TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 5, 2014

HAPANA CHEZEA WEMA SEPETU WEWE:ANGALIA PICHA 20 ALIVYOWAFANYIA PARTY KAJALA MASANJA NA B 12

OLYMPUS DIGITAL CAMERA Mastaa wawili Hamisi Mandi maarufu kama B12 na Kajala Masanja ambao wote ni marafiki na wote wawili na share siku moja ya kuzaliwa. Leo ndiyo ilikuwa birthday yao ambapo Kajala Masanja alianza kwa kupeleka misaada kwa watoto yatima na baadaye kuungana na B12 kwenye party waliyoandaliwa na Wema Sepetu nyumbani kwa Wema. Kutoka bossngasa.com tunawatakiwa maisha mema na marefu wote wawili na hizi hapa ndiyo picha zenyewe ambapo shughuli nzima ilitanguliwa na futari. CONTINUE READING






Wema Sepetu akimlisha keki B12

Zamu ya Kajala ilifika

Kulikuwa na keki zaidi ya nane kama unavyoziona

Hapa B12 akiwa kwenye futari ambayo iliandaliwa na Wema Sepetu

Wadau,ndugu na marafiki ambao walialikwa na Wema Sepetu

Kutoka Fish Crub anaitwa Lamaar

Kajala Masanja,Zamaradi Mketema,Wema Sepetu

Hii keki ndiyo iliyotia fora kwenye party
Add caption
Keki hii kutoka kwa Wema kwenda kwa Kajala

Keki nyingine kwa ajili ya Kajala

Nyingine tena kwa ajili ya Kajala

Kutoka kwa Wema kwenda kwa B12
`
Add caption
Kajala Masanja aliletewa keki za kutosha siku hii

Hawa ndiyo watoto waliozaliwa siku hii

Beautiful people
OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Hapa ilikuwa ni lights,camera then Instagram
OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Wema akiongoza wimbo wa happy birthday
OLYMPUS DIGITAL CAMERA

B12 akimlisha keki mfanyakazi mwenzake wa Clouds media group Zamaradi Mketema

SAUDIA YAIPATIA SERIKALI YA TANZANIA ZAIDI YA SH. BILIONI 45 KUBORESHA HUDUMA ZA JAMII NCHINI


 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana hati ya  mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania waliosaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
 Baadhi ya waandishi wa habari na watumishi wa wizara ya Fedha pamoja na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia wakiwashuhudia Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
 
04/12/2014
Serikali ya Tanzania imesainiana  mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya  shilingi bilioni 45.2 na Shirika la Maendeleo la Saudia kwa lengo la kuboresha miradi wa maji kwa wilaya ya Same, Mwanga na ujenzi na ukarabati wa barabara Visiwani Zanzibar.

Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.

Akiongea na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Waziri Saada alisema kuwa kati ya mkopo huo shilingi bilioni 41.25 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 25 zitagharimia mradi wa maji katika wilaya za Same na Mwanga na  shilingi bilioni 3.96 kwa ajili ya maradi wa barabara Pemba, visiwani Zanzibar.

Waziri Saada alilishukuru Shirika la Maendeleo la Saudia kwa jitihada zao za kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kautatua tatizo la maji wilaya za Same na Mwanga pamoja na uboreshaji wa barabara katika visiwa vya Pemba.
 
Aidha, mradi wa maji wa Same- Mwanga utagharimu Dola za Kimarekani milioni 110.34 ambazo benki ya BADEA, Shirika la Maendeleo Kuweit, OPEC na mashirika mengine wamekubali kukamilisha sehemu ya fedha iliyobakia.

Mradi wa maji wa Same- Mwanga baada ya kukamilika utasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji vijijini amabapo utasaida kuboresha hali ya maisha wa wananchi wa maeneo hayo, upatikanaji nwa maji safi na salama kwa maendeleo ya afya za wakazi hao na kuboresha uchumi wao kwa kutumia muda mwingi kwa shuighuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas amesema kuwa makataba waliosaini leo unaonesha kuwa Saudi Arabia iko mstari wa mbele katika kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wake kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa wizara ya Fedha na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia.

