuvutana kuhusu fedha baada ya Wazazi wa Mwanamke kukubali kurudisha fedha hizo pamoja na vitu walivyopokea huku kikubwa kikiwa ni upande wa Mwanaume kudai wapewe papo hapo.

Vitu vinavyodaiwa ni Fedha taslimu takribani Shilingi 310,000/= ambazo zilitolewa kwa ajili ya Mkaja pamoja na kiingilio, Blanketi na Mashuka.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao wako kila wakati unaokupa habari zisizoacha shaka kwa msomaji.

Na Shaaban Mpalule

Miss World finals 2014

miss-world_3137837kThe 2014 Miss World contest has been held at London’s ExCel centre. After parading in their national costumes, evening gowns and showing off their dance moves, the 120 women from around the globe were whittled down to one overall winner, Miss South Africa Rolene Strauss.Picture: Leon Neal/AFP

Wengi wajitokeza uchaguzi wa Serikali za Mitaa Katika Mkoa wa Katavi

unnamed2
Wasimamizi wa Uchaguzi wakielekeza namna ya kupiga kura wapiga kura walijitokeza kupiga kra mkoani Katavi Uchaguzi wa Seriklali za Mitaa.
(Picha zote na Kibada Kibada –Katavi)
………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada -Katavi
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Katika Mkoa wa Katavi umekamilika kwa wananchi kujitokeza kupiga kura kwa kufuata taratibu kanuni na sheria zinazoongoza uchaguzi wa serikali za Mitaa ingawa kulikuwa na changamoto cha hapa na pale kama kuchelewa kufika kwa karatasi za kupigia kura na vituo vingine uchaguzi kuahirishwa dakika za mwisho kutokana na Mgombea kukosa Sifa ya kugombea .
 
Akizungumzia kuahirishwa kwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nsanda Kata ya Ugalla kwa kile kilichoelezwa kuwa Mgombea kukosa Sifa ya kugombea baada ya kuwa kuwa amehukumiwa kifogo cha mwaka mmoja jela siku moja kabla ya uchaguzi hivyo kukosa sifa ya kuweza kugombea na nafasi hiyo kubaki wazi hadi hapo itakapotangazwa tena na mamlaka husika ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi Betwel Ruhega ameeleza kuwa kwa mjibu wa taratibu mgombea anapokuwa amepatikana na kosa la jinai na kuhukumiwa kifugo tena cha mwaka mmoja hivyo  anakuwa amepoteza sifa za kugombea uongozi  hivyo hafai kuwa kiongozi tena kwa mjibu wa taratibu.
 
Ruhega akaeleza kuwa aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kitogoji cha Nsanda amekosa sifa baada ya kufugwa na siku moja kabla ya uchaguzi hivyo nafasi hiyo kuwa wazi,kwa mjibu wa utaratibu inabidi kuahirisha ili kutoa nafasi kwa chama kupendekeza na kuteua jina la mgombea mwingine wa nafasi hiyo ya mwenyekiti.hivyo uchaguzi umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena kwa mjibu wa Kanuni taratibu na sheria za uchaguzi.sitanislau makungu chadema
A kaongeza kuwa maeneo mengine mambo yameenda kama yalivyopangwa na wananchi wamejitokeza kwa wingi kupiga kura na hivi wanasubiria matokeo.
Na taarifa zilizopatikana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Kata ya Mpandandogo wagombea nafasi ya Uenyekiti wa Kitongoji Igagala B’ wamegongana kura hivyo inabidi uchaguzi huo urudiwe upya.
Kwa Mjibu wa Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mpanda Charles Linda amesema wagombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Kitongoji  cha Igagala C Kijiji cha Igalala Kata ya Mpnda Ndogo wamegona kwa kupata kura sawa hivyo inabidi uchaguzi urudiwe upya .
 
Linda amewataja waliolingana kura kuwa ni  Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti kuptia tiketi ya CCM Isaya Daud  na Stanslaus Makungu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Katika hatua nyingine wapiga kura wa kituo cha kupigia kura Mnyagala walilazimika kusubiri kuanza kupiga kura majira ya saa nane mchana baada ya kuchelewa kuwafikia karatasi za kupigia kura  hivyo kurazimika kusubiri hadi zilipo fika karatasi hizo wakaanza kupiga kura.
Kwa Mjibu wa Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura Steven  Msomi alieleza kuwa wananchi walijitokeza tangu asubuhi kusubilia kupiga kura na hawakuchoka na hamasi ilikuwa kubwa hasa akina mama na vjiana wengi wamehamasika na kujitokeza kwa wingi.na hali ya usalama ni shwari.
Katika maeneo mengine Mkoani humo uchaguzi umeendeshwa kwa amani na usalama hadi kufungwa kwa vituo vya kupigia kura kullikuwa hakuna taarifa zozote zilizoripotiwa zinazohusiana na uvunjifu wa amani.

