TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 19, 2012

MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI JEREMIAH SUMARI HATUNAYE TENA

Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh. Jeremiah Sumari amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya uvimbe kichwani. Kuzaliwa Marehemu Jeremiah Sumari alizaliwa Machi 2 mwaka 1943 katika kijiji cha Akeri wilayani Arumeru Mkoani Arusha. Elimu yake Alisoma elimu ya msingi kati ya mwaka 1950-1957 katika shule ya msingi Meru Magharibi mkoani humo mwaka 1958- 1964 alisoma katika shule ya sekondari ya Old Moshi Mkoani Kilimanjaro na baadae aliendelea na elimu ya juu huko Uingereza kama ifuatavyo- ACCA, CIS, Certificate in Marketing. Uk, Lincesed Broker (LR), CPA (Tanzania). Utumishi wake Mwaka 1996-2004 alikuwa Mkurugenzi wa bodi ya soko la Hisa Stokck Exchange mwaka 1998-2003 Trustee Privatization Trust, mwaka 1999-2006 alikuwa Mkurugenzi wa bodi Benki ya maeneleo ya Afrika Mashariki, mwaka 2005 mpaka sasa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Januari 4 mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Waziri wa kazi Ajira na Maendeleo ya vijana na mwaka 2008 mpaka 2010 alikuwa Naibu waziri wa Fedha na Uchumi. Marehemu Jeremiah Sumari alikuwa mbunge wa Arumaru Mashariki mpaka umauti ulipomkuta Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi Amen.

AFISA WA MFUKO WA AFYA YA JAMII KUTOKA KANDA YA KUSINI BWN. PATRICK KUHUNGA AKIANDIKISHA WANACHAMA WAPYA KUTOKA WILAYA YA NACHINGWEA MKOANI LINDI BAADA YA UHAMASISHAJI KUHUSU UMUHIMU WA UCHANGIAJI WA HUDUMA ZA MATIBABU KUPITIA MFUKO WA AFYA YA JAMII,WANANCHI WANAPASWA KUELIMISHWA DHANA YA UCHANGIAJI WA HUDUMA ZA MATIBABU.
HII NI SEHEMU YA TANGAZO LINALOTOA MWONGOZO WA MSINGI KWA WANANCHI KUHUSU NAMNA YA UCHANGIAJI UNAVYOWEZA KUFANYIKA SANJARI MATARAJIO YA UWEPO WA UHAKIKA WA HUDUMA YA MATIBABU KWA MWAKA MZIMA,TANGAZO HILI LIPO KWENYE HOSPITALI YA WILAYA YA NACHINGWEA KAMA LILIVOKUTWA NA MPIGA PICHA WETU.
WANANCHI WAKIELIMISHWA KUHUSU UMUHIMU WA KUCHANGIA HUDUMA ZA MATIBABU UFANYA MAAMUZI YENYE TIJA KAMA AMBAVYO PICHANI JUU WANANCHI WAKILIPA MICHANGO YAO YA MWAKA ILI KUJIHAKIKISHIA HUDUMA WAKATI WOTE KWENYE HALMASHAURI YA NACHINGWEA,MFUKO WA AFYA YA JAMII NDIYO MKOMBOZI WA MWANANCHI KWENYE SEKTA YA AFYA SHIME TUJIUNGE KUZIJENGEA UWEZO HOSPITALI NA ZAHANATI ZILIZOPO KWENYE MAENEO YA VIJIJINI HUSUSAN HALMASHAURI.

Kwanza Tunapenda wasalimu wakubwa wetu Shikamoo na vijana wenzetu Mambo vipi.. Tunatambua kuwa Wanavyuo wenzetu walimu walikuwa hawana kazi kwa muda mrefu Jambo ambalo liliwafanya wengi kuwa na wasi wasi na mwajiri wao. Tunapenda kuwapa tarifa kupitia mtandao wenu wa Matukio na wanavyuo (www.tzwanavyuo.blogspot.com) kuwa, Walimu wahitimu wote Jana usiku majira ya sa saba Nafasi hizo zilitangazwa Rasmi, Pia sisi Tunapenda kuwasilisha majina ya wanafunzi ambao wamechaguliwa Tunaomba mchukue Muda wenu kutazama kwa umakini majina yenu yote yapo hapa. Hongereni sana.
Imeandaliwa na, Matukio na Wanavyuo Crew

No comments:

Post a Comment