Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo akizungumza na waandishi wa habari |
Mwenyekiti
wa Chama cha Soka mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo amempa siku saba kocha
wa timu ya Mwadui Jamhuri Kihwelo amuomba radhi kwa kile alichodai
kuwa ametoa lawama zisizo za kweli dhidi yake kupitia vyombo vya habari.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kitumbo alisema amesikitishwa na taarifa
alizozitoa kocha huyo dhidi yake zinazomhusisha kuwa amekuwa akileta
vurugu katika michuano ya ligi daraja la kwanza kwa madai kwamba amekuwa
akifanya fitina kupitia kuwahonga fedha waamuzi ili timu mbili za
mkoa wa Tabora Rhino Rangers na Polisi Tabora ziweze kufanikiwa kuingia
ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.
Kitumbo
kupitia vyombo vya habari amemtaka kocha huyo Jamhuri Kihwelo
kuthibitisha madai yake vinginevyo atamchukulia hatua zinazostahili kwa
kile alichodai kuwa kiongozi huyo wa timu ya Mwadui amesema uongo.
Alisema
kitendo cha kocha huyo kuelezea tuhuma dhidi yake kupitia Star Tv
katika kipindi TUONGEE ASUBUHI ambazo alidai kuwa zimemharibia mwenendo
wa kazi zake si za kweli na kuwataka watanzania kutomwamini kocha huyo
ambaye si mkweli.
“Naomba
kocha Jamhuri Kihwelo aniombe radhi kwa muda wa siku saba na ninampa
siku saba kuanzia leo tarehe 3 Desemba 2014 na kama asipofanya hivyo
asinilaumu kwa hatua nitakazozichukua,najua kuwa TFF wananisikia kwa
haya ninayoyasema nitamfikisha kwenye vyombo vyenye mamlaka ya soka
viweze kumshughulikia”alisema Kitumbo.
No comments:
Post a Comment