Mkurugenzi
wa Utetezi na Maboresho ya Sera wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC), Halord Sungusia (katikati), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa tathmini ya
mwenendo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
kushughulikia sakata la fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow. Kushoto
ni Ofisa Mipango Dawati la Uangalizi wa Serikali wa LHRC, Hussein Sengu
na Wakili, Hamisi Mkindi. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Wakili, Hamisi Mkindi (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema Mahakama isitumiwe kama kinga ya kufanya uhalifu.
Hayo
yamebainishwa Dar es saalam leo na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho ya
Sera wa LHRC, Halord Sungusia wakati akizungumza na wanahabari
alipokuwa akitoa tathmini ya mwenendo wa Bunge la Tanzania katika
kushughulikia sakata la fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
“Mahakama
ni taasisi kuu kitaifa ya kutoa haki kwa wananchi wote lakini isitumiwe
na mtu au taasisi yoyote kama kinga yake ya kufanya uhalifu” alisema
Sungusia.
Aidha
alibainisha kuwa katiba ya sasa inatoa mianya mingi ya kutozingatiwa kwa
miiko ya uongozi hasa baada ya kufutwa kwa azimio la Arusha na rasimu
ya pili ya katiba iliweka msingi huu wa maadili ya uongozi kwa upana na
kwa msisitizo.
Sungusia
aliongeza kuwa nchi haitokuwa salama kama katiba inayopendekezwa
itapitishwa kama ilivyo kuwa kwani inayopendekezwa haizungumzii kwa
mapana maadili na miiko ya viongozi wa umma, haiweki misingi bora ya
uwajibikaji na kusimamia dhamana ya uongozi na kanuni za uongozi wa
umma.
Katika
hatua nyingine LHRC kimetaka wale wote ambao watabainika katika sakata
la utoaji wa fedha katika akaunti hiyo wachukuliwe hatua kali za
kisheria.
No comments:
Post a Comment