ZIARA YA KINANA MIKOA YA LINDI NA MTWARA YAINGIZA WANACHAMA ZAIDI YA 40,000 CCM
Wakazi
wa Mtwara mjini wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM
ukiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa
Mtwara mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
Mashujaa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kazi ya CCM ni kuisimamia
Serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mtwara mjini na kuwaa
Mbunge
wa Mtwara Mjini Ndugu Hasnain Murji akieleza utekelezaji wa ilani ya
CCM ulivyotekelezwa vizuri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
viwanja vya Mashujaa ambapo pia alieleza changamoto zinazowakabili
wananchi wa Mtwara mjini hivyo kumtaka Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana kusaidia katika kufanikisha baadhi ya mambo ambayo
yameonekana kukwamishwa na viongozi wa juu serikalini.
Wananchi
wakilizunguka gari alilopanda Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana mara baada ya kumaliza kuhutubia kwenye viwanja vya Mashujaa
Mtwara mjini.
MAPOKEZI YA KINANA MTWARA MJINI
Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana wakati akiwasili Mtwara mjini ambapo alishiriki
shughuli mbali mbali za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
Msafara wa Katibu Mkuu ukielekea Mtwara mjini.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mikindani
mara baada ya kukabidhi leseni kwa madereva 70 wa boda boda waliohitimu
mafunzo chini ya udhamini wa Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji.
MTWARA VIJIJINI
Wananchi
wa kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kijiji hicho kinachopakana na nchi
ya Msumbiji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji
cha Kitaya kilichopo mpakani na nchi ya Msumbiji ikiwa sehemu ya ziara
yake mkoani Mtwara ambapo anakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
pamoja na kujenga na kuimarisha chama.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya
Nanguruwe ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna sheria
zinazomkandamiza mkulima inabidi zitazamwe upya kwani zisipobadilishwa
mkulima atakuwa anakandamizwa kila siku na kutoona faida ya kuwa mkulima
wa korosho.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye
akiwasalimia wakazi wa kata ya Nanguruwe wakati wa ziara ya Katibu Mkuu
wa CCM kwenye wilaya ya Mtwara Vijijini,tarehe 28 Novemba 2014.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mnara wa shujaa
Ahamad Mzee aliyepambana na Wareno waliokuwa wanataka kuivamia Tanzania
mwaka 1972 mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
TANDAHIMBA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa
Tandahimba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa zao la korosho lina
hadithi nyingi sana na njia pekee ya kuleta ukombozi kwa mkulima ni
kujenga kwa viwanda vya kutosha vya kubangulia Korosho nchini pia
aliwataka wazazi wa Tandahimba kusisitiza elimu kwa watoto wao kwani
ndio mkombozi pekee atakayekuja kuwakomboa kwenye maisha yao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akihutubia wakazi wa
Tandahimba ambapo aliwaambia wasihadaike na wapinzani ambao muda wao wa
ujana wameutumia wakiwa CCM na uzeeni kuingia upinzani na kuanza kuhadaa
watu walioishi kwa amani kwa muda mrefu.
Wananchi wa Tandahimba mkoani Mtwara wakifuatilia kwa makini hotuba za
viongozi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana ambaye anazunguka nchi nzima kukagua na kuimarisha uhai wa Chama.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya
Mndimba wakati waujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mdimba wilayani
Tandahimba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizorudishwa na wapinzani kata ya Mdimba wilaya ya Tandahimba.
NEWALA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaonyesha wananchi wa
Mkwedu kadi ya CUF iliyorejeshwa kwake na Hakika Ibrahim ambaye
alirudisha kadi hiyo baada ya kuona na kuelewa utekelezaji wa ahadi za
CCM unavyokwenda vizuri.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionnyesha kadi juu zilizorudi
kutoka upinzani ambapo wanachama hao kutoka upinzani wameahidi
kushirikiana na CCM kwa ajili ya kuleta maendeleo yaTengulengu wilayani
Newala.
Aliyekuwa
Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu Adam Lawi
Nangwanda Sijaona akivua nguo za Chadema mbele ya Katibu wa NEC Itikadi
na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye.
Wananchi
wakishangilia kurejea kwa Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema
wilaya ya Newala Ndugu Adam Lawi Nangwanda Sijaona kwenye mkutano wa
hadhara uuliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo Newala
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Newala kwenye
viwanja vya Mahakama ya Mwanzo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa
Serikali lazima itafute namna ya kuhakikisha uzalishaji wa korosho wote
unafanyika nchini kwa kujenga viwanda vya kutosha vya korosho.
Aliyekuwa
Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu Adam Lawi
Nangwanda Sijaona akiwa amekabidhi kadi yake na ya mkewe kwa Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
NANYUMBU
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mangaka
wilaya ya Nanyumbu ambapo aliwaambia CCM ya sasa itakuwa kali kuliko
wakati wowote na itaisimamia serikali na kuipongeza inapofanya vizuri na
itakapofanya vibaya itasemwa.
No comments:
Post a Comment