MultiChoice Africa, kampuni
inayoongoza katika kutoa burudani ya kulipiwa ya dijitali pamoja na IPP
Media wamesaini makubaliano yatakayoleta chaneli maarufu zaidi Tanzania,
ITV, kuwa sehemu ya jukwaa la DStv.
Ushirikiano huu wa kusisimua utawapa watazamaji wa Tanzania kote
nchini fursa ya kuangalia vipindi vilivyotengenezwa hapa hapa nchini
vikiwa na ubora mkubwa kidijitali. Chaneli hii itapatikana kwenye
vifurushi vyote vya DStv ikiwemo kifurushi kilichozinduliwa hivi
karibuni cha Bomba, Family, Compact, Compact Plus na Premium.
Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV Bi
Joyce Mhaville alisema: “Tunajivunia sana ushirikiano huu ambao tumekuwa
tukiufanyia kazi kwa muda mrefu. Fursa zinazojitokeza kutokana na
makubaliano haya yatanufaisha kampuni zote mbili pamoja na kuwanufaisha
watazamaji wetu, hasa kwa wakati huu ambao tumehama kutoka katika mfumo
wa analojia kuingia dijitali. ITV ina vipindi vyenye ubora
vilivyotengenezwa hapa hapa nchini na ambavyo vinawafaa watanzania
wakati DStv itatuwezesha kupanua wigo wetu.”
Akizungumza juu ya hili, Mkurugenzi wa MultiChoice Africa kanda
ya Afrika Mashariki Bwn Stephen Isaboke alisema: “MultiChoice
imejizatiti kuwapa watazamaji wake chaneli nyingi mbalimbali zikiwepo
zinazoonyesha vipindi vya hapa hapa na vile vya nje. Kwa kuwa ITV
inakuwa kwa kasi na ina watazamaji wengi, ushirikiano huu utatufaa kwa
vile unaongeza vipindi vilivyotengenezwa hapa nchini. Tutaendelea
kuwekeza katika kuwaletea vipindi vyenye utofauti. Kwa kupitia vifurushi
vyetu mbalimbali, tunawapa wateja wetu chaneli nyingi kwa bei tofauti
ili wawe na uwanja mpana wa kuchagua.”
Bw Isaboke na Bi Mhavile walionyesha kufurahishwa sana na
kujitoa kwao kwa ushirikiano huu. Waliwahamasisha watanzania kununua
DStv ili waweze kufurahia ITV na chaneli zingine nzuri.
No comments:
Post a Comment