Mratibu
wa Uhurumarathon Tanzania Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar Es Salaam juu ya kukamilika kwa maandalizi yam bio
hizo zinazotarajiwa kufanyika jumapili hii jijini Dar Es Salaam katika
viwanja vya Leders Club kushoto ni katibu mkuu wa shirikisho la Riadha
la Taifa Selemani Nyambui.
………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
MAANDALIZI ya mbio za Uhuru, Uhuru
Marathon, zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es Salaam
yamekamilika, huku wanaridha kadhaa kutoka ndani na nje ya nchi
wakithibitisha kushiriki mbio hizo zenye lengo la kuulinda uhuru wetu,
kudumisha umoja, amani, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana, Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, maandalizi
yote yamekamilika, huku wanariadha wa hapa nchini kutoka nje ya Dar es
Salaam wakiwa wamewasili tayari kwa ushiriki wao.
Melleck pia alisema, kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi ulinzi umeimarishwa kwa kiwango kikubwa
ili kuhakikisha usalama unakuwa mkubwa kwa washiriki wote na barabara
zitakazotumika zitafungwa katika kipindi hicho.
“Kila kitu kimekamilika na
washiriki kutoka nje ya Dar es Salaam wameanza kuwasili kwa ajili ya
mbio hizo na tunawahakikishia usalama utakuwa mkubwa mno katika kipindi
chote cha mbio hizo n mpaka kufikia jana (juzi) tayari washiriki
waliojitokeza walikuwa 4000,” alisema.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha
Tanzania (RT), Selemani Nyambui alisema, wanariadha maarufu wa hapa
nchini watakaoshiriki ni pamoja na Fabian Joseph na Dickson Marwa, huku
Jacqueline Sekini aliyeshinda mbio hizo kwa upande wa wanawake mwaka
jana, naye akiapa kutetea ubingwa wake.
“Wapo wanariadha wengi
watakaoshiriki, lakini nataka kutoa angalizo kwa wanariadha kutoka
Kenya, sisi tumetumwa mwaliko kwa wa chama husika na wao ndio watutumia
majina ya wanariadha kumi, watano wa kiume na waliobaki wa kike,
hatutapokea mwanariadha kutoka nchi hiyo ambaye hatujapewa jina lake,”
alisema.
Nyambui alisema, tayari waamuzi
watakaosimamia mbio hizo wapo tayari na akasisitiza ni lazima taratatibu
zote zitafuatwa ili kupata mshindi halali.
Mbio hizo zinatarajiwa kuanzia
viwanja vya Leaders Club na zitakuwa za kilomita 21, kilomita 5 na
kilomita 3 ambazo ni maalumu kwa ajili ya viongozi wa kitaifa, dini na
taasisi mbalimbali.
Aidha Melleck alisema, tayari namba kwa washiriki zimeanza kutolewa na wanaweza kuzipata katika viwanja vya Leaders Club.
Mgeni rasmi katika mbio hizo anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment