Mwenyekiti
wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Dkt
Ibrahim Msengi akifungua kikao cha tano cha bodi ya barabara Mkoa kwenye
ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, kulia kwake ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Rajabu Rutengwe ambaye awali alikuwa Mkuu wa
Mkoa wa Katavi sasa amehamishiwa mkoa wa Tanga na Nafasi yake
kuchukuliwa na Dkt Msengi aliyemkabidhi uwenyekiti wa bodi ya
Barabara.(Picha zote na Kibada Kibada -Katavi) Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahimu Msengi Mwenye suti ya Bluu na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Dkt Rajabu Rutengwe wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi
wa mikutano mjini Mpanda muda mfupi baada ya kutoka kwenye Kikao cha
Tano cha Bodi ya Barabara kilichofanyika leo mjini Mpanda. Wajumbe
wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi wakifuatilia mjadala wa
kikao hicho mbele ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda
Estomhn Chang’ah mwenye suti ya kahawia na Selemani Lukanga Mkurugenzi
wa Mji Mpanda. Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mpanda Estomihn Chang’ah akitoa taarifa ya
utekelezaji wa miradi ya barabara kwenye kikao cha bodi ya Barabara Mkoa
wa Katavi.
………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada –Katavi
Mwenyekiti wa Kikao cha Bodi ya
Barabara Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Dkt Ibrahim
Msengi ameshauri wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara kufanya kazi kwa
ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha barabara za Mkoa huo zinajengwa
kwa kiwangokinachokubaliki kuliko kukaa kinywa kusubiria hadi kikao
kiitishwe ndiyo waseme mapungufu yaliyojitokeza.
Dkt Msengi alitoa kauli hiyo
wakati akifungua Kikao cha tano cha Bodi ya Barabarakilichofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mji Mpanda
Mkoani Katavi na kuzungumzia changamoto mablimbali zinazoikabili sekta
ya miundo mbinu Mkoani humo hasa sekta ya Barabara.
Alisema kikao cha Bodi ni cha
kisheria hivyo Wajumbe wake wanawajibu na jukumu la kusimamia na
kufuatilia kazi zote zinazofanyika katika Mkoa kwa kufuata taratibu
zinazotakiwa bila kuingilia mchakato mingine ya kisheria kama mambo ya
zabuni na masuala ya Kifedha lakini kubwa zaidi ni ushirikiano wa karibu
miongoni mwao taasisi nyingine kwa kuwa kila kitu kinahitaji
ushirikiano na mawasiliano ya karibu.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema
haitakuwa busara barabara zinajengwa chini ya kiwango na wajumbe wa bodi
wapo waaona na kuacha kushauri hadi kazi inakamilika ndipo wanaanza
kuhojii wakati ungeweza kusimamia mapema na kusaidia kuondoa kasoro hizo
kwa kutoa ushauri mapema.
Akashauri kuwa ni vyema
ufuatiliaji uwepo tangu mwanzo ili kuhakikisha taratibu zote
zinafuatiliwa kwa kufuata utaratibu na sheria na kuona barabara kama
zinajengwa kwa wakati,akaeleza kuwa hiyo ni moja ya kazi ya bodi ya
barabara.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa
Katavi Mhandisi Emmanuel Kalobelo alieleza Bodi ya Barabara Mkoa wa
Katavi ilizinduliwa mwaka 2012 wakati linazinduliwa Mkoa ulikwa na
mtandoa wa barabara zinazohudumiwa zikiwa katika hali mbaya lakini
bodi imefanya jitihada mbalimbali na kazi mbalimbali zimeendelea
kufanyika chini ya uongozi wa Bodi hii.
AIisema kazi mbalimbali
zimefanyika na zinaendelea kufanyika akataja barabara ya Mpanda –
Uvinza,iko katika hali ya usanifu pia barabara ya Mpanda – Ugalla hadi
Kaliua undyankulu Kahama, Mpanda –Inyonga, shughuli zinaendelea katika
kuhakikisha Mkoa unafunguka.
Kwa upande wake aliyekuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara na Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye amehamia
Mkoa wa Tanga Dkt Rajabu Rutengwe akimkaribisha Mwenyeiti Mpaya wa Bodi
ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa mpya wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi ameeleza
kuwa Mkoa wa Katavi ni moja ya Mkoa ambao uko nyuma kwa maendeleo ya
Barabara za lami nchini hadi wakati unaanzishwa mwaka 2012 ulikuwa na
kilometa (2)mbili za lami tofauti na maeneo mengine nchini lakini sasa
unamtandao wa barabara za lami kilometa 34 hayo ni maendeleo kwa kipindi
cha miaka miwili tu juhudi zimefanyika.
Amesema Mkoa una sura ya Samaki
ya Pweza ili uende sehemu nyingine kutoka makao makuu ya mkoa lazima
uende moja kwa moja halafu lazima urudi ulikoanzia safari hivyo
ameshauri wajumbe wa bodi ya Barabara na wananchi kwa ujumla
kutoaushirikiano wa karibu kwa Mkuu wa Mkoa Mpya kama waliompatia wakati
yeye alipokuwa mkuu wa mkoa na mwenyekiti wa Bodi ya Barabara hivyo na
mwenzake apewe ushirikianokam aliokuwa akipewa ilikuleta maendeleo
katika Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment