TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, April 29, 2013

WASANII BONGO FLEVA WAFUNIKA KAMPENI YA AIRTEL YATOSHA JIJINI MWANZA

17
Wananchi mbalimbali wa mkoani mwanza walijitokeza na kujiuga na Airtel
ili waweze kutumia huduma za Airtel Yatosha Msanii Hiphop anaeshabikiwa kwa wingi Ney wa Mitego akikamua wakati tamasha maalum
la uzinduzi wa AIRTEL YATOSHA mkoani mwanza katika viwanja vya
Furahisha
19 
Wananchi mbalimbali wa mkoani mwanza walijitokeza kwenye tamasha la AIRTEL YATOSHA 20 
Msanii Chipukizi aliyeonyesha kipaji cha hali ya juu kwa kughani
mashairi yenye mvuto kwa miondoko ya HIPHOP wa mkoani Mwanza maarufu
kwa jina la Dogo D alifanya burudani kali katika tamasha maalum la
Airtel yatosha mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha 23 
Msaniii wa Miondoko ya Hip Hop ROMA Mkatoliki akitoa burudani kwa
maelfu ya wakazi wa Mwanza waliofurika katika viwanja vya Furahisha
Mkoani humo kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha
uliofanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mbili mfululizo. Madee akifanya mambo (1) 
Msanii wa Bongo Flava toka kundi la Tip Top Connection lenye makazi
yake mtaa wa Manzese Dar es salaam maarufu kwa jina la Madee
akitumbuiza katika tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel
Yatosha lililofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha
mwishoni mwa wiki hii(Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania)

WASANII wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva)  wamefunika kwa kutoa
burudani ya nguvu kwenye kampeni inayoendeshwa na Kampuni ya Airtel
nchini ya airtel yatosha  na kuwapa raha maelfu ya wapenzi wa muziki
huo waliofurika katika  viwanja vya wazi vya Furahisha Jijini Mwanza.
Kampeni hiyo ya siku mbili iliyofanyika katika viwanja hivyo na
kushuhudia na maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza kupata ushuhuda wa
Airtel yatosha kwa kununua laini za simu za mkononi za Kampuni hiyo na
jinsi ya kutumia huduma ya Internet, kuongea kwa kujiunga na kupata
dakika nyingi za muda wa maongezi kwenda mitandao mingine kwa bei
nafuu zaidi kwa laini moja tu ya Airtel.
Wasanii wa Bongo Fleva waliotoa burudani na kuwaacha hoi maelfu ya
wananchi waliofurika kupitia vibao vyao vinavyotamba kwenye vituo
mbalimbali vya redio na televisheni hapa nchini ni pamoja na Juma
Khasim ‘Nature’ na kundi lake la wanaume halisi, Roma Mkatoliki, Madee
na Ney wa Mitego.
Maelfu ya wananchi walioshuhudia kampeni hiyo waliweza pia kushuhudia
vipaji vya uimbaji kutoka kwa vijana walioshindanishwa na
waliojitokeza kucheza muziki wa Bongo fleva katika viwanja hivyo na
kupata zawadi ya laini na fulana (T-shirt) za Kampuni ya Airtel
zilizotolewa kwa washindi waliopatikana.
“Wananchi wengi wamekuja hapa kupata burudani kutoka kwa wasanii
mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva kama ulivyojionea lakini pia wengi
kwa sasa wanatumia mtandao wa Airtel ikiwemo huduma hii ya Airtel
yatosha pamoja na kununua laini na kupatiwa maelezo ya jinsi ya
kutumia huduma hii”alisema msanii Ney wa Mitego.
Akizungumzia Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Jackson
Mmbando alisema kwamba tangu kuzinduliwa na kufanyika  katika mikoa
sita hadi sasa hapa nchini kumekuwa na mapokeo na mafanikio makubwa
kwa kuongeza wateja wanaotumia mtandao wa Airtel kupitia huduma zote.
Mfanyabiashara wa vituo vya kuuza mafuta Barnabas Mathayo wa Jijini
Mwanza alitoa ushuhuda wa kukubali huduma inayotolewa na Airtel katika
mahojiano maalumu alisema kwamba tangu kuanzishwa kampeni ya Airtel
yatosha amekuwa akinunua kifurushi na kujiunga na kujipatia muda wa
kutosha kufanya mawasiliano na ndugu, rafiki, wavuvi wanao nunua
mafuta kwaajli ya boti zao pamoja na wafanyabiashara mbalimbali
kupitia mitandao yote kwa bei ile ile.
“Huu ni Mkoa wa sita sasa na kama mlivyoshuhudia wingi wa watu
wanaokuja kushuhudia burudani na kupata maelezo ya jinsi ya kutumia
mtandao huu kwa garama nafuu zaidi na ikizingatiwa Mkoa wa Mwanza ni
moja ya mikoa inayojishugulisha na uvuvi, kilimo, ufugaji na
wafanyabiashara kutoka ndani na nchi za maziwa makuu”alisema Meneja
huyo.
“Hatukaangi laini ni moja tu yatosha zingine za nini na ukiangalia
Mwanza ni Mkoa wa burudani, biashara, viwanda, kilimo, uvuvi na
ufugaji hivyo wananchi wake hawana budi kutumia mtandao wa Airtel
ambao umedhamiria kuwainua kiuchumi na kuletwa kwa kampeni hii
itawasaidia kujifunza Airtel kuna nini ndani ya mtandao huu”alisema
Mbando aliongeza kuwa kampeni hiyo inaendelea katika Mikoa ningine na
mwishoni mwa juma hili kampeni hiyo itahamia Jiji kubwa la Dar es
salaam katika viwanja vya Zakhem na kutakuwa na burudani ya kukata na
shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali kutokana na wasanii wengi kuwa
jijini humo na kutoa wito kwa wananchi kufika kushuhudia na kujifunza
ndani ya mtandao wa Airtel kuna vitu gani na kwa gharama nafuuu.

No comments:

Post a Comment