Kiongozi
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza na Meneja wa Uwanja
wa ndege wa Mpanda, Mkoani Katavi Bw. Seneti Lyatuu (Kulia).
Anayefuatilia mazungumzo ni Bw. Omary Abdallah ambaye Kaimu Mkurugenzi
wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango). Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda kujionea shughuli mbalimbali
za maendeleo uwanjani hapo. Kiongozi
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza na Meneja wa Uwanja
wa ndege wa Mpanda, Mkoani Katavi Bw. Seneti Lyatuu (Kulia).
Anayefuatilia mazungumzo ni Bw. Omary Abdallah ambaye Kaimu Mkurugenzi
wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango). Meneja
wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, Mkoani Katavi Bw. Seneti Lyatuu (Kulia)
akifafanua jambo kwa Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto).
Anayewasikiliza ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Abdallah (Katikati). Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakipata maelekezo ya uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda kutoka
kwa Meneja wa uwanja huo, Bw. Seneti Lyatuu (Kushoto).
…………………………………………………………………………….
Na Saidi Mkabakuli, Mpanda
Kufuatia kukamilika kwa ukarabati
na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi, Serikali
imewaasa watumiaji wa uwanja huo kutunza miundombino ya uwanja huo ili
kuweza kuhudumia wakazi na wageni wapitao uwanjani hapo kwa muda mrefu.
Wito huo umetolewa na Kiongozi wa
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani
Katavi.
Bibi Mwanri alisema kuwa serikali
kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imekamilisha kazi ya kuufanya
uwanja huo uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za
binafsi na biashara, hivyo uongozi wa uwanja huo hawana budi ya
kuhakikisha miundombinu ya uwanja huo inatunzwa ipasavyo.
“Kama munavyofahamu Serikali
imekuwa ikiwekeza sana katika uendelezaji wa miundombinu ya usafiri
nchini hasa kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga ili
kuongeza ufanisi na kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja
vya ndege katika maeneo ya kimkakati, hivyo kuna haja ya kuunga mkono
jitihada hizi za Serikali,” aliasa Bibi Mwanri.
Akitoa taarifa ya uendelezaji
uwanja huo kwa msafara wa timu ya ukaguzi, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa
Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo,
unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile
ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.
“Uwanja huu umekarabatiwa na
barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami
kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa
mita 1,820 na upana wa mita 30,” alisema Bw. Lyatuu.
Kwa mujibu wa Meneja huyo,
kukamilika kwa uwanja huo kumevutia idadi ya abiria wanaoutumia uwanja
huo kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14.
Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo
wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16), Miundombinu ni kipaumbele
cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati,
usafirishaji (bandari, reli, barabara na usafiri wa anga), maji (safi,
taka na ya uzalishaji) na TEHAMA.
Serikali imeandaa Mpango wa
Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa
ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za
ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na
unaolenga watu walio masikini zaidi. Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa
Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya
maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali
fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo
kitaifa.
Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment