TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, January 20, 2012

MKUTANO WA WAZIRI WA HABARI NA KAMATI YA BUNGE

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ,Dk.Emmanuel Nchimbi(katikati) akifafanua jambo kuhusu mkataba wa Vijana wa Afrika kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kwenye ukumbi wa mkutano wa Wiizara ya Maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto leo . Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sihaba Nkinga na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Juma Nkamia.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Vijana, James Kajugusi akifafanua jambo leo kuhusu mkataba wa Vijana wa Afrika kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kwenye ukumbi wa mkutano wa Wiizara ya Maendeleo ya Jamii . Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sihaba Nkinga na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ,Dk.Emmanuel Nchimbi(katikati) akiwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kwenye ukumbi wa mkutano wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, wakati wa kujadili mkataba wa Vijana wa Afrika leo .PICHA NA MAGRETH KINABO - MAELEZO

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Burilo Busagi, katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza. Jumla ya wahitimu 374 wa kidato hicho walipewa vyeti. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeyo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Tifugundulwa Tumbika katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza. Tumbika alikabidhiwa cheti hicho kwa kuibuka mwanafunzi bora katika kuzungumza Kiingereza. Wapili kulia ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na mwanafunzi aliyesoma shule ya sekondari ya Nsumba, Mwanza, kati ya mwaka 1954 na 1957 (darasa la nane na kumi) Damas Ngoma, wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo leo. Nape ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo alisoma pia katika shule hiyo hadi kidato cha nne mwaka ambako alimaliza mwaka 97. Watatu ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.(Picha zote na Bashir Nkoromo).

Na Zahira Bilal Maelezo Zanzibar
Waziri wa kazi uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika Haroun Ali Suleiman amesema kuwa idadi ya vyama vya ushirika vinavyoaandikishwa imekuwa ikiongezeka na kwamba vyama hivyo vimekuwa vikiongezewa nguvu ya usimamizi na utaalamu.
Hayo aliyasema leo wakati akijibu swala la Mwakilishi wa nafasi za wanawake Salma Mussa Bilali alietaka kujua hatua zinazochukuliwa na wizara katika kuimarisha vyama vya ushirika wilayani huko katika ukumbi wa baraza la wakilishi chukwani
Waziri Haroun alisema kuwa zoezi la kukusanya takwimu za vyama litakapokamilika litasaidia kujua mahitaji ya wataalamu na watendaji kwa ujumla
Aidha alisema wizara yake inajitahidi kujipanga ili kuweza kuimarisha utendaji wilayani na katika vitengo maalumu vya idara ya ushirika pia kusimamia mpango wa mafunzo kwa maofisa wa ushirika wa ngazi mbali mbali ili kuongeza utaalamu na uwezo wao wa kuhudumia vyama vya ushirika kwa ufanisi zaidi
Alisema wizara yake inampango wa kuanzisha vituo vya stadi maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kwa washirika na kuweza kuimarisha vyama vya ushirika kwa kila wilaya
Alisema kufanya hivyo inaweza kuondoa usumbufu wa tatizo la ucheleweshaji wa usajili wa vyama vya ushirika na kuongeza kasi ya kukagua na kupewa usajili kwa haraka
Sambamba na hayo alisema kufanya hivyo ni kuwawasaidia wananchi wa mijini na vijijini kupata ajira na kuwaondoshea umasikini na ndio malengo ya wizara hiyo

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na mabalozi wapya walioteluliwa na kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete hivi Karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwak jijini Dar es salaam Januari 202012. Kushoto kwake ni Dkt. Batilda Burian-Kenya na Ali Saleh-Oman. Kulia kwake ni Philip Marmo-China, Dkt. Ladislaus Komba- Uganda, Shamim Nyanduga- Msumbiji na Grace Mujuma- Zambia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wapya walioteuliwa na kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni baada ya kuzungumza nao, ofisini kwake jijini Dar es salam Januari 20, 2012. Kutoka kulia ni Dkt. Batild Burian- Kenya, Philip Marmo- China, Shamim Nyanduga- Msumbiji, Dkt. Ladislaus Komba - Uganda, Mohamed Hamza - Misri, Grace Mujuma, Zambia na Ali Saleh - Oman. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Father Alphonse M.Sammot wa kanisa katoliki nchini Malta akitoa mada yake juu ya mambo muhimu ya historia ya Kikristo yaliyoko nchini Uturuki ambapo amewasihi watanzania Wakristo kutembelea nchini Uturuki na kuijua historia hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya ibada maalum huko, Father Alphonse M.Sammot amehudumu muda mrefu huko Uturuki amezungumza hayo katika warsha iliyokutanisha wadau na mawakala wa tiketi za ndege pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo, Warsha hiyo imefanyika kwenye Hoteli ya Hyyat Regency Dar es salaam ya jijini Dar es salaam na imeandaliwa na shirika la ndege la Turkish Airlines la Uturuki.
Bw. Emim Cakmak Mwenyekiti wa Baraza la Maendeleo ya Utalii na afya Uturuki (Turkish Hearth care and Tourism Development)akizungumza katika warsha ya siku moja iliyokutanisha makampuni ya mawakala wa kuuza tiketi za ndege na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo, Warsha hiyo ilikuwa ikizungumzia maeneo mbalimbali yenye historia ya Ukristo ambayo wakristo wanaweza kutembelea na kujionea kumbukumbu hizo na imefanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jijini Dar es salaam
Mustafa Ozkahraman Meneja wa Turkish Airline Tanzania akitoa mada katika warsha hiyo juu ya mambo mbalimbali na ubora wa huduma za usafiri wa anga wa shirika hilo, kushoto ni Bw. Emim Cakmak Mwenyekiti wa Baraza la Maendeleo ya Utalii na afya Uturuki (Turkish Hearth care and Tourism Development).
Wadau mbalimbali wakiwa katika warsha hiyo kwenye hoteli ya Hyyat Regency Dar es salaam leo.
Baadhi ya masista pia wamehudhuria katika warsha hiyo iliyoandaliwa na shirika la ndege la Turkish Airlines.
Kutoka kushoto ni )Bw. Emim Cakmak Mwenyekiti wa Baraza la Maendeleo ya Utalii na afya Uturuki(Turkish Hearth care and Tourism Development), Mustafa Ozkahraman Meneja wa Turkishh Airline Tanzania na Victoria Carmak Meneja Huduma wa Hello Tourism Travel Agency wakiwa katika picha ya pamoja leo.
Baadhi ya viongozi wa dini madhehebu ya Kikristo wakiwa katika warsha hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam leo.
Kulia ni Warda Saad wa shirika la ndege la Turkish Airlines na kushoto ni Bahati Chando kutoka kampuni ya R$R ya jijini Dar es salaam wakiwa katika warsha hiyo.

No comments:

Post a Comment