Mratibu
wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya (D.H.I.S) Suleiman
Salum Ali akieleza mafanikio ya mafunzo hayo yaliyofanyika Hoteli ya
Double Tree Nungwi, wa kwanza (kulia) ni Profesa Kristin Braa kutoka
Chuo Kikuu cha Oslo ambao ni waandaaji wa mafunzo hayo kwa kushirikiana
na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wizara ya Afya Zanzibar. (kati) ni
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliefunga mafunzo hayo. (Picha
na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar) Naibu
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi cheti mmoja ya
washiriki wa mafunzo ya D.H.I.S Osama Al Zubair kutoka Sudan wakati
wa kufunga mafunzo hayo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi, Kaskazini
Unguja. Mgeni
rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya D.H.I.S Mahmoud Thabit Kombo
akiwahutubia washiriki wa mafunzo hayo kutoka Nchi za Afrika, Marekani,
Ujerumani na Mashirika wahisani katika Hoteli ya Double Tree Nungwi. Washiriki
wa mafunzo hayo wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud
Thabit Kombo alipokuwa akiyafunga mafunzo ya siku 10 yaliyofanyika
Hoteli ya Double Tree Nungwi. Mratibu
wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya Suleiman Salum Ali
akizungumza na waandishi wa Habari walioshiriki ufungaji wa mafunzo hayo
katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.Picha
ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za
Afya (D.H.I.S) wakiwa na mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo Naibu
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar).
No comments:
Post a Comment