Mkuuu
wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa, Shadrack Mwakalila
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo, kuhusu mipango na masuala mbalimbali ya chuo hicho. Kushoto ni
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Thomas Ndaluka. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
………………………………………………………………………………………
Dotto Mwaibale
CHUO cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimeiomba Serikali kurudisha utaratibu wa
viongozi mbalimbali wa Serikali kwenye kupata mafunzo ya maadili na
uongozi katika chuo hicho.
Hayo
yalibainishwa na Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila wakati
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi.
“Tulikaa
na kushauriana na wenzangu ambapo tulionelea ni muhimu kuiomba serikali
kurudisha utaratibu huo ili kuwanoa viongozi wetu hasa katika eneo la
maadili” alisema Mwakalila.
Alisema
wana walimu waliobobea kitaaluma na wenye uwezo wa kutoa mafunzo hayo
kwa viongozi hao na wangependa mafunzo hayo yaanze haraka iwezekanavyo.
Profesa
Mwakalila akiongelea kuhusu mipango ya chuo hicho alisema wamejipanga
kuhakikisha mipango yote iliyopangwa inakwenda vizuri hususani suala la
kuongeza hosteli.
Alisema
chuo hicho kinauhaba mkubwa wa hosteli kwa ajili ya wanafunzi ambapo
baadhi yao wamepanga uraiani jambo ambalo si zuri hivyo shauku yao ni
kuona wanazingongoza ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Akiongelea
kuhusu udahili wa wanafunzi alisema ni mzuri na kuwa unategemea na
nafasi ya mwanafunzi muombaji kulingana na somo analotaka kusomea.
“Tunachangamoto
za hapa na pale lakini kubwa ni ruzuku ndogo tunayopata toka serikalini
ambayo haikidhi mahitaji ukilinganisha na mahitaji kwa mfano ikitolewa
ruzuku ya sh.milioni 100 tunapata milioni 50 jambo ambalo linasabisha
kukwama kiuendeshaji” alisema Mwakalila.
Alisema
chuo hicho kilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 6 ya mwaka 2005 ambapo
ilianza kutumika rasmi Oktoba 1 mwaka 2005 kwa mujibu wa Tangazo la
Serikali namba 433 la Desemba 23, 2005.
Alisema
chuo hicho kinamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kuwa majukumu yake makuu
ni pamoja na kutoa mafunzo katika fani za Sayansi Jamii kwa kiwango cha
cheti, Stashahada na shahada, mafunzo ya uongozi, mafunzo ya elimu ya
kujiendeleza kielimu, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaaluma kwa
sekta ya umma na sekta binafsi.
No comments:
Post a Comment