LITAZAME JIMBO LA MBUNGE ALIYESIMAMA KUTETEA WEZI WA ESCROW JINSI LINAVYOKABILIWA NA UMASIKINI WA KUTISHA



MHE  ASUMPTA  MSHANA
Miongoni mwa wabunge  wa ccm ambao walichangia mambo  ya kwenye sakata la ESCROW ni huyu mama wenzake wanachangia kwa uchungu pesa zetu zimeibiwa yeye analeta ushabiki usiyokuwa na maana kwenye ishu za msingi , ni  aibu  san  kwa  mama  kama  huyu  kusimama  na   kutetea  wezi  wakati jimbo  lake  la  NKENGE  linakabiliwa  na  umasikini  wa  kutisha.

LAKINI   TAZAMA   HALI  HALISI  YA  JIMBO  LAKE  JINSI  WANANCHII  WAKE  WANAVYOKABILIWA  NA  UMASIKINI  MKUBWA   TENA  WA  KUTISHA  LAKINI  BILA  AIBU  BADO  ANAPATA  KIBURI   CHA  KUSIMAMA  KUWATETEA  MAFISADI








watu  wanaishi  kwenye  nyumba  hizi

HIKI  NI  CHOO


h
Hivi  kwa   hali  hii  mtu  unapata wapi  uwezo  wa  kusimama  na  kutetea  wezi  wakati  bado   wananchi  wako  wanaishi  kwenye  umasikini??

KAMA MNALITAFUTA JOKA BASI HUYU ESCROW NI YAI MOJA TU, JOKA LENYEWE BADO HALIJAKAMATWA !!!.



Kwa namna ninavyoona mambo yanakwenda Watanzania tusipokuwa makini tutakuwa watu wa matukio, watu wanaoendeshwa kwa matukio, kama tukikubali hali hiyo itakuwa jambo baya sana kwa taifa letu. 

Matukio kama haya huwa ni matokeo ya chanzo fulani, matukio haya huwa ni chanzo cha udhaifu wa mifumo yetu ya udhibiti pahala fulani. Kwa sababu haiwezekani jambo likishatokea ndio tuulizane ilikuwa kuwa vipi, nafuatilia mjadala wa Bunge ninaona kila anayezungumza ama anasema mtu au taasisi fulani alipaswa kujua.


Haya mambo hayakufanyika kwa kutumia mbinu za kijasusi, mbinu ambazo hutumia intelijensia ya hali ya juu kiasi kwamba hata kama ulikuwa mlinzi anayelinda lango lakini mtu akapita katika lango hilo pasina kuonekana. Jambo linaloendelea kujadiliwa bungeni wala halikutokea kwa kificho au kutumia intelijensia ya hali ya juu kufanya wanaotuhumiwa kutenda wasijulikane kwa namna yoyote, la hasha.


Hii inanipeleka katika hoja nyingine kwamba, unapoona katika nchi yenye utawala wa sheria, mchana kweupe mambo makubwa na ya kutisha hasa yale yenye nasaba na ubadhirifu wa mali ya umma yanafanyika mchana kweupe basi hatupaswi kusubiri kuona mawingu kujua mvua itanyesha.


Ninayaandika haya kwa maana ya kujifunza, hata kama tungepata Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri wazuri kiasi gani, kama mifumo ya utawala wa nchi haijashonwa vema na kwa umadhubuti kikatiba kazi yao njema ingeishia katika jitihada zao za kibinadamu na kukosa usaidizi wa mifumo na taasisi za kikatiba. Binadamu kwa asili amekuwa kiumbe ambaye bila kujitungia kanuni huwa ni msumbufu kabisa, hata kama binadamu ni mwema kiasi gani, iwapo ataishi katika mazingira yasiyo na kanuni basi wema wake utakuwa hatarini kughiribika.


