TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 19, 2012

SIMBA NA YANGA ZAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI YA VODACOM



SIMBA NA YANGA ZAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI YA VODACOM

Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF wakati kampuni ya bia ya TBL ilipokabidhi vifaa vya michezo kwa timu za Simba na Yanga, tayari kwa kuanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza Jumamosi Januari 20 2012.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah, Steven Kilinde Mkurugenzi wa Mahusiano TBL, George Kavishe Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro, Evodius Mtawala Katibu Mkuu wa Simba na Boniface Wambura Msemaji wa TFF wakionyesha vifaa vilivyokabidhiwa ka timu ya Simba.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Kilimanjaro Steven Kilinde akikabidhi jezi kwa Katibu Mkuu wa timu ya Yanga Selestine Mwesigwa katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania leo katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro Bw. George Kavishe na kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Kilimanjaro Steven Kilinde, Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro Bw. George Kavishe, Katibu Mkuu wa timu ya Yanga Selestine Mwesigwa na kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah wakionyesha vifaa vilivyokabidhiwa kwa timu ya Yanga katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania leo.
Viongozi wa Yanga na Simba pamoja na TBL wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa timu ya Simba na Yanga

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Batlda Burian, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kumuaga rasmi kwenda kuanza kazi nchini Kenya baada ya uteuzi wake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Batlda Burian, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kumuaga rasmi kwenda kuanza kazi nchini Kenya baada ya uteuzi wake. 

H-BABA AKAMILISJA SINA RAHA NA BANZA STONE

MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamis Ramadhan ‘H-Baba’ amekamilisha kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Sina Raha, akimshirikisha gwiji wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja, ‘Banza Stone’ Mwalimu wa Walimu.
Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto, H-Baba, alisema kuwa kibao hicho ni miongoni mwa nyimbo zake 10 zitakazokamilisha albam yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Shika hapa acha Hapa’ inayotarajia kuingia sokoni mwezi wa tatu mwaka huu. 
Aidha alisema kuwa wimbo ambao amemshirikisha Banza Stone, amerokodia katika Studio ya Allan Mapigo, ambapo tayari amekamilisha maandalizi ya kurekodi video ya wimbo huo mwishoni mwa wiki hii.
H-Baba alisema kuwa katika wimbo huo mashabiki wake watarajie kupata vitu tofauti ikiwa ni pamoja na staili mpya na midundo iliyo ‘shiba’ na sauti murua ya Banza Stone, aliyeonyesha uwezo wake katika wimbo huo.
Alizitaja studio alizorekodia nyimbo zake zitakazokamilisha albam hiyo kuwa ni pamoja na KGC Studio, Maneke Studio na Allan Mapigo, zote za jijini Dar es Saam.
Pia alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwamo katika albam hiyo kuwa ni pamoja na, Nipe Kidogo, Shika Kichwa, Kinacho Niumiza, Zaidi yako Wewe na Nimpende Nani.

No comments:

Post a Comment