TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 16, 2012

Mwanafunzi ajiua Arusha kwa kosa la kusingiziwa kuiba dola 1500



Na Mwandishi Wetu- Arusha Mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la John Justine(17) mkazi wa makao mapya amefariki dunia jana katika hospitali ya mount meru wakati akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwa risasi. Akizungumza na wandishi wa habari kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa arusha Thobias Andeng'enye amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja na nusu jioni ambapo siku hiyo mama wa marehemu aitwaye Betty John alikuwa akitoka kwenye sherehe mara baada ya kufika nyumbani alikuta geti limefungwa ndipo alipowaomba majirani kumsaidia kufungua. Andeng'enye amesema kuwa mama huyo amesema kuwa mara baada ya kuingia ndani akiwa na mtoto wa jirani alimkuta mtoto wake akiwa chini amelala chini huku akihema kwa tabu huku damu zikimtoka kifuani ndipo alipotoka nje na kuomba msaada kwa majirani. Aidha kamanda alisema kuwa mma huyo pamoja na majirani walisaidina kumkimbiza hospitali ya Dkt.Mohamed iliyopo eneo la Tank la maji Ilboru kwa matibabu ambapo ilishindikana na kumpeleka hospitali ya mkoa ya mount meru ambapo ailipatiwa msaada lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia. Hata hivyo andeng'enye amesema kuwa baada ya polisi kituo kikuu wilaya kupata taarifa walikwenda eneo la tukio kufanya ukakuzi ambapo walikuta bunduki aina ya shortgun Pump Action pamija na ujumbe unaosema"ANASIKITIKA KULAUMIWA NA WAZAZI WAKE PIA ANAWAPENDA SANA" Vilevile walikuta michirizi ya damu kutoka chumbani hadi alipoangukia. Kamanda ameongeza kuwa inasemekana kuwa marehemu alituhumiwa na baba yake mzazi Jastine Kaizer kuwa aliiba fedha kiasi cha dola za marekani 1500 hivyo polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa kumhoji baba mzazi wa marehemu . Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha mount meru ukisubiri uchunguzi zaidi wa daktari.

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MKUU wa mkoa wa Dares Salaam Said Mecky Sadick amesema bado misaada zaidi inahitajika ili kuweza kuwasaidia wahanga wa mafuriko hususan ya shughuli za ujenzi na mahitaji ya watoto walioanza shule.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Sadick wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake jijini Dares Salaam mara baada ya kupokea msaada wa hundi ya sh. milioni tano kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, ambayo ilikadhiwa kwake na Mkurugenzi Mkuu Fadhili Manongi.
“Bado misaada inahitajika tunaendelea kutoa wito kwa watu walioguswa kuweza kutoa michango yao ili kuweza kusaidia shughuli za ujenzi na mahitaji ya wanafunzi walianza shule mfano madaftari, vitabu na huduma zingine zinazohusiana na elimu,” alisema.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine iliyopo ni kujenga nyumba za walimu na kliniki ya wakinamama na watoto,hivyo aliwaomba Watanzania, taasisi, mashirika na watu binafsi walioguswa kuendelea kuchangia.
Wakati huohuo, Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina Tanzania (CBCT),kilikabidhi hundi kivuli yenye thamani sh. milioni 10 ya michango ya vitu mbalimbali kwa ajili ya wahanga hao kwa Mkuu huyo, ambayo ilikabidhiwa katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina kwa Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal juzi usiku.
Hundi hiyo ilikabidhiwa kwa Sadick na Mwenyekiti wa CBRT Zhu Jinfeng, ambapo alisema misaada mingine imendelea kutolewa hivyo michango hiyo hadi leo(jana) imefikia sh. milioni 12,550,000.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa alisema agizo la kuangalia uwezekano wa kuwapatia viwanja wapangaji liko palepale na watalitekeleza kama alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete, hivyo utaratibu utaanza mara baada kukamilisha zoezi la wamiliki.
Aliongeza kuwa utaratibu huo wa wapangaji pia unahitaji fedha kwa ajili ya kufanya tathimni mpya utoaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha maeneo hayo.

Mkuu wa Mkoa wa DSM Sadick Mecky Sadick (kulia) akipokea leo rasmi msaada kupitia kivuli kinachoonyesha vitu mbalimbali na thamani kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara wa kichina Tanzania ZHU JINFENG (katikati) kwaajili ya waathirika wa mafuriko jijini , Msaada huo umekabidhiwa jana kwa Makamu wa Rais Dkt, Gharib Bilal wakati wa sherehe za maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina wenye thamani ya shilingi milioni10. Pamoja na kukabidhi jan 15,2012 lakini leo wamewasilisha rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa DSM Meck Sadick jumla ya milioni 12.5 baada ya kuendelea kuchangia vitu vyengine vikiwemo mabati na saruji, (kushoto) Ni Mmoja wa ofisa kutoka chama cha wafanyabiashara wa kichina nchini Janson Huang . Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Mkuu wa Mkoa wa DSM Said Mecky Sadick (kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Fadhili Manongi (kushoto) leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM kwaajili ya waathirika wa mafuriko wa mkoa wa Da r es Salaam (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO),
Mkuu wa Mkoa DSM (kulia) Sadick Mecky (katikati) Ofisa kutoka chama cha wafanyabiashara wa kichina nchini Janson Huang pamoja na Katibu tawala wa Mkoa wa DSM Theresia Mmbando (kushoto) wakijadiliana leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM baada ya kukabidhi rasmi msaada huo wa kivuli cha mchango wenyethamani ya shilingi milioni 10 ambapo michango hiyo imeongezeka hadi kufikia 12.5/- (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Baadhi ya makocha mbalimbali kutoka mikoa ya Tanzania Bara wakiwa katika kozi hiyo iliyoanza kibaha leo ikitolewa na mkufunzi wa makocha wa Masumbwi wa kimataifa Josef Diouf kutoka Shirikisho la Dunia la mchezo wa ngumi (AIBA) Picha na www.superdboxingcoa
Kocha wa Mchezo wa Ngumi Rajabu (Super D) kulia akibadilishana mawazo na mkufunzi wa makocha wa Masumbwi wa kimataifa Josef Diouf kutoka Shirikisho la Dunia la mchezo wa ngumi (AIBA) katikati ni Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu, Mstaafu, Cleopa David Msuya kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 16, 2011. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri Mkuu, Mstaafu, Cleopa David Msuya, Ofisini kwake jijini Dar es salaam, Januari 16,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT), kimeipa Serikali saa 72, kuwarejesha Hospitali ya Taifa Muhimbili, Wanafunzi waliofuzu udaktari waliondolewa hapo baada ya kugoma wakidai malipo yao. Tamko hilo lilitolewa na Rais wa chama hicho, Dk Namala Mkopi katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana. Chama hicho kimemuomba Rais Jakaya Kikwete, kuwatafutia kazi nyingine, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa kwa kosa la kumshauri vibaya Waziri wa wizara hiyo, Dk. Hadji Mponda. Alisema Dk. Mponda anasamehewa kwani hajui alitendalo ila inatakiwa awaombe radhi kwa kuwaita madaktari wenzao kuwa si madaktari bali bado wangali wanafunzi. Rais wa MAT, Dk. Mkopi, pia alitangaza kuwa kimefutia uanachama kwa mwaka mmoja, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mtasiwa kwa kosa lake la kuusaliti udaktari kutokana na kukiuka kiapo cha udakatari kinachosema kuwa Madaktari wote ni ndugu na nitawatendea haki kama dada na kaka. Alisema endapo Dk. Mtasiwa atanendelea na tabia hiyo ya kudharau taaluma ya udakatari, basi chama kitaamua kumfukuza kabisa na kumuweka kwenye mtandao wa madaktari duniani, ili iwe fundisho kwa madaktari wengine wenye tabia hiyo. Dk. Mkopi alisema kuwa chama kimesikitishwa sana na kwamba hawaoni ni kwa nini Serikali imeamua kuwaadhibu madaktari wenzao waliokuwa wakidai haki ya msingi, na kuwaacha kuwaadhibu watu waliosababisha ucheleweshaji wa makusudi wa kutowalipa malipo yao madaktari.

