Mahafali ya nane ya Chuo cha
Teknolojia Dar es Salaam (DIT), yanatarajiwa kufanyika Januari 31 mwaka
huu katika viwanja vya chuo hicho na yatatanguliwa na utoaji wa tuzo na
zawadi mbalimbali kwa wahitimu ambao wamefanya vizuri katika masomo yao.
Taarifa ya DIT kwa vyombo vya habari imesema kuwa tuzo kwa
wanafunzi zitatolewa Januari 23 mwaka huu ikiwa ni wiki moja kabla ya
mahafali hayo ambayo wahitimu katika ngazi na masomo tofauti
watatunukiwa.
Wahitimu watakaotunukiwa ni siku hiyo ni pamoja na wa
Stashahada ya Uhandisi (Ordinary Diploma), cheti cha awali cha TEHAMA
(IT) mwaka wa masomo 2013/2014.
Wahitimu wametakiwa kusoma utaratibu wa kuthibitisha kushiriki
mahafali hayo katika tovuti ya Taasisi www.dit.ac.tz na “Rehearsal”
itafanyika Ijumaa tarehe 30 Januari 2015.
“Malipo ya Tshs 30,000/= kwa ajili usajili yatafanyika kwenye
tawi lolote la NBC kwenye akaunti namba 018101003145 na kujisajili
kupitia tovuti ya Taasisi www.ac.dit.tz” Inasema taarifa hiyo.
Malipo yanatakiwa klufanyika kwa kutumia jina kamili kama
linavyoonekana kwenye orodha ya wahitimu iliyotolewa kwenye tovuti ya
Taasisi, namba ya usajili na dhumuni la malipo mf. Ada, transcript na
graduation.
Kulingana na taarifa hiyo, mwisho wa kujisajili ni tarehe 31
Desemba, 2014 na wahitimu wametakiwa kufahamisha kuhusiana na mahafali
hayo.
No comments:
Post a Comment