TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, March 11, 2014

Zaidi ya watu 70,000 wamepatiwa mafunzo ya kukuza na Kutambua uwezo wao

Peak-Performance-Logo_0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 10, 2014 Daressalaam, Peak Performance kama kampuni ya kimataifa katika nyaja ya kubadilisha mitazamo ya watu imepata mafanikio makubwa katika eneo la kuongeza tija ya rasilimali watu kwa kuwapa mafunzo zaidi ya watu 70,000 ndani ya miaka takribani 10 ya utendaji hapa Afrika ya mashariki, kusini,Misri na Ethiopia.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosambazwa kwetu, Mkurugenzi Mkuu wa Peak Performance International Tanzania, PPIT bwana Philemoni Kisamo amesifia mafanikio hayo na kusema wataendelea kujikita katika kuwajengea watu na kutambua uwezo wao barani Afrika.
“Tumekuwa tukisaidia makapuni na watu binafsi kutambua na kutumia uwezo wao wote kwa miaka kumi sasa. Programu zetu zimepata mafanikio makubwa kutoka kwa watu ambao tumewahudumia. Tutaendelea kuhubiri dira yetu ambayo ni kuwawezesha watu wa Afrika na zaidi kuwa na ujuzi ambao utawafanya kuamsha matamanio yao ili kutambua uwezo wote walionao” alisema bwana Kisamo.
Aliongeza kuwa utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Jukwaa la uwakala wa ajira la nchini Marekani, Jobvite unaonesha kuwa asilimia 51 ya wafanyakazi walio ajiriliwa Marekani  aidha wanasaka ajira kwa nguvu zote au wako na bahasha mikononi wakitafuta ajira mpya. Katika Utafiti huo wanaume ndio wanaongoza kusaka ajira zaidi ya wanawake kwa asilimia 60 kwa 40.
Kuna sababu nyingi ambazo zinapelekea hali hiyo hapo juu ila ukosefu wa umoja, kutokufanya kazi kama timu, kutokuridhika kwa wafanyakazi, Mpangilio wa kampuni na utamaduni zinatajwa kuwa miongoni mwa visababishi.
“Taasisi na makampuni inabidi waone umuhimu wa kuwasaidia wafanyakazi wake kutambua uwezo mkubwa ulio ndani yao. Utafiti unaonesha kuwa asilimia 80 katika mafanikio yanatokana na saikolojia ya mtu na asilimia iliyobaki, 20 ndio inapatikana kwa kutumia nguvu za mwili.
Aliendelea kusema,Makampuni na Taasisi inabidi waliangalie hili kwa jicho la tatu kwa kuwapatia mafunzo  wafanyakazi wake iliwatumie uwezo wote walio nao ndani yao.” Bwana Kisamo alihitimisha.
KUHUSU PEAK PERFORMANCE INTERNATIONAL (T) LTD
Peak Performance International (T) LTD ni kampuni inayoongoza Afrika mashariki kwa kubadilisha watu ili kukuza uwezo wao na kuutumia.Dira ya Kampuni ni kuwawezesha watu wa Afrika na zaidi kuwa na ujuzi ambao utaamusha matamanio ya kutumia uwezo wao ipasavyo. Tumejikita katika kufundisha   watu binafsi na makampuni ilikuwabadili kwa uwezo wetu wa miaka kumi sasa katika tasnia ya kuendeleza uwezo wa watu. Tumehudumia watu tofauti tofauti katika makampuni mbalimbali kama vyombo vya habari, Mawasiliano,benki, Bima,Serikali n.k
Kwa Mawasiliano zaidi
Ngwegwe Mussa
Afisa Maendeleo ya Biashara na Uhusiano
Peak Performance International (T) LTD
P.O.BOX 77037
Simu ya mezani: 255222781012
Simu ya Mkononi: 0658778670
Tovuti; www.peakperformance-int.com

No comments:

Post a Comment