Meneja
Uhifadhi wa Shirika la Utunzaji wa Mazingira WWF Tanzania, Dr. Amani
Ngusaru ,akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo
vya habari mbalimbali katika semina ilioandaliwa na (WWF) iliofanyika
Disemba 2-3, 2014 mkoani Morogoro juu ya utunzaji wa mazingira ili
kuleta uwiano sawa wa rasilimali zinazopatikana maeneo mbalimbali
nchini. Mkurugenzi
wa Shirika la Utunzaji wa Mazingira WWF Tanzania Bw. Bell’Aube
Houinato akielezea malengo ya Shirika hilo, ambayo pamoja na mambo
mengine ni kuhakikisha ulinzi wa viumbe hai na misitu izingatiwe ili
kulinda mazingira na kuinua uchumi wa taifa. Kiongozi
wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira WWF, CEA (Coastal East Africa
Global Initiative Leader), Peter Scheren akifafanua jambo katika mkutano
wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika utendaji wao kazi katika
uhifadhi wa mazingira. Kwamba kuwepo na ushirikiano katika utunzaji wa
mazingira ili kuleta uwiano sawa na rasilimali ambazo zinapatika katika
maeneo husika. Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Bw.Magese Bulayi akisisitiza jambo kuhusiana uvuvi haramu wakati wa semina hiyo. Mtaalam
wa Maendeleo ya Uhifadi kutoka Shirika la WWF Tanzania, Prof.Hussein
Sosovele akiwakilisha mada yake wakati wa semina hiyo ambapo amesema
kuwa kutoka na elimu inayotolewa na WWF katika maeneo mbalimbali hapa
nchini, baadhi ya jamii zimeshatambua umuhimu wa hifadhi katika
maeneoyao. “Mapato hayo ni kiwango kikubwa mno, kwa kuwa yanasaidia
kusukumamiradi ya maendeleo kakika kijiji husika. Ingawa kuna changamoto
zahapa na pale lakini tunaamini haya ni mafanikio na kila mmoja
wetuanapaswa kushiriki katika utunzaji wa mazingira,” alisema Profesa
Sosovele.
Wahariri
na waandishi wa habari wakiwa katika majadiliano ya namna ya
kukabiliana uvuvi haramu katika mwambao wa bahari ya Hindi.
Kulia
ni Idda Mushi kutoka ITV, lilian Lucas kutoka Mwanchi (katikati) na
Monica Liumpawe TBC wakiwa kwenye harakati za kundaa habari wakati wa
semina hiyo. Wahariri na waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment