TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, December 21, 2014

TWIGA CEMENT YAZINDUA RASMI TIMU YA KOMBAINI YA MAKIPA WA LIGI KUU TANZANIA DHIDI YA TIMU YA KOMBAINI YA WAANDISHI WA HABARI TASWA F.C

Kikosi cha Timu ya Makipa walioshiriki katika Mchezo huo ni Fatuma Omari, Adam John Mahona, Helon Lupembe, Mstafa Ally mstafa(Baterzi), Benny Karama, Deogratius Munishi ‘Dida’. Abuu Hashim, Juma Kaseja, Shaaban Kado, Ivo Mapunda, na Kabal Faraji. wengine walioingia kuchukua nafasi ni pamoja na Mstafa Mabuluki, Hashimu Kizota, Ndizi Shomari, na Sarehe Malande,
Kikosi cha Timu ya Makipa walioshiriki katika Mchezo huo ni Fatuma Omari, Adam John Mahona, Helon Lupembe, Mstafa Ally mstafa(Baterzi), Benny Karama, Deogratius Munishi ‘Dida’. Abuu Hashim, Juma Kaseja, Shaaban Kado, Ivo Mapunda, na Kabal Faraji. wengine walioingia kuchukua nafasi ni pamoja na Mstafa Mabuluki, Hashimu Kizota, Ndizi Shomari, na Sarehe Malande,
Kikosi cha Timu ya Makipa walioshiriki katika Mchezo huo ni Fatuma Omari, Adam John Mahona, Helon Lupembe, Mstafa Ally mstafa(Baterzi), Benny Karama, Deogratius Munishi ‘Dida’. Abuu Hashim, Juma Kaseja, Shaaban Kado, Ivo Mapunda, na Kabal Faraji. wengine walioingia kuchukua nafasi ni pamoja na Mstafa Mabuluki, Hashimu Kizota, Ndizi Shomari, na Sarehe Malande,
 Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Kombaini ya Makipa( Chama cha Makipa) wakati wa Mapumziko
Wachezaji wa Timu ya Chama cha Makipa Tanzania, Muda Mfupi baada ya Kuwasili kwenye Viwanja vya Bora Kijitonyama.
  Na: Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Twiga Cement ya jijini Dar es Salaam, jana imefanikiwa kuzindua rasmi Chama cha Wachezaji wa Nafasi ya Golikipa wanaoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania, ambapo katika uzinduzi huo timu hiyo ya Makipa ilicheza mchezo wa Kirafiki dhidi ya Timu ya Kombaini ya Waandishi wa Habari TASWA F.C.uliofanyika kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na Ushindani wa Kipekee kutokana na Timu zote kuwa na Wachezaji Nyota na Tegemeo katika Vipaji vyao, Mashabiki waliofika kushuhudia mchezo huo walifurahishwa na jinsi kila mchezaji alivyoonyesha Ujuzi binafsi na kiwango cha hali ya juu.
 
timu ya makipa ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufanya shambulizi kwenye lango la timu ya TASWA ambapo dakika ya 26 mchezaji Shaaban Kado alikosa Penalt kutokana na beki wa Taswa Martin Peter kunawa akiwa eneo la kumi na nane na penalt hiyo ilidakwa na kipa nyota wa TASWA Ahmed Famau.
 
hadi kipindi cha kwanza kinamalizika kikosi cha timu ya Makipa kilikuwa mbele kwa bao 1-0,lililofungwa na Juma Kaseja baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa TASWA, ambapo kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko ambapo Taswa iliwatoa, Majuto Omary, Ibrahim Masoud, Ally Mkongwe, Zahoro Mlanzi, Shafii Dauda, na nafasi zao kuchukuliwa na Salum Jaba, Juma Ramadhani, Hatibu Naheka,na Paul Limoy,mabadiliko ambayo hata hivyo yalishindwa kupunguza kasi ya wachezaji hao Makipa wa Ligi kuu waliokuwa muda wote wakilisakama lango la TASWA FC.

pamoja na kuwa na wachezaji wa akiba timu ya Makipa lakini walishindwa kufanya mabadiliko, kutokana na wachezaji wengi kuwa na pumzi ya kuwamudu TASWA ambapo Makipa hao walisaidiwa na mlinda mlango kutoka timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars, Fatuma Omary ambaye hata hivyo alionyesha kiwango kikubwa baada ya kudaka michomo ya wazi kutoka kwa washambuliaji wa Taswa,Ibrahim  Masoud, Shafii Dauda,Majuto Omary pamoja na Ally Mkongwe waliokuwa wakilisakama Lango la timu ya makipa kila wakati.

goli la pili lilipatikana kunako dakika ya 67 kupitia kwa Ivo Mapunda aliyefunga kwa shuti kali lililomshinda mlinda wa TASWA  Ahmed Famau,kabla ya shaaban Kado kuhitimisha Kapu la Magoli kwa timu hiyo ya Makipa.
 
 Pamoja na Kufungwa kwa Taabu 3-0 timu ya TASWA FC, iliweza kuwachezesha mputa mputa wachezaji hao nyota wa Ligi kuu pamoja na kwamba wachezaji hao muda mwingi wanakuwa kwenye Mazoezi Makali na Timu zao za ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,kitendo ambacho kiliwafanya kuonekana wakiwa na Uhai wa kukimbiza huku na kule katika kipindi cha dakika zote za mchezo.
 
Taswa ambayo kwa asilimia kubwa iliwachezesha wachezaji wake wengi ambao ni wafanyakazi wa vyombo mbali mbali vya habari, ilisifiwa na mashabiki waliohudhulia mchezo huo kwa kuwa Muda mwingi wanakuwa katika shuguli za kiofisi ambapo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Timu hiyo wachezaji ukutana mara moja kwa wiki kwa ajili ya mazoezi ya Pamoja.
 
"timu yetu ni nzuri sana hii TASWA, mwenyewe umeona wachezaji walivyowapeleka mpuata hawa Makipa pamoja na kwamba hii timu ya Makipa ni Wachezaji wa ligi kuu, nasema ligi kuu kwa kuwa wanashiriki hiyo ligi isipokuwa tofauti wao ni makipa, na tunapozungumzia suala la Wachezaji, mwenyewe unajua timu ili iwe bora ni lazima kwanza iwe na Makipa wazuri ndipo iwe bora, na kipa bora ni yule anayeweza kuwapanga wachezaji wake, hivyo kama hawa wachezaji ndiyo wapangaji wa timu zao wakati wa Mashindano, mimi nasema tumecheza na Timu ya Taifa na si kama unavyofikili wewe, na ndiyo maana nathubutu kusema kuwa kufungwa kwetu mabao 3-0 ni sawa na kupata ushindi sisi, maana hata hivyo wametuleta kwenye Uwanja wao, nadhani wakati wa mchezo wa Marudiano bila shaka itakuwa zamu yetu kuibuka na ushindi maana leo wameshinda wao na mpira ni mchezo wa mmoja kushinda, asiyekubali kushindwa siyo mshindani" alisema majuto
 
na kuongeza kwamba mchezo huo kwa pande zote mbili umewapa changamoto ya kuifanya sasa timu hiyo ya Kombaini ya Makipa kutambuliwa kote Nchini.
"mkakati uliopo sasa ni kuhakikisha kwamba timu hii inazunguka kwenye Majiji Makuu kwa ajili ya kufanya michezo yake ya kirafiki na timu za Mikoa, lakini lengo kubwa ikiwa ni kuwapa Fursa wakazi wa Maeneo hayo kuwatambua zaidi hawa Makipa wetu, lakini pia wakati wachezaji hawa wakiwa kwenye hayo maeneo ya Majiji watakuwa na jukumu la kuwaandaa wachezaji wengine zaidi vijana katika nafasi za kipa ili kuweza kuwa na Makipa wengi zaidi kwa ajili ya Faida ya Taifa letu la Tanzania" alisema Majuto
 
Naye kocha wa Taswa FC Ally Mkongwe wakati akizungumza na wachezaji wa timu zote alisema kuwa ni jambo la kufurahisha ambalo limeweza kufanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuwa lengo ilikuwa ni kufanya uzinduzi na timu zote zimeweza kucheza kwa hali kubwa bila vurugu wala kuonyeshana mchezo mbaya.
 