Katika ulimwengu wa leo utaratibu wa kuenenda katika jamii na Taifa lolote lile ni Katiba na sisi tumeamua kuandika Katiba Mpya na Bora. Ni Katiba Mpya na Bora ndiyo pekee inaweza kuwa silaha ya mwisho kuliangamiza joka ambalo limekuwa likitaga mayai kama vile Epa, Majengo ya Benki Kuu, Richmond na haya ni mayai ambayo tumeyaokota kweupe, bado hatuna hakika ya mayai ambayo joka ameyataga kwenye mashimo, vichakani na mayai ambayo joka huenda akayataga hivi karibuni tena. Sumu ya joka ni Katiba Mpya ambayo inatuwezesha wananchi kutumia mamlaka yetu kuiwajibisha Serikali, Bunge na Mahakama. Nchi ambazo zilipuuza kushughulika na joka kikatiba zimeishia kuwa mataifa yaliyoshindwa “failed states”. Tusikubali kufika huko.


Matukio ya escrow na Katiba
Nitumie pia fursa hii kutoa rai yangu kwa Watanzania kwamba, kuwa na Katiba Bora na inayotungwa na wananchi ndiyo mwarobaini wa kuziba mianya ya ubadhirifu katika Taifa letu. Kuwa na Katiba Bora ndiyo itakuwa salama yetu katika kuona wale tuliowapa dhamana wanawajibika haraka iwezekanavyo pindi tuhuma za ubadhirifu zinapotokea katika maeneo na mamlaka yao.


Sikiliza na usome pia, kwa namna ambavyo mjadala wa sakata hili umejipambanua katika Bunge letu la Jamhuri je, unadhani, viongozi wetu hawa watadiriki kwenda kutunga masharti makali na magumu ya kuwawajibisha viongozi wanafanya ubadhirifu wa mali ya umma, ilhali wao wenyewe ni viongozi wa umma wakati huo?


Nikuoneshe kidogo Rasimu ya Warioba ilisema hivi katika suala la Maadili na Miiko ya Viongozi na Watumishi wa Umma, akiwa katika kazi za ofisi au kazi binafsi au wakati amejumuika na watu wengine, atahakikisha kwamba mwenendo wake: hauruhusu kutokea mgongano wa masilahi kati ya masilahi binafsi na maslahi ya utumishi wa umma; hauhatarishi masilahi ya umma kwa ajili ya masilahi binafsi; au haushushi hadhi ya ofisi anayofanyia kazi. (2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kusimamia utekelezaji wa masharti yanayohusu kanuni za uongozi wa umma. (3) Wadhifa wa “Kiongozi wa umma” kama ulivyotumika katika Sehemu hii utajumuisha viongozi wa kuchaguliwa (hii inamaanisha Rais, makamu wa rais, wabunge, madiwani n.k) na kuteuliwa (Mfano, mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu na manaibu wao, wakurugenzi wa idara za Serikali n.k) kama watakavyoainishwa kwenye sheria za nchi.


Ibara hii pamoja na mambo mengine imefutiliwa mbali na Katiba Inayopendekezwa na zaidi ya yote masharti yake mahususi yakielekezwa kutungiwa sheria na Bunge. Hebu nikuulize tena, juzi ijumaa Bunge ilibidi liahirishwe baada ya wabunge kushindwa kutengeneza sentensi ya pendekezo la hatua za kuchukuliwa kwa wale ambayo wanatuhumiwa katika sakata la escrow, unadhani wabunge hawa watakaa na kutunga masharti mahususi na makali yatakayowabana na kuwawajibisha wao dhidi ya ubadhirifu ambao huenda baadhi yako wakaja kuufanya hapo baadaye? Jambo la kuhuzunisha zaidi hata ile Ibara ndogo ya 2 inayosema Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kusimamia utekelezaji wa masharti yanayohusu kanuni za uongozi wa umma hakuna tena.


Yaani tunarudi kule kule ambako Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma isiyo na meno ambayo wananchi waliipigia kelele sana kwamba kuna tuhuma nyingi kuliko masuala yanayoshughulikiwa na sekretarieti hiyo na hasa hasa wananchi wakaweka msisitizo kwa wale watuhumiwa wakubwa wakubwa.


Matukio ya escrow na maadili
Masharti mahususi yafuatayo kuanzia 203(2)(b)(e) hadi (o) yamefutwa kutoka katika Rasimu ya Warioba na hayamo katika Katiba Inayopendekezwa.


