TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, March 11, 2014

NMB YAPIGA HODI KWA WAKAZI WA BUZURUGA

NMB yazindua rasmi tawi la Buzuruga mkoani Mwanza .Tawi hili likiwa ni tawi la tisa kuzinduliwa katika mkoa huo, huku NMB ikiendelea kuwa ndio benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania.
1 (1)Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bw. Baraka Konisaga akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Buzuruga. Wanaoshuhudia uzinduzi huo kutoka kushoto ni Naibu Meya Jiji  la Mwanza mhe. John Minja, Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Bw. Halifa H. Hidana kutoka kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Bw. Straton Chilongola, Meneja Tawi la NMB Buzuruga, Gadiel Sawe na Meneja Mawasilianowa NMB, Josephine Kulwa.
 Akizungumza katika sherehe ya ufunguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga ameipongeza benki ya NMB kwa hatua nyingine iliyopiga kwa kusogeza zaidi huduma kwa wateja na kuitaka iendelee kuwa kinara wa huduma za kibenki nchini.
Aliwahamasisha wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi waitumie fursa ya kuwepo kwa tawi la NMB  Buzuruga kukidhi mahitaji yao ya kibenki. Vilevile, aliwasihi wananchi waache kuweka fedha kwenye chaga za vitanda na badala yake watumie njia salama ya kuweka fedhabenki. 
“Ni matumaini yangu kuwa uwepo wa tawi hili la Buzuruga ni neema kubwa kwa wakazi wa Mabatini, Buzuruga, Nyakato, Igoma, Kishili, Buswelu na hadi Kisesa hasa wafanyabiashara katika hizi mashine za mpunga kwani kesi za watu kuporwa fedha majumbani au maofisini zitapungua badala ya kuongezeko kwasababu wateja wanaofungua akaunti ndio itakua habari ya eneo hili” alisema Konisaga.
3 (1)Kikundi cha Bujora kikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi huo.
Kwa upande wake, Bw.Straton Chilongola, ambaye ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, alisema “Tangu kuanzishwa kwa tawi hili tumeshuhudia wakazi wengi  wakija kufungua akaunti na kutumia huduma za benki hii. Hii ni uthibitisho kuwa wakazi hawa walikuwa na kiu ya kupata huduma za kibenki karibu na milangoni kwao. Lakini pia tutaendelea kubuni mbinu mbalimbali zitakozotuwezesha kuwafikia wateja wetu karibu zaidi ili kuondoa msongamano kwenye matawi na pia kuokoa muda wa wateja ili waweze kutumia muda wao kwa shughuli endelevu.”
Tawi hili la Buzuruga, linatoa huduma zote za kibenki, ikiwa ni pamoja na huduma ya mikopo ya aina mbalimbali bila kusahau mikopo ya Kilimo.
Tawi hili litakuwa wazi kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi  jioni ( 2:30 asubuhi  – 10:00jioni) na Jumamosi kuanzi saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (2:30 asubuhi – 6:30 mchana), Jumapili na siku za Sikukuu hakutakuwa na huduma ndaniyatawihili.
NMB daima benki yako!

No comments:

Post a Comment