Na: Mahmoud Ahmad, Arusha
Zoezi la upigaji kura katika
uchaguzi wa serikali za mitaa,Vijiji na Vitongoji linaloendelea katika
maeneo mbali mbali hapa nchini huku kwa upande wa mkoa wa Arusha
hususani jiji la Arusha limekwenda salama bila ya kuwa na dosari zozote.
Jiji la Arusha ambalo huwa na
heka heka ya matukio mbali mbali wakati wa kampeni hadi uchaguzi lakini
uchaguzi huu wa serikali za mitaa umeenda salama huku wakazi mbalimbali
wakijitokeza kutumia haki yao ya kikatiba kuwachaguwa wenyeviti wa
serikali za mitaa.
Pamoja na yote licha ya tukio la mheshimiwa Mbunge wa jimbo
la Arusha Mjini Godbless Lema Kuchezea Kichapo na vijana wa mtaani
almaarufu Chokoraa ambapo alilazimika kufyatua risasi tatu juu
kuwatawanya vijana hao ambao walikuwa wakipigana kutokana na hali ngumu
ya kusaka maisha na mbunge kulazimika kushuka kwenda kuamuaa ugomvi huo
ndipo vijana hao walipoamua kuhamisha ugomvi wao kwa mbunge huyo
sakata hilo lilitokea siku moja kabla ya
hitimisho la kampeni za uchaguzi huu hali imekuwa shwari katika jiji
hili huku wakazi waliojiandikisha wakitumia haki yao kuwachagua
wenyeviti wa serikali za mitaa na kesi ya Mbunge huyo aliechiwa kwa
dhamana siku hiyo hiyo huku akizitaka mamlaka husika kuchukuwa hatua kwa
vijana hao waweze kuishi kama jamii.
Moja wa wapiga kura katika Mtaa
wa Giriki kata ya Sakina Izadin Salum alisema wananchi ndio wanawafahamu
wagombea na wao watatumia haki yao kumchagua kiongozi anayewafaa bila
ya kujali anatoka chama gani.
Alisema kuwa ameshiriki chaguzi
mbali mbali hapa jijini Arusha na kukiri kuwa uchaguzi huu umerudia
katika hali iyokuwa hapa kabla ya mwaka 2009 na kuwataka wakazi wa jiji
la Arusha kuwachaguwa viongozi watakaosimamia maendeleo na kuacha
malumbano yasio na lazima kwani watu wate wana haki sawa.
Kwa upandi wake msimamizi wa
kituo cha Mitaa 200 kata ya Nagerenaro Regina Mfoi alisema kuwa hali
katika kituo hicho ipo shwari na kila mtu anatumia haki yake kupiga kura
na kuwa vifaa vipo vya kutosha kwa watu wote waliojiandikisha kupiga
kura na hakuna malalamiko yoyote hadi sasa.
Mfoi alisema kuwa zoezi hilo
kwenye kituo hicho limeenda salama bila ya manung’uniko yeyote na wakazi
wa mtaa huo wamejitokeza kwa wingi kupiga kura bila ya matukio yeyote
ya uvunjifu wa Amani.
No comments:
Post a Comment