…………………………………………………………………………………….
Mwandishi wetu,Arusha
WIZARA ya Fedha, imeitaka Bodi ya
Wataalam wa Ugavi na Manunuzi nchni (PSPTB), kutafuta ufumbuzi wa
tatizo la kufanya manunuzi bila kuzingatia thamani halisi ya fedha na
kuwataka waajiri kuacha mara moja kuwaajiri watu wasio na sifa kufanya
kazi hizo
Naibu Waziri wa Fedha,Adam
Malima ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua mkutano wa tano wa mwaka
wa Siku mbili unaofanyika kwenye jengo la Mikutano la AICC jijini Arusha
ambapo aliwataka Wataalamu hao kuzingatia maadili na miiko ya kazi yao.
Amesema katika bajeti ya mwaka
2014/15 serikali imetega bajeti ya Sh trilioni 20 kati ya hizo asilimia
65 hadi za 70 zinatumika kwenye manunuzi ya bidhaa na huduma
mbalimbali,hivyo taaluma hiyo kuwa na umuhimu wa kipee katika kudhibiti
mapato ya serikali yasitumike vibaya.
Awali Mwenyekiti wa Bodi hiyo,
Sr. Dk. Hellen Bandiho, amesema kauli mbiu ya mkutano huo “Thamani
halisi ya fedha za Manunuzi” ikilenga kuhakikisha serikali inapata
huduma bora kulingana na fedha inazotumia ili kuinua uchumi wa nchi.
Amesema Bodi hiyo imezalisha
wataalam zaidi ya 23,000 katika ngazi mbalimbali ambayo ni sawa na
asilimia 47 pekee huku waajiri wengi wakiwa wamewajiri watumishi
wasiosajiliwa na Bodi hiyo.
No comments:
Post a Comment