"tumefurahi sana, niwapongeze wachezaji wote yaani Makipa na Taswa, jambo hili si la mzaha kama tulivyofikili hapo mwanzo, lakini kumbe mwitikio wa watazamaji ulikuwa ni mkubwa sana na wengi wamekuja kuwatazama wachezaji na Waandishi wa habari, Watangazaji, na wakati umefika tukae tuangalie namna ya kuboresha mahusiano haya yawe ya kudumu baina ya TASWA na timu hii ya Kombaini ya Makipa wa Ligi kuu, isipokuwa tusameheane kwa yale Mapungufu madogo yaliyotokea maana sisi ni binadamu lakini wakati mwingine nadhani hayatatokea kwa pande zote mbili endapo yametokea kwa mchezo wa leo" alisema Mkongwe.
 
Hata hivyo wachezaji hao Makipa wametakiwa kufanya jitihada za kuhakikisha wanakuwa chachu ya kuleta Makipa wengine nyuma yao kutokana na kwamba nafasi ya Makipa kwa Tanzania inazidi kupungua kutokana na nafasi hiyo kuwa ngumu ukilinganisha na nafasi za wachezaji wengine wa ndani ambao wanakuwa ni wengi.
 
Naye mmoja wa Makocha wasaidizi wa timu ya TASWA Ibrahim Masoud aliwaasa wachezaji hao kuwa kioo kwa wenzao na kuwa kishawishi cha kuwapata vijana wengine watakaokuwa makipa wa Tanzania miaka ijayo"Sina Mengi ya Kusema kwa kuwa Kocha na Mwenyekiti wameeleza kwa kirefu lakini mimi niko tofauti kidogo na wenzangu, kikubwa hapa mimi ni kuhusu nyie Makipa wetu, kumbukeni kwamba nyinyi kina Kaseja, Ivo Mapunda, Shaaban Kado, Dida, mstafa na nyinyi wote, nyie sasa mnaelekea Ukingoni, ni kama kina Mwameja wakati wao, kina Manyika, Mfaume,nk, walikuwapo lakini walipopotea hao makipa Tanzania iliyumba sana kuwapata nyinyi, na hiyo inatokana na kwamba Wachezaji wengi Makipa hawapati Fursa ya kuandaliwa, na niwatake sasa kutumia mwanya huu kwa kuwa tayari mmekuwa ni makipa Hodari kuhakikisha kwamba wakati wa Mapumziko ya Ligi, muweze kuingia Darasani kwa ajili ya kupata ujuzi wa kuwa Walimu wa Makipa, Kila mmoja kwa wakati wake lengo mtakapomaliza muda wenu wa kuitumia Tanzania katika Soka, muweze kuwa walimu wazuri na wazalishaji wazuri wa Makipa wengine" alisema Ibrahim Masoud(Maestro)
 
Kwa Upande wao Makipa hao wao hawakuwa na la kusema isipokuwa kwa niaba ya wachezaji wote wa Makipa Ivo Mapunda alisema kuwa wanashukuru kwa Sapoti kubwa kutoka Chama cha TASWA, ambao mara zote wamekuwa mstari wa mbele kuwapa maelekezo, kitendo kilichowaweka karibu zaidi hata wakati wa Uzinduzi wa Chama hicho cha Magolikipa," Sisi binafsi tumefurahi kukutana na timu hii ya TASWA, maana kiujumla wachezaji wengi wa Taswa wanafahamu mpira, ila tumewafunga kutokana na kukosa Pumzi tofauti na sisi wengi tunafanya mazoezi kila siku na timu zetu tena timu kubwa za ligi kuu, mimi Kesho( Leo) naelekea Zazibar Kambini, kujiunga na Timu yangu, kwa hiyo unaona jinsi mchezo huu ulivyokuwa ni muhimu sana kwetu hata nimeshindwa kuongozana na wachezaji wazangu pamoja na Mwalimu wangu kutaka nisicheze hii leo lakini nimemkatalia kwamba ni lazima nijumuike na Makipa wenzangu kwenye jambo hili la Umoja, maana sasa sisi Makipa pia tumekuwa ndugu wa karibu na Marafiki wa Kweli, zama za kale kwamba huyu na huyu aziivi eti kwa kuwa wote ni Makipa imepitwa na wakati, utatukuta mimi, Kaseja, Kado, Dida, Mstafa, na wengine tukizungumza na kufurahi pamoja, sisi siyo maaduni ni marafiki tena niwapongeze Wadhamini wa Mpambano huu(Uzinduzi) Kampuni ya TWIGA CEMENT kwa kufanya jambo hili, limezidi kutuweka karibu zaidi, na naamini kwamba watazidi kutuunganisha na kuandaa michezo Mingi zaidi kwa ajili ya kuwapa Raha wakazi na mashabiki wetu Mikoani" alisema Ivo Mapunda

