Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya miaka
70 ya Usafiri wa anga duniani yanayoendelea nchini na namna Serikali
kupitia Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ilivyojipanga kuhakikisha
usalama wa ndege na abiria wanaotumia anga la Tanzania.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) Bw. Charles Chacha
akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa anga Tanzania
na namna Tanzania ilivyofanikiwa kupunguza idadi ya ajali za ndege.
Meneja
wa Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga kutoka Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA) Bw. John Mayunga akifafanua utekelezaji wa majukumu
ya Mamlaka ya Hali ya Hewa katika usafiri wa anga.Afisa
mwongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere Bi. Mossy Kitangita akiwahamasisha baadhi ya vijana na
wanafunzi waliotembelea banda la maonesho la kitengo cha kuongozea ndege
(hawapo pichani) kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kupata fursa ya
kujiunga na fani ya uongozaji wa ndege ndani na nje ya nchi.Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, akimsikiliza Ofisa
Utawala, kutoka Baraza la Ushauri la Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA-CC),
Ms Catherine Monarya, wakati alipotembelea banda hilo kujua shughuli
mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo, Katibu Mkuu ameishauri taasisi
hiyo kutoa elimu zaidi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, akimsikiliza Kaimu
Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa katika Usafiri wa Anga na Maji kutoka
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), wakati alipotembelea banda hilo
katika maonesho ya sekta ya Usafiri wa Anga, ambayo yanafanyika katika
viwanja vya Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), leo
asubuhi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka(mwenye tai nyekundu),
akimsikiliza Muongozaji Ndege katika kiwanja cha Mwalimu Julius Nyerere
(JNIA), Bi. Mossy Kitang’ita, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya
Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), leo asubuhi katika viwanja vya Ofisi za
Mamlaka hiyo.
No comments:
Post a Comment