TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 13, 2014

WASAIDIZI WA KISHERIA KATIKA MASOKO MANISPAA YA ILALA, WAMALIZA MAFUNZO YA SIKU 25 YALIYOANDALIWA NA SHIRIKA LA EfG

Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika lisilo la Kiserikali la Equality For Growth (EfG), Jane Magigita, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo. Kutoka kulia ni Mwakilirishi kutoka Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Doris Gweba, Diwani wa Kata ya Mchikichini Mhe.Riyani na Mgeni rasmi, Leopold Kaswezi.
Mgeni rasmi, Leopold Kaswezi (katikati), akizungumza na wahitimu hao. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mchikichini, Mhe.Riyani na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika lisilo la Kiserikali la Equality For Growth (EfG), Jane Magigita.
Mjumbe wa EfG, Emanuel Tuju akizungumza wakati akitoa shukurani kwa mgeni rasmi.
Muhitimu wa mafunzo hayo, Bakari  Yusuph kutoka soko la Feri, akikabidhiwa cheti chake na mgeni rasmi.
Muhitimu wa mafunzo hayo, Batreti Malemula kutoka soko la Feri, akikabidhiwa cheti chake na mgeni rasmi.
 Soko la Ilala Boma Consolata
Muhitimu wa mafunzo hayo, Mwalimu Halima Kilimo kutoka soko la Buguruni kikabidhiwa cheti chake na mgeni rasmi.
Muhitimu wa mafunzo hayo, Mwalimu Chiku Hamisi kutoka soko la Buguruni, akionesha cheti chake kwa furaha baada ya kukabidhiwa.
Wahitimu wakiwa kwenye hafla hiyo.

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WASAIDIA UJENZI WA MAABARA KATIKA SHULE YA MIHANDE WILAYANI KIBAHA MKOA WA PWANI

Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akimkabidhi, Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa (kulia), bati na rangi zenye thamani ya sh.milioni 3.5 zilizotolewa na mfuko huo jana, kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari ya Mihande ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na maabara. Anayeshuhudia makabidhiano hayo katikati ni Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha.
Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akipeana mkono na Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha wakati akikabidhi msaada huo. Kulia ni   Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa. 
Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akipeana mkono na Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha.   
Hapa ni kubadilishana mawazo baada ya makabidhiano hayo.
Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Jengo la maabara la shule hiyo lililokamilika ujenzi wake.
Jengo la maabara ambalo ujenzi wake unaendelea.
Baadhi ya majengo ya shule hiyo yanvyoonekana.
Jengo la utawala la shule hiyo.
 
Dotto Mwaibale
 
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umeunga jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na maabara kwa kutoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh.milioni 3.5 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari ya Mihande iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Mlandizi wilayani humo jana, Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki wa mfuko huo, Isaya Mwakifulefule alisema mfuko huo umejiwekea utaratibu wa kusaidia kutoa misaada mbalimbali katika  shughuli za maendeleo ya kijamii.
“Mfuko wetu kila kanda nchini wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo na katika hilo mnaweza kuwa mashuhuda kwani siku za hivi karibuni mmeweza kuona tulivyotoa msaada kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (albino)” alisema Mwakifulefule.
Alisema ujenzi maabara katika shule hapa nchini ni muhimu sana katika wakati huu wa ulimwengu wa sayansi na teknolojia ambapo wanahitaji wanayansi wengi kwa utaalamu wa aina mbalimbali hasa katika masuala ya utafiti.
Alitaja vifaa vilivyotolewa na mfuko huo kuwa ni mabati na rangi kwa ajili ya kukamilishia ujenzi wa maabara hizo na alitoa mwito kwa wadau wa maendeleo na mifuko mingine kujitokeza kusaidia eneo hilo kwani kuna mahitaji makubwa ya maabara nchini.
Akipokea msaada huo kwa niana ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa wilaya hiyo, Doris Semkiwa alisema msaada huo utapunguza changamoto ya ujenzi wa maabara kwenye shule hiyo.
Alisema ujenzi wa maabara katika wilaya hiyo umekamilika kwa asilimia 67 na kuwa ujenzi huo unaendelea kwa kasi ambapo wanatarajia kukamilisha kazi hiyo mapema iwezekanavyo.
 