 Akizungumzia mchezo huo Afisa Masoko wa TWIGA CEMENT,Alex Gideon, alisema kuwa maandalizi yamekwenda kama walivyopanga isipokuwa mkanganyiko umetokea kwenye eneo dogo la Uwanja, ambapo awali mchezo huo ilikuwa ufanyike kwenye uwanja wa KARUME kwa mujibu wa Matangazo yaliyofanywa na vyombo vya habari,

 " sitaki kulizungumzia sana suala la mkanganyiko wa Uwanja, lakini nadhani TFF katika hatua za mwisho imeshindwa kuruhusu mchezo wetu kufanyika kwenye viwanja vyao ambako vyombo mbali mbali vilitangaza, hivyo mashabiki wengi walifika Karume, na nichukue fulsa hii kuwataka radhi sana wote waliotufuata kwenye viwanja vya Karume, mchezo wetu ulibadilishwa uwanja kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu na kwa kuwa ni TFF wenyewe waliopanga hatua za Mwisho Mchezo wa Ligi daraja la kwanza kufanyika humo hatukuwa na kipingamizi, ni jambo la kimchezo na ukizingatia ni ligi yetu pia sisi watanzania hivyo hilo niombe radhi kwa mashabiki wetu wote, lakini kuhusu wadhamini wetu kama ulivyoona mwenyewe wamejitaidi na huu ni mwanzo na maandalizi yamefanyika kwa siku chache zana, wakati ujao tutaboresha na kulifanya jambo hili kuwa la kudumu na lenye kuleta tija ya Maendeleo kwa hawa Makipa wetu, kingine niwapongeze TASWA kwa ushirikiano wao maana wametufariji na kutupa sapoti kubwa"
 alisema Alex Gideon

aidha mchezo huo ulikuwa kwa ajili ya kujenga mahusiano mema baina ya timu zote, wachezaji pamoja na kufanya Uzinduzi wa Chama cha Makipa Tanzania, waandishi na Makipa wanaocheza ligi kuu Ya Vodacom Tanzania.

UJENZI WA MABWENI SHULE ZA PEMBEZONI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WANAFUNZI MIJINI.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

Jamii imetakiwa kuendelea  kuunga mkono juhudi za Serikali za ujenzi wa mabweni katika shule  za Sekondari  zilizoko pembezoni mwa miji hasa maeneo ya vijijini ili kukabiliana na tatizo la msongamano wa wanafunzi mijini linalosababishwa na baadhi ya wanafunzi kushindwa kujaza nafasi wanazopangiwa   maeneo ya pembezoni mwa miji kutokana na umbali.

Kauli hiyo ilitolewa juzi jijini Dar es salaam na Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando wakati akizungumza na viongozi wa Elimu wa mkoa na walimu wakuu wa Shule za Sekondari za mkoa wa Dar es salaam wakati wa kikao cha Kamati ya Uchaguzi wa wanafunzi wa watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015.

Alisema  mwaka huu  mkoa wa Dar es salaam umekuwa na kiwango cha juu cha ufaulu  kitaifa kwa kuwa na wanafunzi wanaokidhi vigezo vya kuendelea na masomo ya sekondari kwa kiwango cha asilimia 78 ukifuatiwa na mkoa wa Kilimanjaro ambao umepata asilimia 69.

Alifafanua kuwa kati ya wanafunzi 60,709 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka huu , wanafunzi 59,577 ambao ni sawa na asilimia 98.14  waliofanya mtihani huo, wavulana wakiwa 28,419 na wasichana 31,158.

Bi. Mmbando alibainisha kuwa  kati ya hao watahiniwa 1,132  sawa na asilimia 1.86 katika mkoa wa Dar es salaam hawawakuweza kufanya mtihani huo kutokana sababu mbalimbali zikiwemo utoro, vifo, ugonjwa na sababu nyinginezo.

