Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wakiwa wamepanga mstari katika
moja ya Vituo vya kupigia kura kitongoji cha Mnyagala Kata ya Kabungu Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi.
Wasimamizi wa Uchaguzi wakielekeza namna ya
kupiga kura wapiga kura walijitokeza kupiga kra mkoani Katavi Uchaguzi
wa Seriklali za Mitaa.
(Picha zote na Kibada Kibada –Katavi)
………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada -Katavi
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Katika Mkoa wa Katavi umekamilika kwa wananchi kujitokeza kupiga kura
kwa kufuata taratibu kanuni na sheria zinazoongoza uchaguzi wa serikali
za Mitaa ingawa kulikuwa na changamoto cha hapa na pale kama kuchelewa
kufika kwa karatasi za kupigia kura na vituo vingine uchaguzi
kuahirishwa dakika za mwisho kutokana na Mgombea kukosa Sifa ya kugombea
.
Akizungumzia kuahirishwa kwa
uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nsanda Kata ya Ugalla kwa kile
kilichoelezwa kuwa Mgombea kukosa Sifa ya kugombea baada ya kuwa kuwa
amehukumiwa kifogo cha mwaka mmoja jela siku moja kabla ya uchaguzi
hivyo kukosa sifa ya kuweza kugombea na nafasi hiyo kubaki wazi hadi
hapo itakapotangazwa tena na mamlaka husika ya uchaguzi wa serikali za
mitaa.
Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi Betwel Ruhega ameeleza kuwa kwa mjibu wa
taratibu mgombea anapokuwa amepatikana na kosa la jinai na kuhukumiwa
kifugo tena cha mwaka mmoja hivyo anakuwa amepoteza sifa za kugombea
uongozi hivyo hafai kuwa kiongozi tena kwa mjibu wa taratibu.
Ruhega akaeleza kuwa aliyekuwa
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kitogoji cha Nsanda amekosa sifa
baada ya kufugwa na siku moja kabla ya uchaguzi hivyo nafasi hiyo kuwa
wazi,kwa mjibu wa utaratibu inabidi kuahirisha ili kutoa nafasi kwa
chama kupendekeza na kuteua jina la mgombea mwingine wa nafasi hiyo ya
mwenyekiti.hivyo uchaguzi umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena kwa
mjibu wa Kanuni taratibu na sheria za uchaguzi.sitanislau makungu
chadema
A kaongeza kuwa maeneo mengine
mambo yameenda kama yalivyopangwa na wananchi wamejitokeza kwa wingi
kupiga kura na hivi wanasubiria matokeo.
Na taarifa zilizopatikana kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Kata ya Mpandandogo wagombea nafasi ya
Uenyekiti wa Kitongoji Igagala B’ wamegongana kura hivyo inabidi
uchaguzi huo urudiwe upya.
Kwa Mjibu wa Afisa Uchaguzi wa
Halmashauri ya Mpanda Charles Linda amesema wagombea wa Nafasi ya
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Igagala C Kijiji cha Igalala Kata ya Mpnda
Ndogo wamegona kwa kupata kura sawa hivyo inabidi uchaguzi urudiwe upya .
Linda amewataja waliolingana
kura kuwa ni Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti kuptia tiketi ya CCM Isaya
Daud na Stanslaus Makungu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo.
Katika hatua nyingine wapiga
kura wa kituo cha kupigia kura Mnyagala walilazimika kusubiri kuanza
kupiga kura majira ya saa nane mchana baada ya kuchelewa kuwafikia
karatasi za kupigia kura hivyo kurazimika kusubiri hadi zilipo fika
karatasi hizo wakaanza kupiga kura.
Kwa Mjibu wa Msimamizi wa Kituo
cha kupigia kura Steven Msomi alieleza kuwa wananchi walijitokeza tangu
asubuhi kusubilia kupiga kura na hawakuchoka na hamasi ilikuwa kubwa
hasa akina mama na vjiana wengi wamehamasika na kujitokeza kwa wingi.na hali ya usalama ni shwari.
Katika maeneo mengine Mkoani
humo uchaguzi umeendeshwa kwa amani na usalama hadi kufungwa kwa vituo
vya kupigia kura kullikuwa hakuna taarifa zozote zilizoripotiwa
zinazohusiana na uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment