TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, May 1, 2013

MPANDA MKOANI KATAVI AMEZALIWA MTOTO MWENYE VIUNGO VYA AJABU


MASAI
Na Kibada Kibada-Mpanda Katavi
Katika hali isiyo ya kawaida  mwanamke aitwaye Johari Raphael ( 35)  mkazi wa  mtaa wa Makanyagio  Halmashauri ya Mji wa Mpanda  Mkoa wa Katavi  amejifungua  mtoto wa kiume  mwenye viungo  vya ajabu    utofauti na banadamu wa kawaida.  
Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya  ya Mpanda Naibu  Mkongwa   aliwaambia waandishi wa Habari Ofisini kwake jana kuwa  mwanamke huyo  alijifungua  mtoto  wa ajabu ambae  alikuwa na kichwa kikubwa  kama cha mtu mwenye umri mkubwa  huku  mikono na miguu yake  ikiwa mifupi mfano wa  pingili  za miwa.
Dkt Mkongwa alieleza kuwa  mwanamke huyo alijifungua mtoto  mwenye  uzito wa  kilo  nne na  nusu(4.5)  hata hivyo  alifariki dunia  muda mfupi  baada ya mama yake kujifungua kwa njia ya upasuaji  baada ya kushindwa  kujifungua kwa njia ya kawaida  katika hospitali hiyo.
Madaktari waliamua kumfanyia  upasuaji  baada ya kupata maelezo kutoka kwa mama huyo alipoeleza kuwa  huo ulikuwa ni  uzao wake wa  tano   na  kati ya  zao hizo amekuwamara hizo   akijifungua kwa  shida  hali iliyo pelekea  kujifungua watoto  wawili wakiwa wameisha kufa.
Dkt Mkongwa akifafanua  zaidi alieleza kuwa baada ya kupata historia  ya mama huyo  waliamua kumfanyi a uchunguzi na walipobaini kuwa  mama huyo hawezi kijifungua kwa njia ya kawaida kutokana  na ukubwa wa kichwa  alicho kuwa nacho  mtoto  ambacho mwanamke  yoyo hawezi kujifunga kwa  njia ya kawaida
Alisema  kutokana na hari hiyo  madakitari wa waliamua kumfanyia upasuaji  na ndipo mtoto huyo wa kiume alipotolewa  na alifariki muda mfupi  baada ya kuzaliwa
Kwa upande wake muuguzi mkuu wa hospital hiyo ya wilaya ya Mpanda Elexzanda Kasagula  alisema kuwa mwanamke huyo alifikishwa katika  hospital hiyo hapo juzi na kulazwa katika wodi ya wazazi baada ya kuonekana muda wake  wa   kujifungua umefika
Alieleza  hari ya Johari   ambae amelazwa katika wodi ya wazazi inaendelea  vizuri  na wanasubiriwa ndugu  zake   ili  wakabidhiwe  mwili  wamarehemu kichanga hicho kwa ajiri ya  mazishi
Kasagula  alisema  hili  ni tukio la pili ndani ya kipindi cha miezi mitatu  kwa kuzaliwa watoto wa ajabu  kwani miezi mitatu iliyo pita  alizaliwa mtoto  huku utumbo ukiwa nje  juu t umbo

No comments:

Post a Comment