Akizungumzia  kuhusu ufaulu wa wanafunzi hao kimkoa alisema wanafunzi 46,434 sawa na asilimia 78 walifaulu mtihani huo na kuufanya mkoa wa Dar es salaam kuongoza kwa kuwa na ufaulu wa juu kitaifa wavulana 22,389 na wasichana 24,086.

Alibainisha kuwa wanafunzi 36,610 walichaguliwa katika chaguo la kwanza kujiunga na shule mbalimbali za Sekondari za ndani na nje ya mkoa wa Dar es salaam na kufafanua kuwa wanafunzi 9824 waliobaki sawa na asilimia 21 ambao nao wamefaulu watachaguliwa katika chaguo la pili kufuatia baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa katika chaguo la kwanza kujiunga na shule zisizokuwa za serikali na nafasi zao kubaki wazi.

Katika kufanikisha zoezi hilo Bi. Mmbando alieleza kuwa mkoa tayari umeunda timu tatu zitakazofuatilia idadi ya wanafunzi watakaoshindwa kufika katika shule walizopangiwa  kuanzia Januari 14, 2015 katika halimashauri za Temeke, Ilala na Kinondoni ili nafasi zao zijazwe na wanafunzi wengine.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Raymond Mapunda akitoa tathmini ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika nchi nzima mwezi Septemba mwaka huu alisema mkoa wake ulifanya vizuri kutokana na juhudi za walimu pamoja na wanafunzi kuuelewa vizuri mfumo wa ufanyaji mitihani uliotumika wa Optical Mark Reader (OMR).

Alisema kuwa wanafunzi wa shule 506 za jiji la Dar es salaam walifanya mtihani walitumia mfumo huo kwa ufanisi mwanafunzi 1 alifutiwa matokeo yake kwa sababu za udanganyifu, 2 walipata alama 0  huku  wavulana 10 na wasichana 10 kutoka wilaya ya Ilala na Kinondoni waliibuka washindi wa nafasi 10 bora kitaifa.

NSSF YATOA ZAWADI KWA MAMENEJA WAKE

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau, akimkabidhi zawadi Meneja Mwandamizi wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa NSSF ya Gambia, Bw. Baboucarr nyan (kushoto) na Meneja wa Idara ya Bima wa shirika hilo Gambia, Bw. Edward Somez. walipokuwa nchini kwa mafunzo maalumu ya wiki mbili, Dar es Salaam juzi.  (Na Mpigapicha Wetu)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau, akiwakabidhi zawadi maofisa wawili kutoka NSSF Gambia,  Meneja Mwandamizi wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Bw. Baboucarr nyan (kushoto) na Meneja wa Idara ya Bima kutoka shirika hilo, Bw. Edward Somez, waliokuwa nchini kwa mafunzo maalumu ya wiki mbili, Dar es Salaam juzi. (Na Mpigapicha Wetu)

KILICHOTOKEA MSITU WA MAFINGA IRINGA MCHANA WA LEO.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjNbRTftD0cJERshA7m-pJpa-mbWrryCvslGZ-yIl4oSKM8r2uyB4dBjfM2p3CwElJNJBZMJz-yHXQYQEy8-p96FAiyCsHpU1T3rhDjB7lLHSkqSjbj0Fh-gUfvo9-gj78bCiohyX-3lXYR/s1600/unnamed+(1).jpg
Chanzo inasadikika kuwa ni mwendo kasi na gari kuacha njia  kwa sababu ambazo bado hazijajulikana na kupinduka.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0no8NJjZc-jftl1pxxagolqDTun76rL_npfzpP1xefEEXHhjhyphenhyphen_9L6kx-y6E3-cypQh3aE318JBsz3AfWIQ1GiVqP9p1aohOXf8qvzGFSzkH8ypWLJnehvm7C1jbhbH6nir9FrzMgro2W/s1600/unnamed.jpg
Wakati Mkoa wa Iringa unaadhimisha wiki ya usalama barabarani yenye kauli mbiu maamuzi yako barabarani ni hatima yetu - fikiri kwanza - Ajali mbaya imetokea katika msitu wa miti wa Mafinga Iringa mchana huu.
 Kwa mujibu wa Mpasha habari wetu ni kwamba mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Yunith Gwamaka Mwakenja ndiye pekee aliyepoteza maisha  , Dereva wa gari hilo ambaye ni mhadhiri wa chuo cha Tumain makumira Tawi la Mbeya Bw Gwamaka Mwakenja yeye amepata majaraha lakini  pia  majeruhi mwingine ni Joyce Fredy. Abiria Wengine waliokuwa katika safari hiyo wametibiwa na kuruhusiwa.