Alisema kwa wilaya nzima yenye shule za sekondari 8 mahitaji ni kuwa na maabara 24 na tayari wamejenga 14 na kuwa fedha zinazotumika kwa ujenzi huo zinatoka katika mapato ya ndani ya Halmshauri, wadau mbalimbali na nguvu za wananchi.
Aliongeza kuwa ujenzi huo utagharimu zaidi ya sh, milioni 400 na kuwa changamoto kubwa ni mapato ya ndani kuwa kiduchu na kuwa kama wangekuwa na fedha za kutosha wangeweza kumaliza kwa wakati ujenzi huo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha aliwashuku LAPF kwa msaada huo pamoja na Halmsahauri kwa fedha za luzuku inazozitoa kila mwezi kusaidia mambo mbalimbali katika shule hiyo na zingine sanjari na ujenzi wa maabara hizo.
“Naishukuru Halmshauri kwa fedha hizo ambazo imekuwa ikitupa kila mwezi kusaidia katika maeneo mbalimbali” alisema Masha. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

DIWANI MATHIUS WA KATA YA MALANGARINI AFUNGA KAMPENI ZA UCHAGUZI KATANI KWAKE

Diwaniwa kata ya Mlangarini, Mathius Manga akizungumza na wananchi wa kata hiyo katikamkutano wa hadhara wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa CCM kwa ajili yakuwachagua viongozi wa  serikali za mitaa utakaofanyika jumapili Desemba14 mwaka huu.
Diwani Manga amewaasa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura wagombea wa CCM kwani wanasifa stahiki za kuwaongoza. 
Aidha amesisitiza kulimnda amani kipindi cote cha uchaguzi na hata matokeo yatakapo tangazwa na kuepuka vitendo vya vurugu. 
 Wananchi wa kata ya Manyire wakimsikiliza diwani wa kata
hiyo hayupo pichani wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa serukali za
mitaa.
 Diwaniwa kata ya mlangarini Mathius Manga akizungumza huku makada wa CCM wakicheza kwa furaha.
 Viongozi wa CCM wakiwa katika mkutano huo.
 Diwani wa kata ya mlangarini Mathius Manga akiwa na viongozi wenzake wa CCM katika mkutano huo.