China nvjini Tanzania, Liu Xinsheng, wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jinni Dar es Salaam jana jioni Januari 15, katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, sherehe zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT).
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza na Balozi wa China nvjini Tanzania, Liu Xinsheng, wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jinni Dar es Salaam jana jioni Januari 15, katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, sherehe zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT), zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana jioni Januari 15. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Liu Xinsheng.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 16, kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na City Bank Tanzania LTD kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana Januari 15.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 10, kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana Januari 15.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wasanii wa Kichina waliokuwa wakitoa burudani jukwaani wakati wa sherehe hizo, wakati akijiandaa kuondoka katika Viwanja hivyo.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) leo wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kuwa tunza wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri kupitia kazi zao za Muziki kwa mwaka wa 2012.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam meneja wa bia ya Kilimanjaro bwana George Kavishe alisema Mwaka jana Tunzo hizi za Muziki nchini Tanzania zilifanyiwa mabadiliko makubwa ambayo kwa mwaka huu yataendelezwa na kuboreshwa zaidi. Ambapo Mchakato wa kuwapata vinara hao utapitia hatua kuu zifuatazo:
1. ACADEMY:
ACADEMY ya Tunzo za Muziki Tanzania ni mkusanyiko wa wadau wa muziki kati ya hamsini hadi mia moja( 50 mpaka 100)kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambao huwekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua na hatimae kupata wateule (Nominees) wa kinyang’anyiro hicho baada ya majaji kujiridhisha kuwa washiriki waliopendekezwa wamekizi vigezo vyote muhimu ambapo zoezi hili kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika tarehe 27 na 28 Jan 2012.
2. Majaji:
Hatua ya pili ni Majaji ambapo huwa ni hatua muhimu sana ambapo majaji huwa na kazi moja kubwa ya kupiga kura wakizingatia vigezo muhimu vya kiufundi zaidi na vile vile kuhakiki uteuzi wa washiriki uliofanywa katika hatua ya awali kwenye Academy husika ikiwa ni pamoja na kura zitakazopigwa na wananchi. Wao hutumia zaidi vigezo halali vinavyopatikana na mkusanyiko wa rekodi za wasanii zilizotoka kwa mwaka 2011, kazi zao za mwaka 2011, Mafanikio n.k. Jopo hili hujumuisha wadau wa tasnia ya musiki kumi na tano (15).
3. KURA:
Hii ni ni hatua ya mwisho ambapo wapenzi wa musiki waliopiga kura zao Kura hizo hujumuishwa katika kuchangua washindi ambapo kwa shindano la mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitabeba asilimia sabini (70%) na kura za majaji asilimia thelasini (30%.) na katika kufanikisha upigaji kura kutakuwa njia kuu Njia kuu nne za upigaji wa kura :
  • Njia ya ujumbe mfupi (sms).
  • Njia ya barua pepe (Email).
  • Njia ya kujaza sehemu maalum katika Magazeti.
  • Na njia ya mwisho ni njia ya vipeperushi (Fliers.)
Kwa upande wake mwakilishi wa baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Mzee Luhaja amewataka wasanii wa tasnia hiyo nchini kutumia vyema fursa ya tunzo za Kili Music Award kama sehemu ya kuweza kujitangaza katika anga za muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
Alisema msanii mzuri ni Yule anaeweza kutunga nyimbo zenye lengo la kuelimisha jamii na kuburudisha kwa kuzingatia maadili na hayo hujidhihirisha kupitia kwenye tunzo kama hizi ambazo hutoa fursa kwa wasikilizaji kutoa michango yao juu ya mwanamuziki gani aliyeweza kukonga mioyo yao kupitia tungo zake.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kuhusu maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM ambayo yataanza mwanzoni mwa mwezi Februari na kufikia kilele chake Februari 5, 2012. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema maadhimisho ya kuzaliwa kwake ya mwaka huu pamoja na mambo mengine kitayatumia kupiga vita wagombea wote wanaotoa na kupokea rushwa wakati wake mkuu. Pia kitatumia maadhimisho hayo kuhamasisha wananchama wake waadilifu na waaminifu kujitokeza kugombea katika uchaguzi huo utakaofanyika mwaka huu, kuanzia ngazi za mashina hadi taifa. Hayo yalisemwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam. Nape alisema, Chama kitatumia fursa hiyo pia kuwaelimisha wanachama wake na wananchi kwa jumla kuhusu mabadiliko ya Katiba ya nchi yanayokusudiwa kufanyika, ikiwa ni pamoja na msimamo wa kuilinda nchi, amani, na kupatikana kwa Katiba bora itakayokuwa na manufaa kwa watu wote. Alisema, maadhimisho hayo yataanza Februari mosi na kufikia kilele chake Februari 5, 2012 yakiambatana na shughuli mbalimbali yakiwemo matembezi ya mshikamano yatakayofanyika kila mkoa wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo kitakachofanyika Mwanza. Nape alisema . "Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Mapinduzi kufikisha miaka 35 ya uhai wake yangu vyama vya TANU na ASP vilipovunjwa na kuundwa chama kipya cha CCM chenye nguvu, Februari 5, 1977",lisema Nape na kuongeza. "Sherehe hizo huadhimishwa kwa Chama na Jumuia zake kufanya shughuli mbalimbali za kisiasa na kijamii. Aidha, Kitaifa Chama huteua mkoa mwenyeji wa sherehe hizi ambazo huambatana na matembezi ya mshikamano". Alisema kwa kuwa mwaka huu ni wa Uchaguzi Mkuu wa Chama kimependekeza kaulimbiu mahsusi itakayotumika katika sherehe hizo kuwa ni "CCM Imara na Madhubuti inaanza na mimi; naimarisha Chama Changu kwa kuchagua viongozi bora na waadilifu". Nape alisema uzinduzi wa sherehe hizo utafanyika kila mkoa Januari 30, mwaka huu na kufuatiwa na wiki ya shughuli za Jumuia, ambazo kila Jumuia itapanga ratiba ya mikutano ya ndani na shughuli za kijamii kama kupanda miti. CCM imewataka wajumbe wa Kamati ya Siasa na Halmashauri Kuu ya mikoa kutumia wiki hiyo kufanya ziara katika matawi kuimarisha uhai wa Chama

