Wadau
mbalimbali wakishiriki sherehe za kilele cha Wiki ya Usafiri wa Anga
zilizofanyika leo katika viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga jijini Dar es
salaam.
Meneja mradi wa ujenzi wa
jingo jipya la abiria (Terminal 3) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,
Muhandisi Mbaraka Shafii akimweleza Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe
(wa pili kutoka kulia) maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo utakaokuwa na uwezo wa
kuwahudumia abiria milioni 6 kwa mwaka.
Waziri wa
Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe ( kulia) akimweleza jambo Muhandisi Mwanaidi Mkwizu
kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa jengo
jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere eneo la
Kipawa jijini Dar es salaam.Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Miundombinu Mh. Peter Selukamba.
Waziri wa
Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Bw.Ralph
Goetz , Mtaalam wa masuala ya Miundombinu wa kampuni ya Switzport Tanzania kuhusu ujenzi wa jengo la kutolea
huduma kwa abiria wa kampuni hiyo leo jijini Dar es ikiwa ni sehemu ya ushiriki
wa sekta binafsi katika kuendeleza sekta
ya usafiri wa anga nchini.
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe
(wa pili kutoka kulia) akiwasisitiza baadhi ya wahandisi wa wanawake
wanaosimamia mradi wa ujenzi wa jengo jipy la abiria katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa kuzingatia
viwango vilivyowekwa.
Waziri wa
Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea maandamano ya wadau wa sekta ya
Usafiri wa Anga walioshiriki maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Usafiri wa Anga leo
jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya Usafiri wa Anga
wakishiriki maandamano wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Usafiri wa
Anga jijini Dar es salaam.
Baadhi ya
Wanafunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga kilichoko jijini Dar es salaam wakipita
mbele ya mgeni rasmi, Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa
kilele cha Wiki ya Usafiri wa Anga leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Miundombinu Mh. Peter Selukamba wakifurahia jambo walipotembelea
banda la maonesho la kitengo cha kuongozea ndege katika uwanja wa Kimataifa wa
ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa kitengo cha
Zimamoto na Uokoaji uwanja wa ndege,
Sajenti Thomas Lichenjela alipotembelea banda la maonesho la kitengo hicho
kuona namna walivyojipanga kukabiliana na majanga mbalimbali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Mafunzo kwa marubani Tanzania Bw. Quentin Gray (kulia) akitoa ufafanuzi kwa
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na watendaji wa Mamlaka ya Usafiri
wa Anga Tanzania namna kituo chake kilivyojipanga kutoa mafunzo katika fani ya urubani
na uongozaji wa ndege leo jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha Wiki ya
Usafiri wa Anga.
Waziri wa
Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akiwapokea baadhi ya wanafunzi wa shule za 3 msingi
kutoka wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala walioshiriki ziara ya mafunzo katika
masuala ya Anga katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini
Zanzibar. Vijana hao pia walifanya ziara katika uwanja wa Kimataifa wa Mwl.
Julius Nyerere.
Waziri wa
Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe,Viongozi na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri
wa Anga Tanzania(TCAA), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mh. Peter
Selukamba na Viongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA) wakiwa
katika picha ya pamoja baadhi ya wanafunzi wa shule za 3 msingi kutoka wilaya
za Temeke, Kinondoni na Ilala walioshiriki ziara ya mafunzo katika masuala ya
Anga katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar.
(Picha Zote Na: Aron Msigwa –
MAELEZO. .
No comments:
Post a Comment