Siku ya Kimataifa ya
Kujitolea Duniani huadhimishwa tarehe 5 Desemba kila mwaka kwa lengo la
kutambua mchango wa kujitolea unaotolewa kwa ajili ya maendeleo katika
jamii tunamoishi, kitaifa na kimataifa.
Kujitolea hujumuisha hiari, umoja, utu na kuaminiana na kunatoa
fursa muhimu katika kupambana na maradhi, ujinga, umasikini, hifadhi ya
mazingira na maeneo mengi ya kimaendeleo ambayo yanahitaji msukumo.
Aidha, kujitolea kunatoa mchango
muhimu katika kushughulikia majanga pale yanapotokea, kuimarisha umoja
katika jamii na kuboresha maisha ya watu.
Tanzania kama sehemu ya jamii ya
Kimataifa itaadhimisha siku hiyo katika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii
kilichopo karibu na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),saa mbili na nusu
asubuhi.
Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo mwaka huu ni ‘Ushiriki na
Ushirikishwaji katika kuleta maendeleo katika ngazi zote za mitaa, taifa
na kimataifa.’
Katika maadhimisho hayo, wananchi
hasa vijana watashiriki katika mdahalo kuhusu umuhimu wa kujitolea kwa
ajili ya kuleta maendeleo. Aidha, kutakuwa na shuhuda na maonyesho ya
taasisi zinazoshiriki katika shughuli za kujitolea ili kuhamasisha na
kufufua moyo wa kujitolea miongoni mwa jamii.
Watanzania hususan Vijana
wanahamasishwa kuibua shughuli za kujitolea na kushiriki katika zile
zilizokwisha anzishwa ikizingatiwa kuwa wao ndiyo nguvu kazi kubwa ya
jamii.
Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo inawakaribisha wananchi wote kushiriki katika
maadhimisho hayo muhimu ili kushiriki katika mdahalo huo na kujionea
jinsi watu mbalimbali wanavyotoa mchango mkubwa katik jamii kupitia
shughuli za kujitolea.
No comments:
Post a Comment