By A Correspondent EXIM Bank (Tanzania) Limited has introduced yet another innovative deposit product aimed at encouraging regular savings among low income earners and salaried employees and Corporates, known as "Haba na Haba Account" The bank said in a statement issued in Dar es Salaam yesterday that the product was a New Year gift to its clients, who are ready to demystify financial planning and become good savers. "You only need to drop just a bit of your earnings in your Haba na Haba Account after authorising Exim Bank to set aside a small portion of your savings or salary regularly or every month, for a fixed period ranging from 12 to 120 months. "Put your money to work. You will be surprised how money grows on the Exim tree!" the bank said in the statement.
The depositor gets Tsh 100 mio with a monthly investment of Tsh.515,000/-only for a period of 10 years, as per the prevailing rates.
It noted that in today’s hard pressed times and fluctuating world economies, more and more families are finding themselves cash-strapped. The key word today is security and the only goal is resource augmentation.
The bank further said the minimum amount to be deposited could be as low as 20,000/- per month, but there is no upper limit.
"The scheme is open for new, existing and corporate clients by just authorising the bank to set aside every month the desired amount from the savings account into Haba na Haba Account," it adds.
Exim Bank is Tanzania’s sixth largest bank in terms of total assets, deposits and finances and has a network of 22 branches and 48 Automated Teller Machines (ATM) across the country.
It is the only locally bank which has dared to spread wings outside Tanzania, with opening of subsidiaries in Djibouti and Comoros Island. It has a single branch in Djibouti and two branches in the Indian Ocean Island.
The bank recently acquired a new core banking solution from M/S Polaris Software Labs Limited ,one of the leading IT enabled banking solution provider in the world market that has helped the bank provide services more convenient and effectively.

