Mgombea
wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Kupitia tiketi ya Chama
cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Japhet Kembo akifurahia huku
akipongezwa na wanachama na wapenzi wa Chadema mara baada ya kuibuka
mshindi wa Kiti cha Mwenyekiti kwa Kupata Kura 510 huku CCM wakiwa
wamepata kura 215 na NCCR kupata kura 205
Mawakala
wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Migombani
wakihesabu kura ambapo sanduku hilo ndio lilikuwa sanduku la mwisho
kuhesabiwa katika Kituo cha Kupigia kura cha Migombani ambao wakazi wa
Mtaa wa Migombani walikuwa wakisubiria matokeo
Askari Polisi wakiwa katika kituo cha Kupigia Kura cha Migombani
kwaajili ya kuimarisha ulinzi na mpaka zoezi la kuhesabu kura
likimalizika kwa Mgombea wa Chadema kuibuka Mshindi hakuna fujo
zilizotokea.
Baadhi
ya wakazi wa Mtaa wa Migombani Wakisubiria Matokeo ya Uchaguzi wa
Serikali ya Mtaa wa Migombani ambapo mpaka matokeo yanatangazwa Chadema
iliibuka na Kura 510, CCM ikiwa imepata kura 215 na NCCR wakiwa na kura
205.
Baadhi
ya wapita njia nao ilibidi wasimame maana uchaguzi huu ulivuta hisia za
watu wengi kutokana na hali iliyoonyeshwa na wakazi wa mtaa huo kukaa
mpaka dakika za mwisho
Msimamizi
wa Uchaguzi katika Kituo cha Kupigia Kura cha Migombani akitangaza
Mshindi wa Uchaguzi huo uliomalizika kwa Mgombea wa Chadema akiwa
ameibuka Mshindi kwa Kupata Kura 510 huku wapinzani wake wakiwa na Kura
215 za CCM na Kura 205 za NCCR
Wakazi
wa Mtaa wa Migombani wakishangilia ushindi mara baada ya Mgombea wa
Chadema Kutangazwa Mshindi wa Kiti cha Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani
Wakazi wakishangilia kwa Ushindi,
Mgombea
wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Japhet Kembo (Kushoto
aliyenyoosha mkono) akipongezwa na wakazi wa Mtaa wa Migombani kwa
kuibuka Mshindi wa uchaguzi
Wakazi
wa Mtaa wa Migombani Segerea wakishangilia mara baada ya mgombea wao
kuibuka mshindi katika kinyanganyiro hiko.Picha Zote na Josephat Lukaza
wa Lukaza Blog
No comments:
Post a Comment