(2) Bila ya kuathiri masharti ya jumla ya ibara ndogo ya (1), majukumu mahususi ya Tume yatakuwa ni: (b) kufanya upekuzi kwa kushirikiana na taasisi nyingine; (e) kutoa ushauri juu ya masuala ya ubadhirifu wa fedha kwa mamlaka husika; (f) kufanya upekuzi kwa kiongozi wa umma anayepewa dhamana kabla ya kuingia madarakani; (g) kutoa elimu kwa umma kuhusu maadili na miiko ya viongoziwa umma; (h) kufanya uchunguzi kwa uamuzi yake yenyewe, au baada yakupokea malalamiko kutoka kwa mtu yeyote, kutokana nakutenda au kutokutenda kwa kiongozi wa umma au mtumishi (i) yeyote wa umma, au wakala wa Serikali, ikiwa kitendo kilichotendwa au kutokutendwa ni kinyume cha maadili ya umma; (j) kumwelekeza, baada ya kupata malalamiko au itakapoona inafaa, kiongozi wa umma au mtumishi wa umma, taasisi auwakala wa serikali au chombo chochote cha umma kufanya jambo lolote linalotakiwa na sheria, kuacha, kuzuia au kusahihisha utendaji mbaya au usiyo sahihi wa majukumu yake;


(k) kutoa ushauri kuhusu kuchukuliwa hatua kiongozi wa umma au mtumishi wa umma; (l) kumwelekeza kiongozi wa umma au mtumishi wa umma, kwa mujibu wa sheria za nchi, kutoa nyaraka zinazohusiana na matumizi ya ofisi, matumizi ya fedha au mali za umma, au kutoa taarifa ya matumizi mabaya kwa Tume, kwa hatua stahiki; (m) kuomba msaada au taarifa muhimu kutoka kwa mamlaka yoyote ya Serikali au binafsi katika kutekeleza wajibu wake,na kukagua kumbukumbu muhimu na nyaraka husika; (n) kwa kuzingatia sheria, kutangaza kwa umma, mambo yote yanayohusiana na uchunguzi uliofanywa na Tume, iwapo mazingira yanaruhusu; (o) kuchunguza jambo au mazingira yoyote yanayokiuka au kusababisha ukiukaji wa maadili.


Ninapofuatilia sakata hili sishangai sana kwanini masharti haya mahususi yameondolewa na badala yake Katiba Inayopendekezwa ikasema katika ibara yake ya 231(3) kwamba “Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Ibara hii”.


Mtu yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu na anayependa kuona tunasifika kwa vivutio vya kitalii na siyo ufisadi kwa hakika atahakikisha Katiba Inayopendekezwa inaboreshwa na kurudisha masharti haya muhimu. 

Aidha, ikumbukwe kwamba ili Katiba Inayopendekezwa iboreshwe Sheria ya Kura ya Maoni inasema katika kifungu chake cha 35, kwamba Katiba Inayopendekezwa ikipata kura za “hapana” itakuwa ni fursa ya kuiboresha kabla haijapelekwa katika duru ya pili ya Kura ya Maoni.

. IPTL SASA YAMGEUKIA KAMISHNA MKUU WA TRA KWA KUITAKA MAHAKAMA IMKAMAT


Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi
 

Dar es Salaam. Kampuni za Pan Africa Power Solution Tanzania Limited (PAP) na Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), zimewasilisha maombi ya kutaka Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) akamatwe kwa kukiuka amri ya Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB) kwa kufuta Hati za Malipo ya Kodi za Mauzo ya Hisa (Capital Gain Certificate).  

Kampuni hizo mbili, ambazo ziko kwenye mgogoro wa umiliki, ndizo zinahusika kwenye sakata la uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya kuuza umeme unaofuliwa na IPTL, kwa Shirika la Umeme (Tanesco), wakati wa kusubiri uamuzi wa mahakama katika kesi ya kupinga tozo hilo.
 

PAP, ambayo inadai imenunua hisa zote za IPTL, ndiyo iliyolipwa fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti hiyo na kuamsha mjadala mkubwa bungeni ulioisha kwa Bunge kufikia uamuzi wa kuwawajibisha kisheria wote waliohusika, wakiwemo mawaziri.
 

