TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 21, 2012

MWIZI AGEUKA NINJA KARIAKOO, ARUKA MAGOROFA NA KUWAACHA WANANCHI WALIOKUWA NA ASIRA KALI ZA KUUA.


 Jamaa huyo baada ya kula kichapo, aliingia humu ndani wanapochezea michezo ya Bahati na Sibu
 Wananchi waliendelea kujazana na kudai wanahitaji roho yake
 Baada ya ukosefu wa Amani eneo hilo, na Ibilisi kuzingira, ghafla alitokea Askari, na kuanza kuwatuliza wananchi waliokuwa hawashikiki, tulieni basi nimpeleke Polisi "alisema Askari
 Raia wengine walinyoosha mikono juu kulalamika, "we askari vipi toka tuachie huyo bhana, roho yake tunywe Damu, la sivyo na wewe tutakudungua mawe"walisema wananchi
 Afande naye" Mimi ni Askari sawa eh, kazi yenu imeisha umebaki wakati wangu, huyu anakwenda kunyea Debe, saawa jamani, Amri ni moja sasa natoka naye"alisema Afande
 Naingia Ndani kumtoa, ila msimguse tena,
 Afande, Wataniua hao Mzee, nikitoka humu ndani, si unaona walivyokasirika, na wewe upo pekee sasa utanisaidiaje, au ndo unataka kunitoa kafara, najuta kuiba hii Simu, Nikipona Leo Siibi tena, EH-Mungu Nisaidie, nimekosa kwako na Kwa Raia Pia, YESUUUUUU Niokoe
 We, Pumbavu zako, Yesu ndiyo kakutuma kuiba Simu ya Watu, sasa leo utaona , lazima tunywe Damu yako na Huyu afande hatokusaidia hapa, hata uniangalie roho hiyo tunaitoa sawa, hakuna huruma Tena,
 Kizaa zaa kilianza baada ya Afande kutoka naye nje, Raia tuachie huyooooooooo tumsulubu, Polisi -Hapana jamani mwacheni tumpeleke akatumikie Serikali, Raia Serikali ya nini huyo Izraeli anamuitaji, Mbona wetu huyo, Kelele za Mabishano zilipozidi, Afande alijinasua na kumwacha
 Haya sasa tunakupeleka Kukutoa Roho, Twende Mwizi wewe,"Jamani nioneeni huruma, basi, Duh, nikiponyoka Mikononi mwao hapa ni mbio na wataona wenyewe mchezo, ngoja niwalie taiming
 Gafla alidandia gari lililokuwa mwendo kasi kidogo, Dereva aliamuli kusiamama hadi alipotelemshwa kwa virungu, matofari, mawe, hadi gari hilo kuvunjwa Vioo, Telemka wewe hapa kipigo tu
 Raia waliendelea kukamua kisawasawa, kipigo kilizidi, Damu ilizidi kumwagika, na hapo ndipo walipobugi, baada ya kupata Upenyo tu, alinyoropoka na kuingia kwenye Majengo ya Serikali(NHC) yanayokaliwa na Wahindi, na kupanda Juu kabisa ya Gorofa tano, mchezo uliofuata mazee
 Hawa watu hawajui kwamba mimi na Osama Bin Laden Tulisoma Shule Moja nini, nilikuwa nawapigia Heaabu tu, na hapa wamekosea tayari Siku ingine wanitafute siyo leo tena, kama wanaweza kufuata jeshi la Mtu Mmoja kazi kwao, Jamaa aliomndoka kwa mfumo huo na kuwashinda watu wote Kariakoo leo. gorofa kwenda gorofa na zaidi ya gorofa tano karuka kama ninja

Wananchi waliokuwa na Asira kali walibaki kumtafuta bila mafanikio,(Duh huyu jamaa ni kiboko, katuacha hivoi hivi, hapana siamini , ila lazima tumkamate" alisema jamaa hapo juu aliyesimama lakini  hadi mwisho wa mchezo kama za OSAMA, NA MULLA OMARY(Picha Zote na Shaaban Mpalule).

No comments:

Post a Comment