TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, January 20, 2012

WAFANYABIASHA WAONYWA KUACHA KUSAFIRISHA FEDHA BILA YA ULINZI WA POLISI

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar Wafanyabiashara wakiwemo wawekezaji wa kigeni waliopo hapa nchini, wameonywa kuacha mtindo wa kusafirisha fedha nyingi kutoka eneo moja hadi lingine pasipo na ulinzi wa Polisi.
Onyo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Shamsi Vuai Nahodha, wakati akizungumza na wawekezaji wenye Mahoteli katika Fukwe za Bahari ya Hindi na Hifadhi ya Mjini Mkongwe mjini Zanzibar.
Waziri Nahodha amesema kuwa pamoja na kuwapo kwa usalama na amani hapa nchini, lakini hali hiyo isiwafanye watu wakajiamini na kusafirisha fedha nyingi pasipo na ulinzi wa kutosha ili kuepuka kuporwa na majambazi.
Akizungumzia Utalii Mh. Nahodha amesema kuwa kwa kutambua kuwa utalii ndio chanzo kikubwa cha uchumi wa Zanzibar na taifa kwa ujumla, Serikali itahakikisha kuwa inaweka miundombinu ya kutosha kiusalama ili kuondoa matishio yoyote kwa wageni wanaoitembelea nchi yetu kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kitalii.
Aidha amesema ili kuhakikisha usalama zaidi, wawekezaji hao hawanabudi kulitumia Jeshi la Polisi katika kufanya uchunguzi kwa watu wanaotaka kazi kwenye maeneo yao ili kuepuka kuajiri watumishi wasio waaminifu.
“Mnapotaka kuwaajiri wafanyakazi, wakiwemo walinzi kwenye maeneo yenu, hakikisheni kuwa mnaowapa nafasi hizo ni vijana wa maeneo jirani ambao wengi wao wanafahamika kwa sura na tabia kulikoni kutoa watumishi mbali ambao hata kama wakifanya uhalifu na kukimbia ni vigumu kumpata”. Alisema Mh. Nahodha.
Mh. Nahodha ameongeza kuwa athari za kumuajiri mtu wa mbali ni kuwa hata pale atakapofanya uhalifu na kukimbi haitakuwa rahiisi kwa Polisi kumpata mtuhumiwa huyo kwa urahisi.
Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Wawekezaji wa Mahoteli Visiwani Zanzibar (ZATI) Zanzibar Association Tourism Industrial Bw. Abullsamad Saidi, alisema kuwa ipo haja kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusaidia kuongeza kasma ya Jeshi la Polisi Visiwani humo ili waweze kumudu vema kazi zao zikiwemo za ulinzi wa vivutio vya kitelii kwa wageni.
Amesema kuwa pamoja na Jeshi la Polisi kufanya kazi zao vizuri, lakini askari wamekuwa wakipata vikwazo kutokana na uduni na ukosefu wa vitendea kazi kama vile usafiri na radio za mawasiliano.
Hoja hiyo pia imeungwa mkono na Mshauri wa Rais katika Masuala ya Utalii Bw. Issa Ahmed Othman, ambaye amesema kusipokuwa na usalama wa kutosha kwenye maeneo ya fukwe na kuna hatari ya kukosa watalii na hivyo kudhoofisha na kupunguza pato la taifa linalotokana na utalii.
Wakichangia hoja kwenye mkutano huo, baadhi ya wawekezaji waliiomba Serikali kuwa na bajeti ya kutosha katika kulinda maeneo ya vivutio vya kitalii.

Bibi Gonsaga Mwingira Shawa a.k.a Bibi Malaika akiwalisha kieki wajukuu zake katika hafla yake iliyofanyika jijini Dar es Salaam wakati al,ipotimiza miaka 75 ya kuzaliwa kwake
Bibi Gonsaga Mwingira Shawa a.k.a Bibi Malaika akifurahia na kushangiliwa na marafiki, watoto na wajukuu zake kwa kutimiza miaka 75 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Keki ya kumpongeza bibi Malaika kufikisha miaka 75.
Bibi Malaika akisalimia na Balozi mstaafu wa Ufaransa Mhando katika sherehe ya kumpongeza Bibi Malaika kufikisha miaka 75..
Ndugu jamana na marafiki wakimpatia bibi Malaika zawadi.

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) na Chuo cha Polisi cha Kimataifa cha Moshi (CCP) wameingia makubaliano ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo vya vijana. Katika Makubaliano hayo yaliyofikiwa mwezi August, 2011, TPBC na CCP watashirikiana kuchagua vijana wenye vipaji vya mchezo wa ngumi na kuwaendeleza ili waweze kucheza michezo ya majeshi pamoja na mashindano mengine ndani na nje ya Tanzania. Makubaliano haya yamekuja wakati ambapo Tanzania inahitaji msukumo mkubwa kwenye medani ya michezo ili kuweza kufufua ari na moyo wa michezo kama ilivyokuwa katika miaka ya 70 na 80. Aidha, Makubaliano haya yana lengo la kuandaa jeshi zuri la wanamichezo hodari watakaoleta sifa jeshi la Polisi pamoja na Tanzania kwa ujumla. Tayari vijana wengi wanafanya mazoezi katika kambi (Gym) ya ngumi ambayo imewekwa katika viwanja vya michezo vya CCP. Kambi hiyo inawashirikisha pia vijana kutoka maeneo mengine mkoani Kilimanjaro ambao sio Polisi. Katika kusimamia hili, Rais wa TPBC Onesmo Ngowi akishirikiana na Afisa Mipango na Utawala wa CCP Superintendent of Police, Lutusyo Mwakyusa watahakikisha kuwa vifaa muhimu vinapatikana pamoja na mazingira ya kufanyika mazoezi na upatikanaji wa wataalam wanaotakiwa wanapatikana. Naye Superintendent of Police, Yahya Mdogo ambaye ni Afisa wa Michezo katika Chuo cha Polisi cha Kimataifa Moshi ataangalia kwa karibu mwenendo mzima wa mahitaji ya kila siku ya mazoezi. Tayari TPBC imeshatoa vifaa muhimu vya mazoezi pamoja na wataalam (Makocha) wa kuwafundisha mabondia hao wako katika sehemu ya mazoezi. Vijana wengi ambao walikuwa hawana kazi au mahala pa kwenda wakati wa saa za jioni kwa sasa wanafanya mazoezi na wenzao katika uwanja wa CCP. Aidha, baadhi ya mabondia kutoka katika mkoa wa Kilimanjaro ambao walikuwa wameweka kambi katika jiji la Nairobi nchini Kenya na Arusha wamejumuika katika kambi hii mpya. Mabondia hao ni pamoja na Pascal Bruno anayejulikana na wengi kama "Price Kilimanjaro", Emilio Norfat, Charles Damas, Alibaba Ramadhani, Robert Mrosso, Bernard Simon na wengine wengi Baadhi ya wataalam waliojitokeza kuwafundisha vijana hawa ni pamoja na Felix Joseph na Pius Msele ambao kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa wachezaji na makocha wa timu ya ngumi ya taifa. Makubaliano haya ni baadhi tu ya mikakati mipya za TPBC za kuamsha ari ya mchezo wa ngumi kwa kuzisambaza mikoani kuliko ilivyozoeleka ngumi kufanyika katika mkoa wa Dar -Es-Salaam peke yake. "Kwa sasa kazi kubwa tulivyo nayo ni kuzipeleka ngumi mikoani ambako tunaamini kuna vijana wengi sana wenye moyo pamoja na vipaji vikubwa" alisema Ngowi.

No comments:

Post a Comment