Onesmo Charles ambaye ni mmoja wa
wanafunzi 130 waliofanya vizuri katika masomo katika Chuo Kikuu cha
Ardhi (ARU), akijaribu kifaa cha kisasa cha kupimia ardhi, viwanja na
ramani za nyumba alichozawadiwa Kampuni ya Hightech Systems (T) Limited
katika hafla ya kuwakabidhi zawadi na tuzo wanafunzi hao bora
iliyofanyika katika chuo hicho leo ikiwa ni sehemu ya mahafali ya nane
ya chuo hicho yatakayofikia kilele kesho kutwa Ukumbi wa Diamond Jubilee
Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Ardhi Dar es Salaam (ARU), Idrissa Mshoro (kulia) akimkabidhi mwanafunzi
Onesmo Charles kifaa cha kisasa cha kupimia ardhi, viwanja na ramani za
nyumba chenye thamani ya sh. mil. 35 baada ya kuwa mmoja wa wanafunzi
130 waliofanya vizuri katika masomo. Hafla ya kuwakabidhi zawadi
wanafunzi hao bora iliyofanyika katika chuo hicho leo, ni sehemu ya
mahafali ya nane ya chuo hicho yatakayofikia kilele kesho kutwa kwenye
Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Godfrey
Ntaki wa Kampuni ya Hightech Systems (T) Limited. iliyotoa zawadi hiyo.
Onesmo akipongezwa na wanafunzi wenzake
Onesmo akiwa katika picha ya pamoja na wenzake
Cheti alichotunukiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ipyana Mwangoka akikabidhiwa zawadi ya cheti
Jonathan Kansheba akitunukiwa cheti
Joyce Kasenga akipatiwa tuzo ya cheti
Mariam Maringe akipatiwa tuzo
Rashid Ngenyi akipatiwa tuzo ya cheti
Rebecca Milano alipatiwa tuzo tano
Tadeus Rudaichi akipokea tuzo
Asha Muhali alituzwa tuzo tano
Anthony Mwashilingi akizawadiwa
Bibian Abel akizawadiwa
Faraja Ally akizawadiwa cheti
Ikukea tuzo ya chetipa Mwakisole akipo
Sehemu ya wanafunzi waliotunukiwa tuzo
Meza kuu
Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chuo hicho pamoja na wafadhili
No comments:
Post a Comment