TUKIO LA UJAMBAZI,MLANDEGE ZANZIBAR

MKUU wa Polisi Wilaya ya Mjini, Ali Makame (wa pili kushoto) akiangalia gari iliyovunjwa na kuibiwa pesa zinazosadikiwa kuwa ni euro elfu moja na shilingi za kitanzania milioni tano, muda mfupi baada ya kufika eneo la tukio katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar.
ASKARI Polisi wakiwa wameizunguka gari iliyovunjwa na kuibiwa pesa zinazosadikiwa kuwa ni euro elfu moja na shilingi za kitanzania milioni tano, tukio hilo limetokea majira ya saa saba mchana katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar leo. Mmiliki wa gari hiyo aliegesha gari yake na kuingia msikitini kwa kusali sala ya Ijumaa katika msikiti jirani na maengesho ya gari katika eneo la mlandege. 
(Picha na Haroub Hussein).

BREAKING NEWSS::MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA MAGEREZA HAYA HAPA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI (Jeshi la Magereza)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, anawatangazia wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Jeshi la Magereza baada ya kufaulu mitihani ya usaili iliyofanyika kati ya tarehe 10 Desemba, 2014 hadi 17 Desemba, 2014 katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam pamoja na wale wa Kidato cha Nne na Sita waliosailiwa kutoka Kambi mbalimbali za JKT.

Wahusika wote wanatakiwa kuripoti Ofisi za Magereza za Mikoa husika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2014 tayari kwa safari ya kwenda Chuo cha Mafunzo ya Awali kilichopo Kiwira Tukuyu Mkoani Mbeya. Mafunzo yatafunguliwa rasmi tarehe 8 Januari, 2015 hivyo mwisho wa kuripoti Chuoni ni tarehe 7 Januari, 2015. Yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa tarehe ya mwisho iliyotamkwa kwenye tangazo hili hatapokelewa na atarudishwa kwa gharama zake.

Wahusika wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
 
i. Vyeti halisi vya masomo na kuzaliwa, vikiwa na nakala 5 za kila cheti,
ii. Picha za rangi(pass-port size) 5 za hivi karibuni,
iii. Fedha taslim Tzs.90,000/=,
iv. Kalamu za wino, kalamu za risasi na madaftari ya kutosha,
v. Chandarua cheupe cha duara ft 31/2, shuka nyeupe mbili, mto wenye foronya nyeupe zisizo na maua/maandishi,
vi. Cheti cha Afya kutoka Hospitali ya Serikali, 
vii. Nguo za kiraia za kutosha, sweta, raba (brown au nyeusi) na soksi, 
viii. Kwa wale wenye kadi za bima za afya waje nazo, na
ix. Kila mwanafunzi atajitegemea kwa nauli ya kwenda.
 
Tangazo hili linapatikana kwenye Mbao za Matangazo zilizopo Bwalo Kuu la Magereza, tovuti ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.go.tz sanjari na blog ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.blogspot.com

Imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza.

J.C. Minja
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
Bofya hapo chini kuona majina ya waliochaguliwa kwa mchanganuo ufuatao:-

