Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Mazingira Binilith Sanato Mhenge (kusshoto) akipokea
mapendekezo ya asasi za kiraia kuelekea mkutano wa kimataifa wa Tabia
Nchi kutoka kwa mwenyekiti wa bodi wa Forum CC Euster Kibona ofisini
kwake jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Mazingira na Naibu wake Ummy Ali Mwalimu wakimsikiliza meneja
mwezeshaji wa Taasisi ya Forum CC Rebeca Muna wakati wakipokea
mapendekezo ya asasi za kiraia kuelekea mkutano wa kimataifa wa Tabia
Nchi unaoendelea kufanyika Lima nchini Peru.
Ujumbe wa Forum CC ukiongozwa
na meneja mwezeshaji wake Rebeca Muna( kushoto), katika picha ya pamoja
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mazingira Binilith
Mahenge(wapili kutoka kushoto) na Naibu Waziri wake Ummy
Mwalimu(katikati), pamoja na mwenyekiti wa bodi ya Forum CC Euster
Kibona (wa pili kutoka kulia) na ofisa maendeleo wa Forum CC Adam
Anthony. wakati wa makabidhiano ya mapendekezo ya asasi za kiraia
kuelekea mkutano mkuu wa kimataifa wa TabiaNchi.
Akiwasilisha mapendekezo hayo mbele ya waziri mwenye dhamana
na Mazingira Mwenyekiti wa bodi ya Forum CC Euster Kibona amesema
serikali inapaswa kubainisha mapendekezo ya kupunguza makali ya
uharibifu wa mazingira kwa nchi zilizoendelea. Pia nchi zilizoendelea
zikubali kuwepo na makubaliano ya kisheria na kuheshimu kanuni juu ya
masuala yote ya mazingira.
Kibona ametoa wito kwa viongozi wa
dunia na Afrika kuwashirikisha wadau wengine katika mchakato wa
mikataba ya kimataifa ili kupunguza manung’uniko ya kutoshirikishwa kwa
wadau. Pia amesema nchi zilizoendelea zinapaswa kutoa fedha ,teknolojia
na kujenga uwezo juu ya kukabiliana na janga la uharibifu wa mazingira.
No comments:
Post a Comment