Bw.
Peragius Cosmas mwanafunzi aliyehitimu shahada ya Uhasibu na kupata
GPA 4.91 akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE
Prof.Emanuel Mjema.
Bi.
May Issa mwanafunzi aliyehitimu shahada ya kwanza ya Usimamizi wa
manunuzi na kupata GPA 4.92 Akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu
wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.
Kwa
kile ambacho kimeonekana ni tishio kwa chuo cha Elimu ya Biashara
(CBE) wanafunzi hawa kutoka kampasi ya Dodoma wameweza kupata ufaulu
mkubwa katika masomo yao.
Bi. May Issa Mwanafunzi
aliyehitimu shahada yake ya kwanza ya Usimamizi wa Manunuzi katika
mahafali ya 49 ya chuo cha Elimu ya Biashara CBE Dodoma mwaka 2014
ametangazwa kuwa mwanafunzi wa kwanza aliyeongoza kwa ufaulu kwa kupata
GPA ya 4.92. ambapo aliweza kupata alama A 28 , alama B+ tatu na
alama B moja kati ya masomo 32 ya shahada yake ya kwanza ya
Usimamizi wa manunuzi akifuatiwa na Bw. Peragius Cosmas aliyepata GPA
ya 4.91.
Kwa upande wake
Mwanafunzi mwingine Bw, Peragius Cosmas aliye kuwa akisoma Shahada ya
kwanza ya Uhasibu yeye pia alionyesha maajabu kwa kuweza kupata GPA
ya 4.91 ambapo aliweza kupata alama A 29 na alama B+ tatu kati
ya masomo 32 ya shahada yake ya kwanza ya uhasibu.
Hivi karibuni katika Chuo
kikuu cha Dar es salaam (UDSM) pia tulishuhudia Msichana Doreen
Kabuche aki ]ongoza kwa ufaulu UDSM kwa kuwa Mhitimu bora wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam mwaka 2014, Doreen Kabuche alitangazwa kuwa kinara
kwa ufaulu kwa kupata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada
ya Takwimu Bima (Actuarial Science). Kwa alama hizo, Doreen alipata
wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia
kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano,
Bi.
May Issa akionekana mwenye furaha siku ya mahafali ya 49 iliyofanyika
hivi karibuni katika chuo cha Elimu ya biashara kampasi ya Dodoma.
Bw.
Peragius Cosmas akionekamna mwenye furaha katika mahafali ya 49 ya
chuo cha CBE iliyofanyika hivi karibuni katika Chuo cha Elimu ya
Biashara kampasi ya Dodoma.
Rais
mstaafu wa Serikali ya Wanafunzi CBE kampasi ya Dodoma 2013/2014 Bw.
Remidius Emmanuel (kulia) akimpongeza Bi. May Issa kwa kufanya vizuri
katika masomo yake kwa kipindi chote cha masomo yake.
No comments:
Post a Comment