Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh, Mwantumu Mahiza siku ya jumamosi wiki hii anatarajia kuongoza Bonanza la Wanavyuo linaloendea sehemu mbali mbali na ikiwa ni sehemu ya tatu kwa kanda ya kaskazini inayoendelea lwemye viwanja mbali mbali chini ya Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o
Ltd kwa kushirikiana na kituo bora cha Matangazo TIMES FM 100.5.
Bonanza hilo ambalo ni kwa ajili ya kupata timu zitakazoshiriki michuano ya NACTE linatarajiwa kuwa gumzo kwa mkoa wa Pwani kutokana na mfumo wake uliobuniwa kiufundi na waandaaji ambapo timu mbali mbali za Viongozi wa Serikali na zile za mkoa upata fulsa ya kushiriki pamoja kwa kufanya michezo ya soka, kikapu,netball pamoja na Voleyball.
Akizungumzia bonanza la jumamosi Mratibu wa Michezo Vyuoni, Mpalule Shaaban alisema kuwa Mh, Mwantumu anatarajia kufanya Uzinduzi wa Michezo hiyo kwa Mkoa wa Pwani kutokana na kwamba sasa Michezo hiyo itafanyika kila mwaka Sehemu mbali mbali za Tanzania.
"Ni heshima ya pekee ambayo Serikali imetoa kwa Vijana wetu wa vyuo vya elimu ya kati kushiriki michezo, kumbuka kwamba michezo hii aijawahi kuwepo tangu NACTE imeanzishwa hivyo hii ni fulsa ya pekee tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba tunahamasisha michezo hii wakati wote ili vijana wanaojiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi, Veta, na wale wa ngazi ya Diploma kushiriki michezo vyuoni"alisema Mpalule.
Sehemu ya pili imefanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya ustawi wa jamii
kijitonyama tarehe 29/11/2014, ambako Vyuo mbalimbali vya NACTE mkoa wa dar es salaam, vilicheza katika michezo ya soka, Basketball,
Voleyball na netball,katika kutafuta timu
zitakazoshiriki ligi ya NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015.
sehemu ya kwanza Ilizinduliwa kwenye chuo cha DIT tarehe 22/11/2014 mwezi huu na
kusisimua wengi katika Michuano lutokana na kuwa na mfumo wa mtoano kuwa kivutio kwa Wachezaji na
Mashabiki ambao wengi wao ni wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali wanaofika
kushuhudia michuano hiyo inayoendeshwa kwa ubunifu wa hali ya juu.
Vyuo vilivyokwisha cheza ni Institute of Adult Education, Institute
of Social Work (ISW) - DSM, Lugalo
Military Medical School - Dsm, St. Joseph College
(University), Dar es salaam City College (DACICO, Dar-es-Salaam
School of Journalism (DSJ) - DSM, National
Institute of Transport (NIT) - DSM, Bandari
College - DSM,huku timu mwalikwa
ikiwa ni Timu ya wafanyakazi wa PPF Dsm.
Vyuo vingine ambavyo tayari vimemaliza michezo yao ya awali ni pamoja na IFM ,DIT, CBE, Muhimbili,TRA, Mlimani Profesianal,na Royal College, waliokuwa kundi la kwanza lililofanyika viwanja vya chuo cha DIT akiba Posta.
Aidha vyuo vyote
vinavyohusika na michezo ya wiki hii zimetakiwa kuwahi Viwanjani ili
kukamilisha taratibu za ukaguzi kabla ya michuano hiyo ya mtoano kuanza na
ikumbukwe kwamba michuano hiyo inaendeshwa kwa mfumo wa Bonanza na inafanyika
kila siku za jumamosi kutokana na wanafunzi kuwa masomoni katika siku za
kawaida.
kila mwaka michuano hii itakuwa ikifanyika kwa kushirikisha
vyuo mbali mbali vya elimu ya kati hapa nchini Tanzania na vilivyopata usajili
wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za Tanzania kupitia vyuo vyao
vitashindana katika michezo mbali mbali kwa wavulana na wasichana ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya
mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo
zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES
SALAAM.
Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa
ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling,
Mashindano ya Vipaji kwa viongozi
wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu,
Mawaziri wa Michezo,Fedha, na Spika ,
watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada
katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa
wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.
Wadhamini
aliojitokeza mpaka sasa na kuonyesha nia ya kusaidia mashindano hayo ni pamoja
na Coca Cola, Vodacom, MLONGE BY MAKAI, CXC –Tours,Bonga Resort & Hoteli, Ikondolelo Hoteli, na 100.5 Times Fm.
lakini hata hivyo dirisha la wadhamini bado
liko wazi kwa maana bado gharama ni kubwa za uendeshaji ambapo wajitokeze
waweze kusaidia michezo hii iliyoanza kwa shamrashamra nyingi na kuwa na mvuto
kwa watazamaji ususani wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliojitokeza.
No comments:
Post a Comment