Radio 5 FM 105.7 imeandaa
“kampeni ya RADIO 5 viwanjani” katika mkoa wa Arusha ambapo
itawakutanisha watangazaji na madjs na wasikilizaji wao katika kumbi za
starehe kwa takribani wiki tano ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru
mashabiki wa Redio hiyo kwa kuwa pamoja kwa mwaka mzima huku mashabiki
wakijipatia zawadi mbalimbali katika kampeni hiyo(katika picha ni
Mtangazaji wa kituo cha Redio 5 Julius Kamafa aliyejizolea umaarufu
mkubwa jijini Arusha kupitia kipindi chake cha funiko base
kinachosikilizwa zaidi na vijana akishow love na msikilizaji wake katika
kampeni ya “Redio 5 viwanjani”ndani ya ACTIVE CLUB – Mbauda jijini
Arusha
Timu kazi ya Redio 5 wakifatilia show
Mtangazaji maarufu aliyejizolea
umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha love cuts Semio Sonyo akiwa
anauliza maswali kwa vijana wa Arusha waliofika katika kampeni ya Redio 5
viwanjani ndani ya ACTIVE CLUB – Mbauda jijini Arusha
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akifurahia jambo katika kampeni ya Redio 5 viwanjani iliyofanyika jijini Arusha
Mtangazaji maarufu aliyejizolea
umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha love cuts Semio Sonyo
akimuuliza maswali shabiki wa redio 5 katika kampeni ya Redio 5
viwanjani yenye nia ya kuwashukuru wasikilizaji wa kituo hicho kwa kuwa
pamoja kwa mwaka mzima
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky
Mwakoyo kushoto akieleza nia ya kampeni hiyo itakayofanyika katika bar
mbalimbali jijini hapa ambapo pia wasikilizaji wa kituo hicho
watajizolea zawadi mbalimbali zikiwemo T-shart,vikombe,vinywaji kutoka
TBL
No comments:
Post a Comment