Uharibifu wa mazingira kutokana na wingi wa mifugo mkoani Katavi wawa tishio

unnamed1
DC Mpanda Paza Mwamlim akiwahutubia wafugaji katika kijiji cha Sibwesa Wilayani Mpanda na kuwasisitiza umuhimu wa hifadhi mazingira na kuwaasa wafugaji.
kupunguza mifugo yao wafuge ufugaji wenye tija,
unnamed 
Baadhi ya maeneo yaliyoathiliwa na uharibifu wa mazingira kutokana na wingi wa Mifugo Katika Halamshauri ya Wilaya ya Wilaya ya Mpanda.(Picha na Kibada Kibada Katavi
………………………………………………….
Na Kibada Kibada –Katavi
Makala
Sekta ya Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi inakabiliwa na Changamoto mbalimbali  hali inayofanya sekta hiyo kutafuta mbinu na mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo ikiwemo uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na wingi wa mifugo uliopo kuliko ukubwa wa eneo la kufugia mifugo hiyo.
Baadhi ya Changamoto hizo ni kuwepo idadi kubwa ya mifugo katika halmashauri,Uzalishaji mdogo wa mazao ya mifugo kama nyama na maziwa na kipato kinachotokana na uwepo wa mifugo hiyo katika Halamshauri.
Changamoto nyingine ni upatikanaji  mdogo wa mbegu bora za mifugo hususani ng’ombe,eneo dogo la malisho ukilinganisha na Idadi ya  mifugo iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Pamoja na kuwepo kwa wingi wa mifugo  pia magonjwa mengi ya mifugo kama ndorobo,ndigana kati na homa ya mapafu nayo ni moja ya changamoto inayoikabili sekta ya mifugo Katika Halmashauri ya Mpanda.
Halmashauri ya Mpanda ambayo ni moja ya Halmashauri katika Mkoa wa Katavi ina idadi ya Ng’ombe wapatao 87,928,mbuzi 44,348,Kondoo 8,712,Nguruwe 2,237, mbwa 7425,na kuku 141.832  hata hivyo uwepo wa mifugo hiyo bado haijatumiwa  vizuri na kubadili maisha ya wakazi wa Halmashauri hiyo na mkoa kwa ujumla kiuchumi na kuinua pato lao kiuchumi.
Tafiti zinaonesha iwapoidadi ya mifugo hiyo iliyopo ikitumiwa vizuri inaweza kuleta tija na kuwaondolea umasikini wananchi katika maeneo husika.
Kwa mantiki hiyo wataalam wa sekta ya mifugo wanayo kazi kubwa mbele yao kuhakikisha wanatumia elimu yao kuwabadili wafugaji waweze kufuga ufugaji wenye tija tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo ufugaji umekuwa wa kutokuwa na tija na kila kukicha imekuwa ni mivutano na migogoro kati ya wakulima na wafugaji ingawa hali hiyo bado haijatokea katika Halmashauri ya Mpanda lakini tunashuhudia maeneo mengi hapa nchini hususani Mkoani Morogoro,wilaya ya Kilosa na Kilombero,Mkoani Pwani ,na Arusha na Tanga wakulima na wafugaji migogoro ya kila mara.
Uwepo wa mifugo mingi katika Halamshauri ya wilaya ya Mpanda pia kumeambatana nanUharibifu wa  mazingira  kutokana na wafugajinhao kuhamahama  na wengine kutumia njia hiyo kwa kufyeka miti na mistu kwa shughuli za kilimo kwa kuwa wafugaji walioko katika Halmsahauri ya Mpanda hao hao ndio wakulima.
Uchunguzi uliofanyika kwa baadhi ya maeneo Mbalimbali Wilayani Mpanda inaonesha maeneo mengi yanaoonekena kuathiri na Uharibifu wa mazingira  na iwapo hatua za  makusudi hazitachukuliwa kwa haraka maeneo hayo yanaweza kugeka jangwa.
Baadhi ya maeneo yaliyoathirwa na uharibifu wa mazingira kutokana na mifugo  ni bonde la Mto Katuma ambao ni tegemeo  kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi hususani Mbuga ya Katavi ya Katavi ambayo wanyama walioko huko hutegemea kupata maji kutoka bonde la mto huo ambalo hutiririsha maji yake kupitia vijito vyake kupeleka hifadhi ya Katavi.
Mbali ya kutegemewa kwa ajili ya maji ya wanyama kama viboko na wengineo pia bonde la mto huo wa Katavi ndilo linalotegemewa kwa kilimo cha mbuga unaozalishwa kwa wingi katika maeneo ya Bonde hilo na kuwasaidia kuwaingizia pato wananchi Mkoani humo.
 
Continue reading →

PINDA AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN NCHINI, ASHIRIKI CHAKULA CHA JIONI NA AKINA MAMA WA (New Millenium Women Group)

