Baadhi ya viongozi mashuhuri na wajumbe walihudhuria mkutano huo
………………………………………………………………………………………………………………………………..
KATIBU Mkuu wa CCm Ndg. Abdulrahaman Kinana , amekipongeza
Chama Cha ZANU PF Cha Zimbabwe kwa kusimama imara licha ya Changamoto
mbalimbali zimazoikabili Zimbambwe ikiwemo vikwazo vya kiuchumi ambavyo
vimewekwa dhidi ya nchi hiyo.
Amewataka wana ZANU PF kuendelea
kuunga mkono chama chao na kuongeza mapambano dhidi ya maadui wote
wanaotaka kurudisha nyuma jitihada za kupigania maslahi ya nchi yao.
Akisoma salamu za mshikamano za
Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano Mkuu wa ZANU PF unaofanyika mjini
Harare Ndg. Kinana aliwakikishia wana ZANU PF na wana Zimbabwe wote kuwa
katika mapambano hayo CCM iko nyuma yao na kwamba haitaacha kupaza
sauti dhidi ya vikwazo vya uchumi ilivyowekewa Zimbabwe.
Alisema vikwazo hivyo having uhalali na kwa ujumla wake vinatoa adhabu isiyo ya haki kwa Wananchi wa Zimbabwe wasio na hatia.
Ndugu Kinana alimpongeza Rais
Mugabe ujasiri na kwa msimamo wake usioyumba wa kupigania maslahi ya
wana Zimbabwe licha ya vitimbi vya wapiga maendeleo.
Alisema ujasiri na msimamo wa
Mugabe pamoja na Chama anachokiongoza Cha ZANU PF ndiyo uliowezesha
Zimbabwe kusimama ilivyo hivi sasa kama Taifa huru na lisilikubali
kuyumbishwa.
Alisema Mugabe na Chama chake
wameonyesha kwa mfano kwamba kume watu wakisimama imara chini ya uongozi
wa chama imara hakuna anayeweza kukwamisha nyendo zao za kimapinduzi
zinazoendana na matakwa ya umma.
Akizungumzia ushindi wa kishindo
wa ZANU PF kwenye uchaguzi Mkuu June mwaka jana Kinana alisema hicho
ndicho kiashiria cha kukubalika kwa Chama na sera zake.
Alisema CCM inaipongeza ZANU PF
kwa ushindi huo na kwamba wana CCM wanajisikia fahari sana wanapoona
ZANU PF ikiendelea kukua na kuimarika.
Aisha Ndg. Kinana alimpongeza
Rais Mugabe na kueleza kuwa CCM na Watanzania kwa ujumla wanafurahishwa
na msimamo wa dhati alionyesha Rais Mugabe katika majukwaa mbalimbali
ikiwemo mkutano wa wakuu wa nchi za SADC uliofanyika Victoria Falls wa
kueleza umuhimu wa kutambua na kuheshimu mchango wa Mwalimu Nyerere
katika ukombozi wa Afrika na hasa kusini mwa Afrika.
Hotuba ya Ndg. Kinana ilipokelewa
kwa shangwe na furaha kubwa sana na wajumbe wa mkutano huo ambao mara
kwa mara walishangalia kuashiria kuridhika na kauli za kimapinduzi na
kidugu kutoka kwa wana CCM.
Ndugu Kinana na ujumbe wake
wataondoka kesho kurejea nyumbani. Ujumbe wa Katibu Mkuu kwenye mkutano
ulimhusisha pia Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa CCM Ndg. Phares
Magesa na afisa wa makao makuu ya CCM Ndg. Thobias Mwilapwa
No comments:
Post a Comment