Waziri wa Fedha
Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa
serikali ya Tanzania kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
Waziri wa Fedha
Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana hati ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali
ya Tanzania waliosaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
Baadhi ya waandishi
wa habari na watumishi wa wizara ya Fedha pamoja na wawakilishi wa Serikali ya
Saudi Arabia wakiwashuhudia Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mkurugenzi wa
Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas wakisaini mkataba wa
mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
04/12/2014
Serikali ya Tanzania
imesainiana mkataba wa mkopo wenye
masharti nafuu wa zaidi ya shilingi
bilioni 45.2 na Shirika la Maendeleo la Saudia kwa lengo la kuboresha miradi wa
maji kwa wilaya ya Same, Mwanga na ujenzi na ukarabati wa barabara Visiwani
Zanzibar.
Mkataba huo umesainiwa
leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya
Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi
Hassan Al-Attas.
Akiongea na waandishi wa
habari katika hafla hiyo, Waziri Saada alisema kuwa kati ya mkopo huo shilingi
bilioni 41.25 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 25 zitagharimia
mradi wa maji katika wilaya za Same na Mwanga na shilingi bilioni 3.96 kwa ajili ya maradi wa
barabara Pemba, visiwani Zanzibar.
Waziri Saada
alilishukuru Shirika la Maendeleo la Saudia kwa jitihada zao za kuisaidia
Serikali ya Tanzania katika kautatua tatizo la maji wilaya za Same na Mwanga
pamoja na uboreshaji wa barabara katika visiwa vya Pemba.
Aidha, mradi wa maji wa
Same- Mwanga utagharimu Dola za Kimarekani milioni 110.34 ambazo benki ya
BADEA, Shirika la Maendeleo Kuweit, OPEC na mashirika mengine wamekubali
kukamilisha sehemu ya fedha iliyobakia.
Mradi wa maji wa Same-
Mwanga baada ya kukamilika utasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji
vijijini amabapo utasaida kuboresha hali ya maisha wa wananchi wa maeneo hayo,
upatikanaji nwa maji safi na salama kwa maendeleo ya afya za wakazi hao na
kuboresha uchumi wao kwa kutumia muda mwingi kwa shuighuli za uzalishaji mali
badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas amesema kuwa
makataba waliosaini leo unaonesha kuwa Saudi Arabia iko mstari wa mbele katika
kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wake kwa
kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa
waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa wizara ya Fedha na wawakilishi wa
Serikali ya Saudi Arabia.
No comments:
Post a Comment