unnamed2Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katka picha ya pamoja na washiriki wa maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa na  Umoja wa wake wa viongozi ( New Millenium Women Group) katika chakula cha jioni kilichoambatana na burdani mbalimbali kwenye ukumbi wa Kardinal Rugambwa, Oysterbay jijini  Dar es salaam, Desemba 12, 2014.  Chakula hicho  kiliandaliwa ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya kituo cha  kulea watoto yatima cha Buhangija mkoani Shinyanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed4Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katka picha ya pamoja na washiriki wa maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa na  Umoja wa wake wa viongozi ( New Millenium Women Group) katika chakula cha jioni kilichoambatana na burdani mbalimbali kwenye ukumbi wa Kardinal Rugambwa, Oysterbay jijini  Dar es salaam, Desemba 12, 2014.  Chakula hicho  kiliandaliwa ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya kituo cha  kulea watoto yatima cha Buhangija mkoani Shinyanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed5 Baadhi ya  washiriki wa maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa na  Umoja wa wake wa viongozi ( New Millenium Women Group) katika chakula cha jioni kilichoambatana na burdani mbalimbali kwenye ukumbi wa Kardinal Rugambwa, Oysterbay jijini  Dar es salaam, Desemba 12, 2014 wakijitambulisha baada ya onyesho hilo.  Chakula hicho  kiliandaliwa ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya kituo cha  kulea watoto yatima cha Buhangija mkoani Shinyanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed6 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na na nalozi wa Sweden nchini, Bw.Lennarth Hjelmaker, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba   13, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WABUNGE KUTOKA IRELAND WAKUTANA NA RAIS DR. SHEIN

unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bibi Fionuala  Gilsenan akiongoza ujumbe wa Wabunge wa Ireland walipofika Ikulu Mjini Unguja leo [Picha na Ikulu.] unnamed1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza  na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bibi Fionuala  Gilsenan (wa pili kulia) akiwa na  ujumbe wa Wabunge wa Irelenad walipofika Ikulu Mjini Unguja leo kwa mazungumzo , [Picha na Ikulu.]

MANISPAA YA KINONDONI YAZINDUA HUDUMA YA BURE YA INTERNETI KWA WiFi KWENYE KITUO KIPYA CHA DALADALA CHA SINZA

theNkoromo Blog, Kinondoni
Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imedhihirisha jitihada zake za kwenda na wakati katika huduma zake, baada ya kuamua kutoa huduma ya bure ya mtandao wa intrenet wa WiFi kwenye Kituo kipya cha Mabasi cha Sinza, jijini Dar es Salaam.
Akizindua huduma hiyo, jana, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda alisema, mtandao wa WiFi umeunganishwa kwenye kituo hicho kupitia mkongo wa mawasiliano kupitia Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Mwenda alisema, mtandao huo utakuwepo usiku na mchana na kila mwenye kompyuta au simu zenye uwezo wa kunasa Wi-Fi ataona katika simu au kompyuta yake akitaarifiwa kuwepo mtandao wa bure wa KMC_FREE WiFi.
Alisema, mdau atakachofanya ni kujinga bure na kuendelea kupata taarifa mbalimbali zikiwemo za tovuti ya serikali na ya Manispaa hiyo ya Kinondoni na nyingine zote atakazotaka.
Mwenda alisema, baada ya kuweka mtandao kwenye Kituo hicho, mwakani Manispaa hiyo itaweka mtandao huo wa WiFi kwenye Kata zote 34 za Manispaa hiyo.
Alisema, mradi huo wa WiFi umegharimu sh. milioni 21, na Manispaa hiyo itakuwa ikiendelea kulipia huduma hiyo sh. milioni 2 kila mwezi ambazo itakuwa inalipa kwa mkupuo kwa mwaka.
Kuzinduliwa kwa huduma hiyo, kumeifanya Manispaa ya Kinondoni kuwa ya kwanza nchini kote, na pengine hata Afrika Mashiriki, kutoa huduma hiyo bure tena bila kutumia namba ya siri.
Mwandishi wa habari hii alishuhudia huduma ya aina hii kwa mara ya kwanza alipotembelea nchini China, ambapo WiFi inapatikana bure kwenye simu hata ukiwa barabarani.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akibofya kompyuta kuzindua huduma ya WiFi ya bure kwenye Kituo cha Mabasi cha Sinza, wilayani humo, Ijumaa, Desemba 12, 2014
 Mwenda akizungumza baada ya kuzindua huduma hiyo
 Mwenda akikata utepe kwenye chumba ilimo mitambo ya kuendesha mtandao huo wa huduma ya WiFi kwenye Ofisi za Kituo hicho cha mabasi
 Baadhi ya wafanyakazi katika ofisi hiyo yenye kugawa WiFi
 Kweli: “WiFi ya Manispaa ya Kinondoni inapatikana bure! vijana wakisema baada ya kuipata WiFi iliyozinduliwa kwenye Kituo hicho cha Mabasi
 Vibao vinavyoonyesha Mabasi yaendeko  kutoka kwenye Kituo hicho

