TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 15, 2014

ASKARI MOSES ALPHAGE ALAMBA MILIONI 2 KWA BIDII YA KAZINI

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova (wa tatu toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Askari wa usalama barabarani, Moses Alphage (wa pili kushoto) aliyeibuka kidedea kwenye programu ya kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalama barabarani jijini Dar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio na kujishindia Sh milioni 2. Wa kwanza kushoto ni Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Albert Maneno na kulia ni mtangazaji wa Clouds Said Mohamed maarufu Bonge.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akimkabidhi Askari wa usalama barabarani, Moses Alphage fedha taslimu Sh. milioni 2 zilizochangwa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wasikilizaji wa kituo cha Redio Clouds FM kupitia programu ya kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalama barabarani jijini Dar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio. Alphage huongoza magari katika daraja la Mlalakuwa, Kawe.
Askari wa usalama barabarani, Moses Alphage, akiondoka zake kwa mwendo wa kikakamavu mara baada ya kukabidhiwa cheti na pesa taslimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 2 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova (hayupo pichani). 
Mfanyaakazi wa Idara ya Masoko wa Kampuni ya Vodacom Albert Maneno (wa tatu kushoto) akiongea kabla ya kukabidhi Sh. milioni 2 kwa askari wa kikosi cha Usalama Barabarani Moses Alphage (wa kwanza kushoto) aliyeibuka kidedea katika programu ya kuibua hamasa ya kazi kwa askari hao jijini Dar es salaam iliyoendeshwa na kituo cha Redio Clouds FM. Fedha hizo zimetolewa na wafanyakazi wa Vodacom pamoja na wananchi mbalimbali walioguswa na programu hiyo. Wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova, akipokea sh. milioni 2 kutoka kwa mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Albert Maneno zilizochangwa na wafanyakazi wa Vodacom na wananchi mbalimbali kwa ajili ya askari wa kikosi cha usalama barabarani Moses Alphage aliyeibuka kidedea katika programu ya kuibua hamasa ya kazi kwa askari hao jijini Dar es salaam iliyoendeshwa na kituo cha Redio Clouds FM.

No comments:

Post a Comment