Mkoa wa Arusha Umetekeleza agizo
la raisi la ujenzi wa maabara kwa asilimia 80% hadi Novemba 30 mwaka huu
ambapo hadi kufikia desemba,10 watakuwa wamekamilisha kwa asilimia 90%
ya ujenzi huo.
Hayo yalibainishwa na Katibu tawala msaidizi wa mipango na
uratibu Anza Amen Ndossa ofisini kwake wakati akiongea na waandishi wa
habari na kusema kuwa wilaya ya Karatu ilikuwa nyuma katika uhamasishaji
kutokana na malumbano ya kisiasa.
Ndosa alisema kuwa mkoa wa Arusha unajumla ya shule 138 za
sekondari za serikali ambapo mahitaji ya vyumba vya maabara ni 414
ambapo vilivyokamilika ni 105 sawa na asilimia 25% huku ambavyo vipo
katika hatua mbalimbali ya ukamilishaji ujenzi na uwekaji wa vifaa ni
309 .
Alibainisha kuwa Halmashauri ya jiji la Arusha ndio inaongoza
ikiwa na shule 24 huku mahitaji ya vyumba vya maabara ni 72 ambapo
vilivyokamilika ni 15 huku 57 vipo katika hatua mbali mbali za
ukamilishaji.
Ndossa,alisema kuwa wilaya ya Ngorongoro ina jumla ya shule 10
huku mahitaji ni vyumba 30 vilivyokamilika 12 huku 18 vipo kwenye hatua
mbali mbali za ukamilishaji.
Alisema kuwa wilaya ya Longido inajumla ya sekondari 7 mahitaji
ni vyumba 21 vilivyokamilika ni 3 huku 18 vipo kwenye hatua mbali mbali
za ukamilishaji
Aliendelea kusema kuwa Halmashauri
ya Arusha DC, ina Sekondari 26 mahitaji ni vyumba 78 vilivyokamilka 23
huku 55 vipo katika hatua mbali mbali,wilaya ya Monduli ina sekondari 13
mahitaji ni vyumba 39 vilivyokamilika ni 15 huku bado24 vipo katika
hatua mbalimbali.
Karatu sekondari 29 mahitaji 87
vilivyokamilika11 huku 76 vikiwa katika hatua mbali mbali za
ukamilishaji,akamalizia na halmashauri ya Meru ina sekondari 29 mahitaji
ni 87 huku 26 vikiwa vimekamilika na vilivyo kwenye hatua ya
ukamilishaji ni 61.
Ndossa,alisema kuwa ziara aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha,
Magesa Mulongo, aliyoifanya Oktoba 15 mwaka huu imesaidia kubadilisha
mitizamo ya wananchi wa Karatu na kuamua kuitikia wito wa kuchangia
ujenzi wa maabara ambao awali walikuwa wakisuasua kutokana na siasa .
Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa
alikutana na baraza la madiwani pia wananchi na kuwaeleza kuwa swala la
ujenzi wa maabara sio swala la chama bali ni swala la maendeleo na hivyo
watoto watakaoshindwa kufanya mazoezi na mitihani ya sayansi kutokana
na ukosefu wa maabara ni wao hivyo ni jukumu lao kuchangamkia ujenzi huo
wa maabara.
“Ujenzi wa maabara umeathiriwa na
ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wahamasishaji wakubwa wa
maendeleo ambao ni wenyeviti wameingia kwenye kampeni za uchanguzi hivyo
ushiriki wao kwenye kuhamsisha ujenzi wa maabara unakuwa ni
mgumu’’alisema Ndossa..
Ndossa,alisema kuwa wananchi
wamepata mwamko wa uchangiaji baada ya ziara hiyo ya mkuu wa mkoa,japo
zoezi hilo limegongana na uchaguzi wa serikali za mitaa,vitongoji na
vijiji ambapo wenyeviti wa vijiji ndio wasimamizi wa uhamasishaji na
ukusanyaji wa michango ya ujenzi huo.
Alisema kuwa wananchi wamepata
mwamko wa uchangiaji japo zoezi hilo liligongana na uchaguzi wa serikali
za mitaa,vitongoji na vijiji ambapo wenyeviti wa vijiji ndio wasimamizi
wa uhamasishaji na ukusanyaji wa michango ya ujenzi huo.
Aliongeza kuwa ifakapo Desemba 9
mwaka huu wakati wa maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru mikoa na wilaya
zitatakiwa kutoa taarifa ya utekelezaji wa agizo la rais kuhusu ujenzi
wa maabara katika shule zote za sekondari nchini
No comments:
Post a Comment