Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh,
Mwantumu Mahiza siku ya jumamosi wiki hii anatarajia kuongoza Bonanza la
Wanavyuo linaloendea sehemu mbali mbali na ikiwa ni sehemu ya tatu kwa
kanda ya kaskazini inayoendelea lwemye viwanja mbali mbali chini ya
Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o Ltd kwa
kushirikiana na kituo bora cha Matangazo TIMES FM 100.5.
Bonanza hilo ambalo ni kwa ajili ya kupata timu zitakazoshiriki
michuano ya NACTE linatarajiwa kuwa gumzo kwa mkoa wa Pwani kutokana na
mfumo wake uliobuniwa kiufundi na waandaaji ambapo timu mbali mbali za
Viongozi wa Serikali na zile za mkoa upata fulsa ya kushiriki pamoja kwa
kufanya michezo ya soka, kikapu,netball pamoja na Voleyball.
Akizungumzia bonanza la jumamosi Mratibu wa Michezo Vyuoni,
Mpalule Shaaban alisema kuwa Mh, Mwantumu anatarajia kufanya Uzinduzi wa
Michezo hiyo kwa Mkoa wa Pwani kutokana na kwamba sasa Michezo hiyo
itafanyika kila mwaka Sehemu mbali mbali za Tanzania.
“Ni heshima ya pekee ambayo Serikali imetoa kwa Vijana wetu wa
vyuo vya elimu ya kati kushiriki michezo, kumbuka kwamba michezo hii
aijawahi kuwepo tangu NACTE imeanzishwa hivyo hii ni fulsa ya pekee
tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba tunahamasisha michezo hii wakati
wote ili vijana wanaojiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi, Veta, na wale
wa ngazi ya Diploma kushiriki michezo vyuoni”alisema Mpalule.
Sehemu ya pili imefanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya
ustawi wa jamii kijitonyama tarehe 29/11/2014, ambako Vyuo mbalimbali
vya NACTE mkoa wa dar es salaam, vilicheza katika michezo ya soka,
Basketball, Voleyball na netball,katika kutafuta timu zitakazoshiriki
ligi ya NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015.
sehemu ya kwanza Ilizinduliwa kwenye chuo cha DIT tarehe
22/11/2014 mwezi huu na kusisimua wengi katika Michuano lutokana na kuwa
na mfumo wa mtoano kuwa kivutio kwa Wachezaji na Mashabiki ambao wengi
wao ni wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali wanaofika kushuhudia michuano
hiyo inayoendeshwa kwa ubunifu wa hali ya juu.
Vyuo vilivyokwisha cheza ni Institute of Adult Education,
Institute of Social Work (ISW) – DSM, Lugalo Military Medical School –
Dsm, St. Joseph College (University), Dar es salaam City College
(DACICO, Dar-es-Salaam School of Journalism (DSJ) – DSM, National
Institute of Transport (NIT) – DSM, Bandari College – DSM,huku timu
mwalikwa ikiwa ni Timu ya wafanyakazi wa PPF Dsm.
Vyuo vingine ambavyo tayari
vimemaliza michezo yao ya awali ni pamoja na IFM ,DIT, CBE,
Muhimbili,TRA, Mlimani Profesianal,na Royal College, waliokuwa kundi la
kwanza lililofanyika viwanja vya chuo cha DIT akiba Posta.
Aidha vyuo vyote vinavyohusika na michezo ya wiki hii zimetakiwa
kuwahi Viwanjani ili kukamilisha taratibu za ukaguzi kabla ya michuano
hiyo ya mtoano kuanza na ikumbukwe kwamba michuano hiyo inaendeshwa kwa
mfumo wa Bonanza na inafanyika kila siku za jumamosi kutokana na
wanafunzi kuwa masomoni katika siku za kawaida.
kila mwaka michuano hii itakuwa ikifanyika kwa kushirikisha vyuo
mbali mbali vya elimu ya kati hapa nchini Tanzania na vilivyopata
usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za Tanzania kupitia
vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa wavulana na
wasichana ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya
mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA
ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER
COLLEGE DAR ES SALAAM.
Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa
ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling,
Mashindano ya Vipaji kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi
kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha, na
Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na
kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na
washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila
mmoja.
Wadhamini aliojitokeza mpaka sasa na kuonyesha nia ya kusaidia
mashindano hayo ni pamoja na Coca Cola, Vodacom, MLONGE BY MAKAI, CXC
–Tours,Bonga Resort & Hoteli, Ikondolelo Hoteli, na 100.5 Times
Fm.
lakini hata hivyo dirisha la wadhamini bado liko wazi kwa maana
bado gharama ni kubwa za uendeshaji ambapo wajitokeze waweze kusaidia
michezo hii iliyoanza kwa shamrashamra nyingi na kuwa na mvuto kwa
watazamaji ususani wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliojitokeza.
No comments:
Post a Comment