MAMA KIKWETE AWATAKA WAKAZI WA WILAYA YA LINDI MJINI KUHAKIKISHA WATOTO WAO WANAKWENDA SHULE

 PICHA NA JOHN LUKUWI
……………………………………………………………………………………..
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
13/12/2014 Wakazi wa wilaya ya Lindi mjini wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanakwenda shule na kusoma kwa bidii kwani Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imejenga shule za kutosha  katika kata zote za wilaya hiyo.
Mwito huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni ya uchaguzi wa Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za mitaa uliofanyika katika Kata za Chikonji na Mingoyo.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema wakati ujenzi wa shule hizo unaanza vyama vya upinzani walizidharau na waliziita za yeboyebu kwa lengo la kuwakatisha tamaa lakini Serikali ya CCM kwa kushirikiana na wananchi hawakukata tamaa na kuendelea na ujenzi.
“Zamani wanafunzi waliokuwa wanajiunga na elimu ya Sekondari walikuwa wachache baada ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hizi hivi sasa kila mwanafunzi anayefaulu mtihani wa darasa la saba anajiunga na elimu ya Sekondari haya ndiyo maendeleo yaliyoletwa na CCM”.
Ili uweze kuendelea ni lazima ukutane na changamoto nasi katika shule hizi tulikutana na changamoto za walimu na maabara, vyuo mbalimbali nchini viliweza kutoa walimu wengi  na kupunguza tatizo la walimu wa masomo ya sanaa na miaka michache ijayo watapatikana walimu wa kutosha wa masomo ya sayansi”, alisema Mama Kikwete.
Aliendelea kusema wakati wa ujenzi wa shule za Sekondari za Kata kulisahaulika ujenzi wa maabara kwa ajili  ya masomo ya sayansi, hivi sasa Serikali kwa kushirikiana na wananchi wanamalizia kazi ya ujenzi wa  maabara katika shule hizo  na hivyo kuwafanya  watoto kusoma masomo ya sayansi kwa fasaha zaidi.
MNEC huyo pia aliwataka wananchi hao kuchagua viongozi wanaofaa kwani uchaguzi ni kwa ajili ya kutengeneza maisha yao kwa  kipindi cha miaka mitano hivyo basi wasiweke rehani maisha yao kwa kufuata mkumbo na kuchagua viongozi wasiofaa.
Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Lindi Adelina Gefi alisema katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji chama hicho kitapata ushindi wa kishindo kwani hadi hivi sasa ndani ya  mkoa huo wagombea katika vitongoji 600, vijiji 80 na mitaa saba wamepita  bila kupingwa.
Gefi alisema CCM inaleta maendeleo na upinzani unachelewesha hivyo basi siku ya uchaguzi ikifika wananchi wajitokeze kwa wingi na kuwachagua wagombea wa chama hicho ili  wawaletee maendeleo.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya  Chikonji mwanachama mmoja aliyejulikana kwa jina la Abdallah Mohammed Kilimbalimba kutoka Chama cha Wananchi (CUF) alijiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Mama Kikwete yupo wilayani humo kwa ajili ya kushiriki  kwenye kampeni na kuwanadi wagombea wa chama hicho wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji  unaotarajiwa kufanyika kesho nchini.