Muongozaji
wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi, Jordan Riber akizungumza katika
uzinduzi wa tamthilia hiyo Sehemu ya pili kwenye ukumbi wa Cinemax
Century jijini Dar es salaam.
MC wa shughuli ya uzinduzi wa Siri ya Mtungi 2, Ambi Lusekelo akimtambulisha muigizaji nyota wa tamthilia hiyo, ChecheKatibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo Katikati na wadau wa Filamu Tanzania waliohudhuria
katika uzinduzi huo wakifuatikia hotuba bali mbali zilizotolewa wakati
wa uzinduzi wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi awamu ya pili.
Maofisa
kutoka kampuni ya John Hopkins University For Communication Programs
(JHU CCP) ambao moja wa wadhamini wa tamthilia hiyo katika picha ya
pamoja.Le
Mutuz akiwa na mmoja wa waigizaji wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi awamu
ya pili Richa Adhia, Msemaji wa Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda na
Muigizaji mkongwe nchini, Mwita nao walikuwepo katika uzinduzi huo
Waigizaji wa Tamthilia ya Siri ya Mtungi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya uzinduzi rasmi kwenye ukumbi wa Cinemax Century
…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Bodi ya
Filamu Tanzania imewataka waandaaji wengine wa fani hiyo kuiga mfano wa
waandaaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi, Shirika Lisilo la Kiserikali
(NGO ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) kwa kutoa
filamu yenye mafundisho mbali ya kuburudisha.
Kauli hiyo
imetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo
kupitia kwa mwakilishi wake, Beatrice Sumari kwenye ukumbi wa Cinemax
Century wakati wa uzinduzi rasmi uliowashirikisha wadau wa fani hiyo,
wadhamini na waandaaji.
Sumari
alisema kuwa Tamthilia ya Siri ya Mtungi Msimu wa Pili mbali ya
kuburudisha, pia imetoa ajira kwa Watanzania wengi, pia imeleta
changamoto kuhusiana na mabadiliko ya tabia kwa jamii.
“Filamu
imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, hii ni fursa kwa wadau wa fani
hiyo kuiga MFDI-Tanzania kwa kuleta katika jamii filamu yenye ubora huu,
naomba wengine wafuate nyayo zao,” alisema Sumari.
“Filamu hiyo
ina ubora wa picha, sauti, maudhui na mfuatano wa matukio wa kipekee na
kuleta burudani ya aina yake.. ni tamthilia ambayo ukianza kuangalia,
hauta kinai na kuwa na hamu ya kufuatilia kile kinachofuata,” alisema.
Afisa kutoka
Taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Ana Bodipo alisema
kuwa wanajisikia furaha kudhamini tamthilia hiyo ambayo imezungumzia
maisha halisi ya Mtanzania.
Bodipo
alisema kuwa alisema kuwa tamthilia hiyo inaelekeza jamii kuhusiana na
ugonjwa hatari wa Ukimwi na kwa wao ni moja ya nyenzo ya kushiriki
katika masuala ya afya katika maeneo mbalimbali nchini.
“Matukio
mengi katika tamthilia hii yana akisi taswira ya kweli katika jamii na
na kuwafanya wafuatiliaji kupata somo halisi kutokana na changamoto
mbalimbali,” alisema Bodipo.
Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka taasisi ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa wamefuraishwa na mapokeo ya tamthilia hiyo pamoja na kuhitimisha na kufichua kilichopo katika mtungini.
alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.
Kamin alisema
kuwa kukamilika kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono wa the
John Hopkins University Centre for Communication Programs (JHU CCP)
ambao walitoa uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi ya
Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii na
MFDI.
Mwisho….
.
No comments:
Post a Comment