TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 21, 2012

UZINDUZI WA ZUKU TV WAFANA DAR-YAFANYA UZINDUZI RASMI

Mkurugenzi wa TCRA,Profesa John Mkoma akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya kuzindua Televisheni ya Zuku Africa kupitia kampuni ya Wananchi Satelite Tanzania inayotoa matangazo yake kwa kutumia ving'amuzi nchini Tanzania , Hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam jana jioni ikihudhuriwa na wadaum mbalimbali na wageni waalikwa. Katika picha kulia ni Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group na kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki wakishuhudia tukio hilo.
Mkurugenzi wa TCRA,Profesa John Mkoma mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kabla ya kuzindua kampuni ya Wananchi Satelite jana katika hafla iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Golden Tulip kulia ni Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group na kulia ni Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki
Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki akizungumza katika uzinduzi huo na kumkaribisha Mkurugenzi wa TCRA Profesa John Mkoma. Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group akimkaribisha Mwenyekitiwa Makampuni ya Wananchi Group Ali Mufuruki.
Kundi la TMK wanaume Family likitumbuiza katika uzinduzi huo jana.
Bendi ya Tanzanite ikiongozwa na mwanamzuiki nguli John Mhina ilitoa burudani ya kutosha katika uzinduzi huo jana.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika uzinduzi huo.
Wadau hawa nao walikuwepo ndani ya nyumba kama unavyowaona wengi wanaipenda ZUKU TV.
Waimbaji wa muziki wa injili pamoja na waigizaji wa filamu hawakukosa uzinduzi huop kutoka kulia ni Mwigizaji Natasha, Monalisa , Mwimbaji Alice na mumewe ambaye pia ni mwimbaji Bw. Robert David wakipozi kwa picha.
Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group katikati na Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki kulia wakimsikiliza Meneja mkuu wa Wananchi Satelite Bw Mohamed Jeneby akiwaelezea jambo.
Richard Bell Afisa Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Wananchi Group kulia i na Mwenyekiti wa makampuni ya Wananchi Group Bw. Ali Mufuruki wakijadili jambo katika uzinduzi huo.
Wadau kutoka ZUKU TV wakipozi kwa picha jana katika uzinduzi huo.
Mwanamuziki AY na wenzake walihudhuria pia uzinduzi huo.
Jaquiline Karanja kulia na Moureen walikuwepo pia hebu wacheki na pozi yao.
Kutoka kulia ni wadau ZIZZOU wa ZIZZOU Fashion, Suzy wa Clouds na mdau Godliver wa Prime Time wakipozi kwa picha.

No comments:

Post a Comment