Matukio Msiba wa Mama Dotto, Kulwa na Nico Mwaibale Jijini Dar

  Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa Bi. Twitikege Mlagha Mafumu unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Bi. Twitikege Mlagha Mafumu enzi za uhai wake
 Baadhi ya waombolezaji wakitoa pole kwa ndugu na jamaa katika msiba wa  marehemu Bi. Twitikege Mlagha Mafumu, ambaye ni mama mzazi wa wanahabari Kulwa, Dotto na Nico Mwaibale Mbagala Kuu, jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba wa Bi. Twitikege Mlagha Mafumu unaofanyika jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba wa Bi. Twitikege Mlagha Mafumu unaofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa Bi. Twitikege Mlagha Mafumu unaofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Global Publishers Ltd (kushoto), wakitoa pole kwa familia ya wafiwa. 
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba wa Bi. Twitikege Mlagha Mafumu unaofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafiwa wakiwa katika msiba wa Bi. Twitikege Mlagha Mafumu unaofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa Bi. Twitikege Mlagha Mafumu unaofanyika jijini Dar es Salaam.

VIONGOZI WA UNESCO WALIPOTEMBELEA MIRADI NGORONGORO

unnamed5Kijana wa jamii ya kifugaji akiwa anawajibika katika kuwapatia malisho mifugo kama alivyobambwa na kamera hii wilayani Ngorongoro hili ni mmoja ya sifa ya hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro kuona mifugo ikiwa na wanyamapori bila kuwa na msuguwano kila mmoja akitafuta mahitaji yake wakiwamo wakazi wa jamii hiyo ya kifugaji.
unnamed9Wakazi wa kata ya Ololosokwan wakicheza pamoja na wageni wakati wa hafla hiyo ya kutembelea miradi ya UNESCO:
unnamed8Eneo la Kreta kama linavyoonekana nyakati za Asubuhi kama lilivyokutwa na kamera hifadhi ya ngorongoro huku watanzania wakitakiwa kupenda kutembelea vivutio hivi kukuza utalii wa ndani na kuipatia serikali mapato kwa maendeleo ya taifa unnamed7Wakitoa masaada wa pikipiki kwa serikali katika kuahakikisha kituo hicho cha utafiti wa kisanyansi kinapata usafiri wa kufika maeneo mbali mbali kwa urahisi na kurahisisha majukumu yao ya kila siku ya utafiti.

MGOMBEA CHADEMA MTAA WA MIGOMBANI SEGEREA, JAPHET KEMBO AWAGARAGAZA WAPINZANI WAKE KWA KUPATA KURA 510

Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Japhet Kembo akifurahia huku akipongezwa na wanachama na wapenzi wa Chadema mara baada ya kuibuka mshindi wa Kiti cha Mwenyekiti kwa Kupata Kura 510 huku CCM wakiwa wamepata kura 215 na NCCR kupata kura 205
 Mawakala wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Migombani wakihesabu kura ambapo sanduku hilo ndio lilikuwa sanduku la mwisho kuhesabiwa katika Kituo cha Kupigia kura cha Migombani ambao wakazi wa Mtaa wa Migombani walikuwa wakisubiria matokeo
  Askari Polisi wakiwa katika kituo cha Kupigia Kura cha Migombani kwaajili ya kuimarisha ulinzi na mpaka zoezi la kuhesabu kura likimalizika kwa Mgombea wa Chadema kuibuka Mshindi hakuna fujo zilizotokea.

 Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Migombani Wakisubiria Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani ambapo mpaka matokeo yanatangazwa Chadema iliibuka na Kura 510, CCM ikiwa imepata kura 215 na NCCR wakiwa na kura 205.

Baadhi ya wapita njia nao ilibidi wasimame maana uchaguzi huu ulivuta hisia za watu wengi kutokana na hali iliyoonyeshwa na wakazi wa mtaa huo kukaa mpaka dakika za mwisho
 Msimamizi wa Uchaguzi katika Kituo cha Kupigia Kura cha Migombani akitangaza Mshindi wa Uchaguzi huo uliomalizika kwa Mgombea wa Chadema akiwa ameibuka Mshindi kwa Kupata Kura 510 huku wapinzani wake wakiwa na Kura 215 za CCM na Kura 205 za NCCR

 Wakazi wa Mtaa wa Migombani wakishangilia ushindi mara baada ya Mgombea wa Chadema Kutangazwa Mshindi wa Kiti cha Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani
 Wakazi wakishangilia kwa Ushindi,
 Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Japhet Kembo (Kushoto aliyenyoosha mkono) akipongezwa na wakazi wa Mtaa wa Migombani kwa kuibuka Mshindi wa uchaguzi
 Wakazi wa Mtaa wa Migombani Segerea wakishangilia mara baada ya mgombea wao kuibuka mshindi katika kinyanganyiro hiko.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Baadhi ya matukio ya picha uchaguzi Serikali za Mitaa jijini Dar es salaam