Waziri Mkuu awasili Qatar kwa ziara ya kikazi

index
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewasili jijini Doha, Qatar jana usiku (Jumamosi, Desemba 20, 2014) kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo inayotarajiwa kuanza leo.
Lengo la ziara ya Waziri Mkuu ni kukuza mahusiano baina ya nchi hizi mbili, kuangalia fursa za kiuchumi na miradi mikubwa inayoweza kuzinufaisha nchi hizo na nje ya mipaka yake kwenye Ghuba ya Arabuni (Arabian Gulf) na bara la Afrika.
Vile vile Waziri Mkuu anatarajiwa kutangaza fursa za uwekezaji nchini Tanzania, fursa za biashara, za utalii na kutafuta mitaji kwa ajili ya sekta za uchimbaji gesi na mafuta, usindikaji mazao, uvuvi na mifugo, ajira na uendelezaji miundombinu.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri Mkuu atakuwa na mazungumzo ya kiserikali na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani. Vilevile atakutana na Mawaziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii; Uchukuzi; Miundombinu na Uwekezaji wa nchi hii. Naibu Mawaziri atakaokutana nao ni wa Uchumi na wa Nishati.
Vilevile Waziri Mkuu amepangiwa kukutana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Qatar (Qatar Business Community), wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Qatar (Chamber of Commerce of the State of Qatar) na pia atakutana na Watanzania waishio Qatar. Atatembelea pia Mamlaka ya Bandari ya Qatar na makao makuu ya kampuni ya uchimbaji gesi ya Qatar.
Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kimani; Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Maalim; Naibu Waziri wa Nishati, Bw. Charles Kitwanga; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi.
Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, wabunge wawili Bi. Amina Makilagi na Bw. Aeshy Hilali na wakuu wa taasisi za TPSF na TPDC.

Hazina SACCOS yakadhi hati za viwanja ambavyo ni rasmi zaidi kwa 150 kwa wanachama.

unnamed 
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kulia) akiwasili viwanja vya Mkumbusho ya Taifa mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa siku mbili (Disemba 20-21) wa wanachama wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina, mkutano huo unaongozwa na kauli mbiu isemayo “Viwanja Rasmi Suluhisho la Makazi Bora”. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Eligius Mwankenja.
unnamed1 
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa siku mbili mwishoni mwa wiki (Disemba 20-21) wa wanachama wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina, mkutano huo unaongozwa na kauli mbiu isemayo “Viwanja Rasmi Suluhisho la Makazi Bora”.
unnamed4 
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Eligius Mwankenja akitoa neno wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofaviwanja vya Mkumbusho ya Taifa mwishoni mwa wiki (Disemba 20-21) jijini Dar es salaam.
unnamed5
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum wakati wa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofaviwanja vya Mkumbusho ya Taifa mwishoni mwa wiki (Disemba 20-21) jijini Dar es salaam.
unnamed6
Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofaviwanja vya Mkumbusho ya Taifa mwishoni mwa wiki (Disemba 20-21) jijini Dar es salaam.
unnamed8
Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofaviwanja vya Mkumbusho ya Taifa mwishoni mwa wiki (Disemba 20-21) jijini Dar es salaam.
unnamed10

NGUNI KUPIGWA JANUARI 2 IFAKARA UKUMBI WA MAKUTANO

  Na Mwandishi Wetu
 
MPAMBANO wa ngumi wa kufungua mwaka unatarajia kupigwa Ifakara mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuhamasisha na kukuza mchezo wa masumbwi nchini. akizungumza na waandishi wa habari promota wa mpambano huo Hiari Bohari amesema kuwa kwa sasa anataka kuaendeleza mchezo wa masumbwi Ifakara kwa kuwa watu wapo na mchezo unapendwa
Aliongeza kwa kusema siku hiyo ya januari mbili itakuwa ni siku ya kufungua mwaka kwa mpambano wa masumbwi kati ya Abdallah Kilima na Abdul Amwenye huku Saleh Makuka akipambanma na Said Chamak
Vile vile kutakuwa na mapambano mawili kwa ajili ya kuhamasisha wanawake washiriki katika michezo ya ngumi siku hiyo Aika George atapambana na Najma Ally
Aliongeza kwa kusema anawaomba wadau mbalimbali kutoa sapoti na kumuunga mkono katika harakati za kuinua mchezo wa masumbwi wilayani Ifakara ili uweze kusonga mbele

