TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, April 29, 2013

TAASISI YA HASSAN MAJAAJAR TRUST NA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LATOA WATOA MSAADA WA MADAWATI SINGIDA

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Misuna P4270212Baadhi ya madawati yaliyotolewa
Zaidi ya wanafunzi 750 katika shule saba za wilaya ya Singida zitapokea msaada wa madawati yaliyotolewa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust na Shirika La Nyumba La Taifa 
Jumla ya madawati 264 yanatolewa na wabia hao kupunguza tatizo sugu la upungu wa madawati katika shule hizo. Hafla ya kukakabidhi madawati hao, imefanyika katika Shule ya Msingi ya Munisa, iliyoko Halmashauri ya Singida. 
Bwana Shariff Maajar, kwa niaba ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust akishirikiana na Bwana Nehemiah Mchechu kwa niaba ya Shirika La Nyumba La Taifa, walikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Parseko V Kone.
“Napenda kutoa shukurani za dhati kwa Wakfu wa Hassan Maajar na Shirika La Nyumba La Taifa kwa msaada hu mkubwa utakaochangia kuboresha elimu Singida’, alisema Dr. Kone. 
Wanafunzi mkoani Singida, hususan, walioko vijijini wanakabiliwa na changamoto kubwa la kwanza likuwa mazingira ya kusomea, hivyo tunafarijika kuona wabia wanotusaidia kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto wetu. Hii inakuza viwango na kuhimiza matokeo bora”, aliongeza.
Chini wa mradi wa Hassan Maajar Trust wa “Dawati Kwa Kila Mtoto”, (A Desk For Every Child) mkoa wa Singida wa pili kati ya mitano itakayonufaika kwa msaada inyaotelewa na Hassan Maajar Trust kwa kutumia fedha zilizopatikana na michango iliyotolewa kufwatia kampeni iliyoanzishwa Desemba 2011. Garama za madawati haya ni Tsh 22,500,000, kati ya hizo Shirika La Nyumba La Taifa limetoa jumla ya Tsh 10,000,000.
“Tunataka kuhakikisha kuwa kampeni ya Dawati Kwa Kila Mtoto inawafikia watoto wengi iwezekenavyo na kujenga maisha bora kwa watoto hao”, alisema Zena Tenga, Mkurugenzi Mtendaji. “Tunashukuru Shirika La Nyumba La Taifa kwa kuunga mkono juhudi zetu. Tutaendelea kuhamasisha ushirikiano na wote wenye nia ya kuona lengo la Hassan Maajar Trust la kuhakikisha watoto wetu wakiondoka sakafuni na kukaa kwenye madawati lina timia”,aliongeza.
 “Tunafurahi kuona kwamba mchango wa shirika letu sasa uko katika hali ya madawati ambapo watoto watakaa na watafurahia masomo ‘, alisema Bw. Mchechu, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La Nyumba La Taifa.   , “ Shirika la Nyumba La Taifa lilishirikiana vema na Taasisi ya Hassan Maajar Trust kuchangia fursa hii adimu kwa wanafunzi na maendeleo ya elimu kwa ujumla”, aliongeza.

No comments:

Post a Comment