Mwenyeliti
wa Chama cha waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa) Juma Pinto
(Wa kwanza kulia) akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya Selom Wireless,
baada ya kutangaza udhamini wa Sh Milioni 30 kwa ajili ya udhamini wa
Tuzo za wanamichezo bora wa 2013/14. Wengine katika picha ni Meneja
Biashara, ukuzaji na Masoko wa Selcom Wireless, Juma Mgori na Gallus
Runyeta ambaye ni Meneja Miradi.
…………………………………………………………….
Kampuni ya malipo ya Kielektroniki
ya, Selcom Wireless imetoa Sh Milion 30 kwa Chama cha waandishi wa
habari za michezo nchini (Taswa) kwa ajili ya kudhamini tuzo za
wanamichezo bora wa msimu wa 2013/14 zitakazofanyika ijumaa ijayo kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee VIP.
Udhamini huo umetangazwa na Meneja
wa Ukuzaji Biashara wa kampuni ya Selcom Woreless, Juma Mgodi katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa City Sports
Lounge wa jijini.
Mgori alisema kuwa wanajivunia
sana kuwa miongoni mwa wadhamini katika tuzo ambazo zitamtoa rasmi
mwanamichezo bora wa msimu wa 2013/14. Wadhamini wengine ni Said Salim
Bakhresa & Co Ltd , IPTL, mifuko ya hifadhi ya jamii, PSPF na NSSF.
Alisema kuwa huo ni mwanzo tu wa kushirikiana na Taswa kwani
wameingia katika dakika za mwisho kutokana na kujali umuhimu wa michezo
nchini na kuona bora kutoa mchango wao.
“Kama unavyojua, kampuni yetu inashughulikia malipo ya
kielektoniki kwa taasisi za fedha 30 na tuna vituo vya malipo (Point of
Services) zaidi ya 8,000, sisi ndiyo tunayoiwezesha jamii katika kila
kona ya nchi yetu, hivyo mwakani tutaingia kwa nguvu zaidi,” alisema
Mgori.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto aliipongeza
kampuni hiyo kwa kuwasaidia na pia kuendelea kuziomba kampuni nyingine
na wadau wa michezo nchini kuwasaidia pamoja na muda kukaribia mwishoni.
“Naishukuru Selcom Wireless na wadhamini wengine kwa kutoa
‘ubani’ wao katika shughuli hii muhimu, bado ni tunahitaji msaada na
tunaamini kuwa wadau wengine watajitokeza kutusaidia,” alisema Pinto.
Katika Tuzo hizo, Taswa itatoa jumla ya tuzo 47 kwa wanamichezo
mbali mbali ikiwa pamoja na mwanamichezo bora wa jumla na aliyetukuka.
No comments:
Post a Comment