Lakini uamuzi huo wa Bunge haukuwa tamati la sakata hilo baada ya kampuni hizo mbili kukata rufaa TRAB dhidi ya Kamishna wa TRA na Msajili wa Kampuni na Leseni (Brela) zikipinga kusudio la kufuta hati hizo.
 

Jana kampuni hizo mbili ziliwasilisha maombi ya hati ya kutaka Kamishna Mkuu wa TRA akamatwe, zikidai kuwa amepuuza amri hiyo iliyomzuia kutekeleza azma yake ya kufuta Hati za Malipo ya Kodi ya Mauzo ya Hisa.
 

Katika maombi hayo walalamikaji hao wanadai kuwa licha ya TRAB kutoa zuio hilo Novemba 26, 2014, Kamishna Mkuu wa TRA, ambaye ni mlalamikiwa wa kwanza, alitoa amri ya kuziondoa hati hizo siku iliyofuata, yaani Novemba 27, 2014, bila kujali amri hiyo.
 

Walalamikaji hao pia wanaiomba TRAB, baada ya kumkamata Kamishna Mkuu wa TRA, itoe amri afungwe kwa kudharau amri halali iliyotolewa na bodi na pia imwamuru akidhi matakwa ya amri ya TRAB ya Novemba 26.
 

Pia walalamikaji hao wanaiomba TRAB imwamuru mlalamikiwa huyo, kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hilo pamoja na amri nyingine ambazo itaona kuwa zinafaa.
 

Maombi hayo ya PAP na IPTL ya hati ya kumkamata na kuamuru Kamishna Mkuu wa TRA afungwe yamepangwa kusikilizwa leo na Katibu wa TRAB, Respicius Mwijage.
 

Hati ya kiapo inayounga mkono maombi hayo inaeleza kuwa mlalamikiwa, akiwa ni raia wa Tanzania, siyo tu kwamba alipaswa kuwa mtiifu kwa mamlaka ya bodi hiyo, bali pia alipaswa kutekeleza sheria za nchi ambazo bodi hiyo ni sehemu yake.
 

Hati hiyo ya kiapo ya mkurugenzi wa operesheni wa IPTL, Parthiban Chandrasakaran, inaeleza kuwa kwa kitendo hicho cha kutotii amri ya bodi hiyo, mlalamikiwa amepoteza sifa ya kuwa mtumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 

Pia inaelea kuwa kama bodi hiyo isipotumia mamlaka yake kukubali maombi hayo ya kutoa amri inayoombwa, basi walalamikaji watapata hasara isiyoweza kufidiwa.
 

Inafafanua hasara hizo kuwa ni pamoja na kodi nyingine ambazo tayari PAP wamelipa TRA kwa ajili ya kuendesha biashara.
 

Pia hati hiyo ya kiapo inafafanua kuwa kuondolewa kwa hati hizo kutahatarisha biashara ya walalamikaji ambayo wamekuwa wakiiendesha tangu walipota hati hizo.
 

Inaendelea kueleza kuwa kwa kuwa walalamikaji wako katika hatari ya kuvunja mkataba na Shirika la Umeme (Tanesco), na wadau wengine, jambo hilo litasabaisha vita ya kimahakama na hivyo kulipa fidia zisizo za msingi.
 

Hati hizo namba 004965600 na 0049657 zilitolewa na TRA Desemba 23, 2013, kwa ajili ya uuzaji wa hisa baina ya kampuni ya Mechmar Corporation (Malaysia) Berhard iliyokuwa ikimiliki asilimia 70 ya hisa za IPTL na Piper Links Investment Limited na kati ya Piper Link na PAP.
 

Hata hivyo baadaye, Novemba 19, 2014 TRA ilitoa taarifa ya siku sita kwa Brela ikionyesha kusudio la kuziondoa hati hizo kwa madai kuwa mkataba wa madai ya mauzo ya hisa hizo ulikuwa ni mkataba wa makubaliano ya uongo.
 