MADIWANI MPANDA MKOANI KATAVI WAFANYA ZIARA MWANZA

unnamed
Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Ilemela mwenye T,shirti ya njano Fabiano  akiwaongoza madiwani kutoka Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi kujifunga masuala ya uendeshaji wa Mwalo hapo wanaeelekea kuangalia samaki jinsi wanavyohifadhiwa  kisha kusindikwa wasioze na kusafirishwasokono kwa walaji.
Picha zote na Kibada Kibada-Mwanza ziara ya Madiwani)
unnamed0
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi mwenye Shati ya kijani mpauko Yasini Kibiriti akiwaongoza madiwani wenzeka ziara ya Kutembelea soko la samaki katika Mwalo  uLIOKO Halmashauri ya Manispaa ya Ilemele kujifunzanamna ya uendeshaji wa mwalo katika Halmashauri yake baada ya kujengwa soko la kisasa Tarafa ya Karema Kata ya Ikola.
…………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada.
Maadiwani wa Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi wafanya ziara mkoani Mwanza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na kujifunza mambo mabali mbali ya uendeshaji wa Mwalo wa Ikola iliopo katika Halmashauri hiyo.
  Ziara hiyo pia i kutoka Idara ya Mifugo na Uvuvi,wajasiliamali  kutoka  Kati ya Ikola ulipojengwa mwalo wa Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi ambao shughuli zake bado kuanza kazi.
Katika ziara hioyo walipokea taarifa za kuhusu uendeshaji mgawanyo wa madaraka na sura nzima ya uongozi wa mwalo kwa kuwa watakuwa na uongozi wao kamili.
 
Soko hilo kwa mjibu wa Afisa  Uvuvi wa Hamalshauri ya Manispa ya Ilemera aalieleza kuwa lilijengwa kwa ufadhi wa serikali ya japani na limegaharimu kiasi cha zaidi ya shilingi Bilion Sita.
 Na linahudumia watu wa aina mbalimbali ndani na nje ya Nchi.
Akaongeza kuwa mahitaji ya dagaa ni mkubwa sana katka nchi za uarabu,hata hivyo akaeleza kuwa katika soko hilo la mwaloni wapo wafanyabiarasha kutoka Nchi ya Kidemokrasi ya Kongo DRC,Burundi,Kenya ,Uganda na Rwanda igawa mahitaji ya soko la samaki na dagaa ni makubwa mno katika nchi za wenzetu.

KITUO CHA RADIO 5 WAFANYA KAMPENI YA USHINDI KWA WATOTO YATIMA

SAM_0388
Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 Arusha wakikabidhi misaada mbalimbali katika kampeni ya “USHINDI”inayoendeshwa na kituo hicho,misaada hiyo ilitolewa na wahisani mbalimbali kwaajili ya watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima Mkoani Arusha,katika Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo kushoto ni Sarah Keiya wakiwakabidhi watoto wa kituo cha kiwohede ndoo ya mafuta ya kupikia kwaajili ya sikukuya Krismass na mwaka mpya jijini hapa jana katika hotel ya world Garden
SAM_0393
Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha kiwohede na huruma katika hotel ya world Garden iliyopo moshono jijini Arusha katika tam
SAM_0390
Mkuu wa vipindi wa kituo hicho Mathew Philip akikabidhi moja ya msaada kwa shcha watoto huruma
SAM_0363
Watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima wakishindana kucheza muziki
SAM_0376
Grace Joseph(12)wa kituo cha Kiwohede akionyesha ujuzi wake wa kucheza katika shindano
SAM_0400
Mtoto anayeishi katika mazingira magumu akiwa jukwaani akiimba wimbo wa “NISEME”wimbo wa Ya moto band
SAM_0358
Mashindano yakiwa yanaendelea
SAM_0361
Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa mzigoni
SAM_0385
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba moja katika shindano la kucheza muziki
SAM_0384
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba mbili baada ya kushinda katika shindano la kucheza muziki
SAM_0364
SAM_0346
Wafanyakazi wa redio5 wakiwa wanaanda sausage kwaajili ya watoto yatima
SAM_0352
Muonekano wa watoto wakiwa katika eneo la kuchezea michezo mbalimbali
SAM_0350
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Bi.Vicky Mwakoyo akiwa na  Meneja masoko wa Redio 5Bi.Sarah Keiya
SAM_0366
Mtangazaji wa kituo hicho Akiba Kilango ambaye alikuwa MC wa shughuli hiyo akiwa anaongea na watoto jukwaani kabla ya mashindano ya kucheza kuanza
SAM_0371
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anafatilia tamasha hilo
Kampuni Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi katika vituo lenye jina “Kampeni ya USHINDI”linalowashirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Arusha
Mkurugenzi wa kituo hicho  Robert Francis anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha sikukuu ili nao wasijione kutengwa
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao ni wale wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na tukifanya hivi watajiskia vizuri
Meneja masoko wa Redio 5 Sarah Keiya ametoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana na kituo hicho kwa kuwezesha kampeni hiyo kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio 5,Pepsi,Fifis bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful company,World garden.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)