unnamedMsimamizi wa Upigaji Kura Faudhia Mbawala akihakiki majina ya washiriki wa wapiga kura katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Hekima Buguruni,  unnamed1Msimamizi wa Upigaji Kura Faudhia Mbawala akihakiki majina ya washiriki wa wapiga kura katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Hekima Buguruni, wanaongalia kutoka kushoto ni Abasi Mzee wakala wa Chama cha Mapinduzi, Omary Issa Wakala wa CUF na Abubakari Said Wakala wa ADC,leo jijini Dar es Salaam.
unnamed2 unnamed3Wakazi Buguruni, Wilaya ya Ilala wakiwa katika foleni kwa ajili ya kupiga kura na kuweza kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Hekima, leo jijini Dar es Salaam unnamed4Wakazi wa Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala wakiwa katika foleni ya kuhakiki majina yao kwa ajili ya lupiga kura na kuweza kuwachaguwa viongozi wao wa Serikali za Mitaa katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Kimanga, leo jijini Dar es Salaam (Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)
unnamed5Wakazi wa Kariakoo Mashariki, Kata ya Kariakoo wakishiriki katika upigaji kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Lumumba katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam unnamed8Mkazi wa karikoo Mashariki , Kata ya Kariakoo akipiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Lumumba ,kwa ajili ya kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa Mitaa akiwemo Mwenyekiti na Wajumbe leo jijini Dar es Salaam.
unnamed9Msimamizi wa upigaji kura, Mwalimu Lucy Buzuka akitoa maelekezo kwa wapiga kura wa Kariakoo Mashariki, Kata ya Kariakoo jinsi ya kupiga kura katika zoezi la kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa ambapo siku ya leo jijini Dar es Salaam.

WANUSURIKA KUFA KWA AJALI UHASIBU TEMEKE

Baadhi ya mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
Polisi wa usalama barabarani akiwa eneo la tukio.
Ajali mbaya ya gari imetokea leo asubuhi eneo Temeke Uhasibu ikihusisha roli na gari dogo aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T399 BKU.Ajali hiyo imetokea kutokana na dereva wa gari dogo kuingia barabara kuu bila kuchukua tahadhari, Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Gari aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T399 BKU likiwa uvunguni mwa roli.

UPIGAJI KURA SERIKALI ZA MITAA JIJI LA ARUSHA WANEDNELA SHWARI

index
Na: Mahmoud Ahmad, Arusha
 
Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa,Vijiji na Vitongoji linaloendelea katika maeneo mbali mbali hapa nchini huku kwa upande wa mkoa wa Arusha hususani jiji la Arusha limekwenda salama bila ya kuwa na dosari zozote.
Jiji la Arusha ambalo huwa na heka heka ya matukio mbali mbali wakati wa kampeni hadi uchaguzi lakini uchaguzi huu wa serikali za mitaa umeenda salama huku wakazi mbalimbali wakijitokeza kutumia haki yao ya kikatiba kuwachaguwa wenyeviti wa serikali za mitaa.
Pamoja na yote licha ya tukio la mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema Kuchezea Kichapo na vijana wa mtaani almaarufu Chokoraa ambapo alilazimika kufyatua risasi tatu juu kuwatawanya vijana hao ambao walikuwa wakipigana kutokana na hali ngumu ya kusaka maisha na mbunge kulazimika kushuka kwenda kuamuaa ugomvi huo ndipo vijana hao walipoamua kuhamisha ugomvi wao kwa mbunge huyo
sakata hilo lilitokea siku moja kabla ya hitimisho la kampeni za uchaguzi huu hali imekuwa shwari katika jiji hili huku wakazi waliojiandikisha wakitumia haki yao kuwachagua wenyeviti wa serikali za mitaa na kesi ya Mbunge huyo aliechiwa kwa dhamana siku hiyo hiyo huku akizitaka mamlaka husika kuchukuwa hatua kwa vijana hao waweze kuishi kama jamii.
Moja wa wapiga kura katika Mtaa wa Giriki kata ya Sakina Izadin Salum alisema wananchi ndio wanawafahamu wagombea na wao watatumia haki yao kumchagua kiongozi anayewafaa bila ya kujali anatoka chama gani.
Alisema kuwa ameshiriki chaguzi mbali mbali hapa jijini Arusha na kukiri kuwa uchaguzi huu umerudia katika hali iyokuwa hapa kabla ya mwaka 2009 na kuwataka wakazi wa jiji la Arusha kuwachaguwa viongozi watakaosimamia maendeleo na kuacha malumbano yasio na lazima kwani watu wate wana haki sawa.
Kwa upandi wake msimamizi wa kituo cha Mitaa 200 kata ya Nagerenaro Regina Mfoi alisema kuwa hali katika kituo hicho ipo shwari na kila mtu anatumia haki yake kupiga kura na kuwa vifaa vipo vya kutosha kwa watu wote waliojiandikisha kupiga kura na hakuna malalamiko yoyote hadi sasa.
Mfoi alisema kuwa zoezi hilo kwenye kituo hicho limeenda salama bila ya manung’uniko yeyote na wakazi wa mtaa huo wamejitokeza kwa wingi kupiga kura bila ya matukio yeyote ya uvunjifu wa Amani.