Wakati Huohuo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kitendo cha kushindwa kuwachukulia hatua wanaotuhumiwa kuchota Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow hadi sasa, ni ishara ya kuwa na Serikali dhaifu.
 

Mbowe, ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema viongozi waliotuhumiwa kwenye kashfa hiyo walitakiwa wawekwe kando kabla ya hatua zaidi.
 

“Leo (jana) ni siku ya tano na Rais Kikwete ameshindwa kutoa uamuzi wowote. Hii inaonyesha jinsi tulivyo na Serikali dhaifu,” alisema Mbowe wakati akihutubia mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Kata ya Vijibweni, Kigamboni.
 

“Hadi leo Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka bado yupo ofisini na anasaini nyaraka mbalimbali za viwanja. Inakuwaje hadi leo wezi bado wapo ofisini?” Kwanini wanalindwa?” alihoji. 
 
“Wanapewa muda wa kukaa ofisini kujipanga ili hata Rais Kikwete atakapochukua uamuzi, wawe wamejipanga na kuchukua kidogo kilichokuwepo.”
 

Mbowe alisema sakata la Escrow lilitikisa nchi na kwamba kitendo cha watuhumiwa kutochukuliwa hatua hadi leo tafsiri yake ni kwamba viongozi wa Serikali wanalindana.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kuongoza Bonanza la michezo ya Vyuo vya elimu ya kati

-zito entertainment kutikisa kibaha

Njuweni Institute of hoteli- wenyeji wa bonanza hilo.

Na: Mwandishi Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh, Mwantumu Mahiza siku ya jumamosi wiki hii anatarajia kuongoza Bonanza la Wanavyuo linaloendea sehemu mbali mbali na ikiwa ni sehemu ya tatu kwa kanda ya kaskazini inayoendelea lwemye viwanja mbali mbali chini ya Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania  &  Entertainment C.o Ltd .

Bonanza hilo ambalo ni kwa ajili ya kupata timu zitakazoshiriki michuano ya NACTE, linafanyika na kuambatana na Sherehe za kwanza za Mahafali ya mkoa wa pwani kwenye viwanja hivyo vya shirika mla elimu huku gumzo kubwa ikiwa ni timu ya wauguzi kutoka chuo cha COTC mkoa wa Pwani.
 timu mbali mbali za Viongozi wa Serikali pia zinashiriki katika michezo ya soka, kikapu,netball pamoja na Voleyball kwa lengo la kuleta changamoto kwa Mkoa wa pwani ambao wamefurahishwa na uwepo wa michezo hii ya vyuo vya elimu ya kati.

Akizungumzia bonanza la jumamosi Mratibu wa Michezo Vyuoni, Mpalule Shaaban alisema kuwa Mh, Mwantumu anatarajia kufanya Uzinduzi wa Michezo hiyo kwa Mkoa wa Pwani kutokana na kwamba sasa Michezo hiyo itafanyika kila mwaka Sehemu mbali mbali za Tanzania.
"Ni heshima ya pekee ambayo Serikali imetoa kwa Vijana wetu wa vyuo vya elimu ya kati kushiriki michezo, kumbuka kwamba michezo hii aijawahi kuwepo tangu NACTE imeanzishwa hivyo hii ni fulsa ya pekee tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba tunahamasisha michezo hii wakati wote ili vijana wanaojiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi, Veta, na wale wa ngazi ya Diploma kushiriki michezo vyuoni"alisema Mpalule.

Sehemu ya pili imefanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya ustawi wa jamii kijitonyama  tarehe 29/11/2014, ambako Vyuo mbalimbali vya NACTE mkoa wa dar es salaam, vilicheza katika michezo ya soka, Basketball, Voleyball na netball,katika kutafuta timu zitakazoshiriki ligi ya NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015.
sehemu ya kwanza Ilizinduliwa kwenye chuo cha DIT  tarehe 22/11/2014 mwezi huu na kusisimua wengi katika  Michuano lutokana na kuwa na mfumo wa mtoano kuwa kivutio kwa Wachezaji na Mashabiki ambao wengi wao ni wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali wanaofika kushuhudia michuano hiyo inayoendeshwa kwa ubunifu wa hali ya juu.

