Na: Mwandishi Wetu
Chuo cha njuweni Institute na Eden Hill College
vyote vya mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki viliweza kutama kwenye Bonanza la Wanavyuo lililofanyika kwenye viwanja vya Shirika la elimu
Kibaha ikiwa ni sehemu ya tatu kwa kanda ya kaskazini chini ya Kampuni ya Miss
Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o Ltd .
Timu ya Chuo cha Njuweni kwa
upande wa mchezo wa mpira wa miguu ndiyo iliyong’ara zaidi huku ikifuatia na
timu ya chuo cha Eden hill waliokuwa washindi wa ili na kujihakikishia kuingia
kwenye hatua ya timu 32 bora za NACTE zitakazoshiriki kwenye fainali kubwa ya
Kanda ya Kaskazini itakayofuata baada ya awamu hii ya mchujo wa awali
kumalizika katika mfuno wa Bonanza.
Akizngumzia Bonanza hilo ambalo
ni kwa ajili ya kupata timu zitakazoshiriki michuano ya NACTE, Mkurugenzi wa chuo cha Njuweni Institute
Hoteli, Bwana Saidi Mfinanga aliema kuwa ni jambo la kupendeza kutokana na
kukutanisha vyuo mbalimbali kwa ajili ya kushiriki kwa pamoja michezo
inayojenga ubora wa afya zao lakini pia ikiwa ni njia ya kuwaunganisha
wanavyuo, Makampuni pamoja na wadau mbalimbali.
“mfumo huu unapendeza sana, na
hata niwapongeze walioanziasha utaratibu huu wa vyuo vya elimu ya kati
kukutanishwa na michezo, mimi binafsi hata chuo changu kisingetwaa nafasi ya
kwanza lakini ningebaki na amani tu kwani huu ni mwanzo, lakini tuwapongeze
hawa walioweza kubuni njia hii sahihi na uliokuwa tukiitamani wakati mwingi,
mimi vijana wangu unisumbua sana inapofika wakati fulani wakidai niwatafutie
timu wakacheze nao, huwa inasumbua sana lakini sasa ufumbuzi umekuja na si
kwangu tu nadhani hata kwa wenzangu, tuwape ushirikiano hawa waliobuni hili
jambo, na pia sisi wenyewe tujitunzie heshima zetu wakati tunashiriki siku zote
katika michezo hii, michezo ni furaha, amani na upendo hivyo tushiriki kwa
Upendo” alisema Mfinanga
Jumla ya Vyuo nane vilishiriki
katika bonanza hilo linaloendelea katika siku za jumamosi kwa kushirikisha
michezo ya Soka, Netball, Basketball na Voleyball, ambapo kwa upande wa mchezo
wa Netball ni timu ya chuo cha Njuweni na Dacico waliofanikiwa kufuzu hatua ya
pili huku Heden hili pia ikiibuka kidedea katika mchezo wa Basketball.
Aidha kwa upande wa mchezo wa
Voleyball ni chuo cha Njuweni waliofanikiwa kuingiza timu huku vyuo vingine
vikishindwa kuwasilisha wachezaji na hivyo kuwafanya njuweni kuingia hatua ya
pili bila jasho katika mchezo huo.
Mratibu wa Michezo hiyo Vyuoni,
Mpalule Shaaban alisema kuwa Michezo hiyo imeanza kwa kusuasua kutokana na
washiriki wengi (Wanafunzi) kutokuwa na vifaa vya michezo jambo linalowapa tabu
wakati wawapo michezoni.
“Jambo ni jema na hata mwitikio
kwa wanavyuo pia ni mkubwa, lakini tatizo ninalolitazama hapa ni ukosefu wa
vifaa vya michezo kwa vyuo pamoja na wachezaji wao, wengi hata viatu vya mchezo
husika hawana wanacheza na viatu visivyokuwa vya mchezo husika, jezi wakati
mwingine wanatumia hazina namba, hivyo bado ni tatizo kwa upande mwingine, ila
kuhusu mwitikio wao kama wanafunzi wamependa sana michezo hii, kubwa tu mimi
niombe kwa serikali na wadhamini wajitokee wasaidie michezo hii ya vyuo,
Wanavyuo ndiyo wafanyakazi wa kesho hapo Ofisini kwako, sasa ni nani anapenda
kuwa na mfanyakazi goigoi? Na hata watu binafsi kama wewe ni mdau jitokeze
kusaidia vifaa vya michezo” alisema Mpalule.
Na kuongeza kwamba, heshima hii
ni ya pekee ambayo Serikali imetoa kwa Vijana wa vyuo vya elimu ya kati
kushiriki michezo, haijawahi kuwepo tangu NACTE imeanzishwa hivyo hii ni fulsa
ya pekee tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba tunahamasisha michezo hii wakati
wote ili vijana wanaojiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi, Veta, na wale wa ngazi
ya Diploma kushiriki michezo vyuoni.
Sehemu ya Nne
sasa inatarajiwa kufanyika Kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
jumamosi hii ya tarehe 13 mwezi huu kwa kushirikisha vyuo kumi mbali mbali, University
Computing Centre - Dar es Salaam, institute
of Tax Administration (ITA) - DSM, National
College of Tourism - Dar es Salaam, Law
School of Tanzania,
The Sinon
College - Dar es Salaam, St. Glory
Nursing School - DSM,
Tanzania
Institute of Education - Dar-es-Salaam, Zoom
Polytechnic College - DSM,
Sehemu ya kwanza mpaka sehemu ya tatu
zimefanyika mwezi uliopita kwenye viwanja vya D.I.T, Ustawi wa jamii
kijitonyama na Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha ambako Vyuo mbalimbali vya
NACTE mkoa wa pwani na dar es salaam vilicheza katika michezo ya soka,
Basketball, Voleyball na netball katika kutafuta timu zitakazoshiriki ligi ya
NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015.
Vyuo
vilivyokwisha cheza ni Institute
of Adult Education, Institute of Social Work (ISW) - DSM,
Lugalo Military
Medical School - Dsm, St.
Joseph College (University), Dar es salaam City College (DACICO, Dar-es-Salaam School
of Journalism (DSJ) - DSM, National Institute of
Transport (NIT) - DSM, Bandari College - DSM, Institute of Procurement
and Supply (IPS) - Dar es salaam, Mount Ukombozi Health
Laboratory Assistants School - DSM, Nyerere Institute of
Technology and Innovation - Kibaha (pwani), KAM College of Health
Sciences - DSM, Eden Hill Community
College - Kibaha, Kibaha COTC - Kibaha, na Njuweni Institute of
Hotel, Catering & Tourism Management Kibaha, IFM ,DIT, CBE, Muhimbili,TRA, Mlimani
Profesianal,na Royal College
Ukiachilia mbali michezo hiyo,
michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni
DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji kwa viongozi
wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu,
Mawaziri wa Michezo, Fedha, na Spika , watakaokuwa wakichuana katika
kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto
wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana
na ushindi wa kila mmoja.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment