Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka
Tigo Bi. Woinde Shisael (katikati) akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na kampeni maalum ya kampuni za simu tatu nchini zilizoungana
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kutokomeza ugonjwa wa Ebola
Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Mawasliano na Mahusiano ya Umma kutoka
Vodacom Bi. Rosalynn Mworia, na Meneja wa Huduma za Kijamii kutoka
Airtel Bi. Hawa Bayumi (kulia). Kuchangia mteja yeyote wa kampuni hizo
tatu tajwa anaweza akatuma neno ‘Tokomeza Ebola’ kwenda 7979
Kampuni za simu nchini
Tanzania zimeingia katika ushirikiano na Tume ya Umoja wa Afrika (AU
Commission) ili kuendeleza vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola unaoendelea
kutishia amani nchi za Afrika Magharibi. Ushirikiano huo unaojulikana
kama ‘AfricaAgainstEbola’ (AfrikaDhidiYaEbola) itatumia mtindo wa ujumbe
wa kiganjani (SMS) kuweza kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwawezesha
watalaam wa afya kutoka Afrika kuweza kwenda na kuhudumia nchi zilizo
athirika.
Watu zaidi ya 5,000 wameshapoteza
maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola kutoka sehemu mbali mbali Afrika
Magharibi tangu ugonjwa huo kulipuka kwa mara ya kwanza nchini Guinea
mwezi Machi 2014. Kutokana na taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO)
huu ni mlipuko mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika bara hili ambayo kwa
sasa ugonjwa huo umeshatapakaa katika nchi nne zikiwemo – Guniea,
Liberia, Sierra Leone na Mali.
Katika mkutano wa kibiashara
uliofanyika hivi karibuni chini ya AU, kampuni za simu zilijitolea
kuanzisha kampeni maalum ya bara nzima ijulikanayo kama “United Against
Ebola” (Pamoja Dhidi ya Ebola). Kampeni hii itakusanya michango kutoka
kwa wateja wa kampuni mbali mbali za simu, na fedha hizo zitakazo
kusanywa katika muda wa miezi mitatu, zitatumika katika mapambano dhidi
ya kirusi hiki cha Ebola.
Akizungumzia kuhusu mpango huu
hivi karibuni, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mheshimiwa Yayi Boni, Rais
wa Jamhuri ya Benin, alisema: Tunayofuraha kuungana na kampuni za
mawasiliano ya simu katika jitihada hizi. Mlipuko huu wa ugonjwa wa
Ebola ni hali ya hatari kwa wanadamu, ni janga kwa familia zilizo
athirika na tishio kwa ustawi wa uchumi ulioweza kufikiwa na nchi
husika.
Aliendelea, “Hatuwezi tukakaa bila
kufanya lolote. Tunaamini kwamba kwa ushirikiano wa sekta binfasi
tunaweza kwa pamoja kutokomeza ugonjwa huu wenye malengo wa kuangamiza
bara la Afrika
No comments:
Post a Comment