 Vyuo vilivyokwisha cheza ni  Institute of Adult Education, Institute of Social Work (ISW) - DSM, Lugalo Military Medical School - Dsm, St. Joseph  College (University),  Dar es salaam City College (DACICO, Dar-es-Salaam School of Journalism (DSJ) - DSM, National Institute of Transport (NIT) - DSM, Bandari College - DSM,huku timu mwalikwa ikiwa ni Timu ya wafanyakazi wa PPF Dsm.


Vyuo vingine ambavyo tayari vimemaliza michezo yao ya awali ni pamoja na IFM ,DIT, CBE, Muhimbili,TRA,  Mlimani Profesianal,na  Royal College, waliokuwa kundi la kwanza lililofanyika viwanja vya chuo cha DIT akiba Posta.

Aidha vyuo vyote vinavyohusika na michezo ya wiki hii zimetakiwa kuwahi Viwanjani ili kukamilisha taratibu za ukaguzi kabla ya michuano hiyo ya mtoano kuanza na ikumbukwe kwamba michuano hiyo inaendeshwa kwa mfumo wa Bonanza na inafanyika kila siku za jumamosi kutokana na wanafunzi kuwa masomoni katika siku za kawaida.

kila mwaka michuano hii itakuwa ikifanyika kwa kushirikisha vyuo mbali mbali  vya elimu ya kati  hapa nchini Tanzania na vilivyopata usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za Tanzania kupitia vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa wavulana na wasichana ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES SALAAM.

Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji  kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha,  na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.

Wadhamini katika Bonanza hilo Mkoa wa Pwani ni Vodacom, Mlonge by Makai,  Bonga Resort & Hoteli na Zito Entertainment wanaojihusisha na Ukodishaji wa Miziki, utengenezaji wa Filamu na wakodishaji wa Magari ya Maharusi.
  
 lakini hata hivyo dirisha la wadhamini bado liko wazi kwa maana bado gharama ni kubwa za uendeshaji ambapo wajitokeze waweze kusaidia michezo hii iliyoanza kwa shamrashamra nyingi na kuwa na mvuto kwa watazamaji ususani wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliojitokeza.
Mwisho.

CELCOM YADHAMINI TUZO ZA TASWA KWA MILIONI 30

TASWA 1 Mwenyeliti wa Chama cha waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa) Juma Pinto (Wa kwanza kulia) akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya Selom Wireless, baada ya kutangaza udhamini wa Sh Milioni 30 kwa ajili ya udhamini wa Tuzo za wanamichezo bora wa 2013/14. Wengine katika picha ni Meneja  Biashara, ukuzaji na Masoko wa Selcom Wireless, Juma Mgori na Gallus Runyeta ambaye ni Meneja Miradi.
…………………………………………………………….
Kampuni ya malipo ya Kielektroniki ya, Selcom Wireless imetoa Sh Milion 30 kwa Chama cha waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa) kwa ajili ya kudhamini tuzo za wanamichezo bora wa msimu wa 2013/14 zitakazofanyika ijumaa ijayo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP.
Udhamini huo umetangazwa na Meneja wa Ukuzaji Biashara wa kampuni ya Selcom Woreless, Juma Mgodi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa City Sports Lounge wa jijini.
Mgori alisema kuwa wanajivunia sana kuwa miongoni mwa wadhamini katika tuzo ambazo zitamtoa rasmi mwanamichezo bora wa msimu wa 2013/14. Wadhamini wengine ni Said Salim Bakhresa & Co Ltd , IPTL, mifuko ya hifadhi ya jamii, PSPF na NSSF. Alisema kuwa  huo ni mwanzo tu wa kushirikiana na Taswa kwani wameingia katika dakika za mwisho kutokana na kujali umuhimu wa michezo nchini na kuona bora kutoa mchango wao. “Kama unavyojua, kampuni yetu inashughulikia malipo ya kielektoniki kwa taasisi za fedha 30 na tuna vituo vya malipo (Point of Services) zaidi ya 8,000, sisi ndiyo tunayoiwezesha jamii katika kila kona ya nchi yetu, hivyo mwakani tutaingia kwa nguvu zaidi,” alisema Mgori. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto aliipongeza kampuni hiyo kwa kuwasaidia na pia kuendelea kuziomba kampuni nyingine na wadau wa michezo nchini kuwasaidia pamoja na muda kukaribia mwishoni. “Naishukuru Selcom Wireless na wadhamini wengine kwa kutoa ‘ubani’ wao katika shughuli hii muhimu, bado ni tunahitaji msaada na tunaamini kuwa wadau wengine watajitokeza kutusaidia,” alisema Pinto. Katika Tuzo hizo, Taswa itatoa jumla ya tuzo 47 kwa wanamichezo mbali mbali ikiwa pamoja na mwanamichezo bora wa jumla na aliyetukuka.

