Mtayarishaji
wa tamthilia ya Siri ya Mtungi Louise Kamin kutoka Shirika Lisilo la
Kiserikali la Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ)
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na msimu wa
pili na wa mwisho wa tamthilia hiyo. Kutoka kulia kwa Kamin ni Karabani
(Muongozaji), Cheche (Muigizaji), Jordan Riber (Muongozaji). Kutoka
kushoto ni Goldliver Gordian (cheusi) na David Michael (Duma). Cheche akizungumza katika mkutano huo
………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Msimu wa pili wa tamthilia ya Siri ya Mtungi itazinduliwa rasmi Desemba 7 kupitia televisheni ya Taifa (TBC).
Akizungumza jijini jana,
Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka Shirika Lisilo la
Kiserikali la Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ)
alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi
kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.
Kamin alisema kuwa kukamilika
kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono wa the John Hopkins
University Centre for Communication Programs (JHU CCP) ambao walitoa
uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi ya Misaada ya
Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii na MFDI.
Alisema kuwa sehemu hii ndiyo
inatoa majibu ya msimu wa kwanza na kuwataka mashabiki watamthilia hii
kuangalia TBC kuanza saa 12.30 jioni kupitia TBC.
“Msimu wa kwanza wa tamthilia ya
Siri ya Mtungi uliwavutia watu wengi wa ukanda wa Afrika Mashariki na
kuwaachia maswali kibao na hii imetokana na tamthilia kubeba vionjo
halisi vya maisha katika jamii na hasa kwa wakazi wa mikoa ya Pwani ya
Tanzania,” alisema Kamin.
Alisema kuwa mapokeo mazuri
kutoka kwa watazamaji kuliwapa nafasi ya kuingia katika vipengele saba
vya tuzo za M-Net Africa Magic Viewers Choice Awards mwaka 2014 ambavyo
ni TV Series, Make Up, Wardrobe, Art Direction, Sound Editor, Acting,
and Indigenous Language Series.
“Msimu wa kwanza ulikuwa hewani
katika vipindi vya miaka miwili tangu mwezi Desemba mwaka jana kupitia
vituo vya televisheni vya ITV/EATV na baadaye kurushwa hewani kupitia
DTV, TV1, MNet Africa Magic, Maisha Magic kabla ya msimu huu kupitia
televisheni ya TBC,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamin, mpaka sasa
wanajivunia kupata mapokeo mazuri kwenye mitandao ya kijamii na hasa
facebook kwa kupata mashabiki 200,000 na kwenye YouTube ambapo tumepata
watazamaji zaidi ya 500,000 kwani tamthilia hii imepata umaarufu mkubwa
kwa kutazamwa na mashabiki wengi kuliko vipindi mbali mbali vya
televisheni hapa nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema kuwa Siri ya Mtungi ni
hadithi ya Kitanzania ambapo wametumia siku 86 kukamilisha kurekodi.
Alisema mbali ya kuwashirikisha waigizaji maarufu kama yvonne Cherie
maarufu kwa jina la Monalisa, pia imewashirikisha warembo maarufu kutoka
Miss Tanzania kama Richa Adhia na Jokate Mwegelo.
“Tumetoa ajira kwa waigizaji 60 ambao walipatikana baada ya mchujo wa watu 2,500,” alisema.
No comments:
Post a Comment