Mkuu wa kitengo cha mauzo ya Vodacom m-pesa Franklin Bagala,akiongea na Mawakala wa m-pesa wa Mkoa wa Dares Salaam katika semina iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania,mahususi kwa mawakala hao kujifunza namna ya kutoa huduma zilizo bora za m-pesa kwa wateja wao,Semina hiyo ilifanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Karimjee jijini.
Mmoja wa mawakala wa mkoa wa Dares Salaam akiinua mkono kuuliza swala katika semina ya mawakala wa m-pesa wa mkoa wa Dares Salaam iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania,mahususi kwa mawakala hao kwa ajili ya kutoa huduma bora za m-pesa kwa wateja wao,Semina hiyo ilifanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Karimjee jijini.
Baadhi ya Mawakala wa m-pesa wa Mkoa wa Dares Salaam waliohudhuria katika semina iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania,mahususi kwa mawakala hao kujifunza namna ya kutoa huduma bora za m-pesa kwa wateja wao,Semina hiyo ilifanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Karimjee jijini Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imefanya maboresho makubwa katika mfumo unaondesha huduma ya Vodacom m-pesa kwa lengo la kuendana na kasi ya ukuaji na mahitaji ya huduma hiyo katika soko nchini.
Maboresho hayo sasa yanawawezesha wateja wa Vodacom m-pesa kufanya miamala yao kwa ubora na kasi ya hali ya juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza amesema maboresho hayo makubwa yamefanyika Disemba mwaka jana ili kuuongeza nguvu na ufanisi mfumo wa mawasiliano unaotumika kutoa huduma za Vodacom m-pesa.
“Tumefanya maboresho kama ilivyodesturi yetu ya kuboresha na kuimarisha huduma zetu mara kwa mara. Tunatambua kwamba wateja wa Vodacom m-pesa walikuwa wanakabiliwa na changamoto za hapa na pale ninayo furaha kubwa kuona kwamba tunaendelea kuiboresha huduma hii”Alisema Bw. Meza
Bw. Meza amesema katika kipindi chote cha mwishoni mwa mwaka huduma ya m-pesa imepatikana kwa kasi na ubora zaidi na hivyo huduma ya m-pesa kuendelea kuwa kiungo muhimu katika kubadili maisha ya wananchi kupitia teknolojia ya simu ya mkononi.
“Wakati wote tunaishi na dhamira yetu ya kutoa huduma bora na kujali mahitaji ya wateja wetu tutaendelea kufanya hivyo mara kwa mara sambamba na kutoa kipaumbele cha kuhakikisha usalama huku tukiongeza pia kasi ya ubunifu na uvumbuzi wa huduma bora”. Alisema Bw. Meza
“Huduma ya Vodacom m-pesa imekuwa kiungo muhimu cha maisha ya wananchi mijini na vijijini imezalisha ajira, imerahisisha maisha na biashara ni kiasi cha kupiga *150#00 kutoka mtandao wa Vodacom na kuanzia hapo kiganja cha mkono kinakusogeza karibu na ndugu jamaa na watoa huduma mbalimbali.” Bw.Meza aliongeza.
Huduma ya Vodacom m-pesa imeanzishwa Aprili 2007 na tangu wakati huo ukuaji wake sokoni umekuwa ni wa kasi kufikia wateja milioni tisa kutokana na kutoa urahisi wa malipo na ununuzi wa huduma mbalimbali ikiwemo Maji,Umeme, muda wa maongezi, Dstv, manunuzi ya tiketi za safari za ndege, utumaji na upokeaji wa fedha kwa usalama,uhakika na kuaminika wakati wote ukiwa na mtandao wa wakala zaidi ya elfu ishirini nchi nzima.

No comments:

Post a Comment