Kampuni za simu Tanzania zashirikiana na AU ‘kutokomeza Ebola barani Afrika’

ttttttttttt
Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni maalum ya kampuni za simu tatu nchini zilizoungana kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kutokomeza ugonjwa wa Ebola Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Mawasliano na Mahusiano ya Umma kutoka Vodacom Bi. Rosalynn Mworia, na Meneja wa Huduma za Kijamii kutoka Airtel Bi. Hawa Bayumi (kulia). Kuchangia mteja yeyote wa kampuni hizo tatu tajwa anaweza akatuma neno ‘Tokomeza Ebola’ kwenda 7979
Kampuni za simu nchini Tanzania zimeingia katika ushirikiano na Tume ya Umoja wa Afrika (AU Commission) ili kuendeleza vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola unaoendelea kutishia amani nchi za Afrika Magharibi. Ushirikiano huo unaojulikana kama ‘AfricaAgainstEbola’ (AfrikaDhidiYaEbola) itatumia mtindo wa ujumbe wa kiganjani (SMS) kuweza kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwawezesha watalaam wa afya kutoka Afrika kuweza kwenda na kuhudumia nchi zilizo athirika.
Watu zaidi ya 5,000 wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola kutoka sehemu mbali mbali Afrika Magharibi tangu ugonjwa huo kulipuka kwa mara ya kwanza nchini Guinea mwezi Machi 2014. Kutokana na taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) huu ni mlipuko mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika bara hili ambayo kwa sasa ugonjwa huo umeshatapakaa katika nchi nne zikiwemo – Guniea, Liberia, Sierra Leone na Mali.
Katika mkutano wa kibiashara uliofanyika hivi karibuni chini ya AU, kampuni za simu zilijitolea kuanzisha kampeni maalum ya bara nzima ijulikanayo kama “United Against Ebola” (Pamoja Dhidi ya Ebola). Kampeni hii itakusanya michango kutoka kwa wateja wa kampuni mbali mbali za simu, na fedha hizo zitakazo kusanywa katika muda wa miezi mitatu, zitatumika katika mapambano dhidi ya kirusi hiki cha Ebola.
Akizungumzia kuhusu mpango huu hivi karibuni, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mheshimiwa Yayi Boni, Rais wa Jamhuri ya Benin, alisema: Tunayofuraha kuungana na kampuni za mawasiliano ya simu katika jitihada hizi. Mlipuko huu wa ugonjwa wa Ebola ni hali ya hatari kwa wanadamu, ni janga kwa familia zilizo athirika na tishio kwa ustawi wa uchumi ulioweza kufikiwa na nchi husika.
Aliendelea, “Hatuwezi tukakaa bila kufanya lolote. Tunaamini kwamba kwa ushirikiano wa sekta binfasi tunaweza kwa pamoja kutokomeza ugonjwa huu wenye malengo wa kuangamiza bara la Afrika

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA TOFAUTI.

uuuuuuuuuuuKATIKA MSAKO WA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MELANIA RICHARD (60) MKAZI KIJIJI CHA KAMFICHENI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.12.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MRISHO RAMADHAN (22) MKAZI AIRPORT ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 01 SAWA NA UZITO WA GRAM 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.12.2014 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA MANGA, KATA YA MANGA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE YA MOSHI/BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.